Changamoto za biashara za mitandaoni

Thad

JF-Expert Member
Mar 14, 2017
13,353
31,475
Watanzania hatujabaki nyuma katika biashara za mitandaoni japo sio kwa kiasi kikubwa sana lakini si haba nasi tunajikongoja mdogomdogo. Nasema tunajikongoja kwasababu walio wengi tunatumia zaidi mitandao ya kijamii kama jamiiforums, facebook, instagram, badoo n.k

Ni vyema sasa tukaelezana changamoto mbalimbali zinazowakabili wauzaji na wanunuzi wa bidhaa zinazonadiwa na kuuzwa mitandaoni kisha tujadili namna bora ya kutatua au kukabiliana na changamoto hizo.

Moja kati ya changamoto za biashara hizi ni ukosefu wa uaminifu. Wauzaji na wanunuzi hawaaminiani kwasababu hawafahamiani kabisa. Hiyo inawafanya wasiaminiane hivyo kuifanya biashara kuwa ngumu.

Pili ni changamoto ya ukosefu wa internet ya uhakika. Kuna baadhi ya maeneo internet ni ya shida hivyo inakuwa ngumu kufanya biashara za mitandaoni. Hali hii hupelekea kuwa na laini nyingi za simu japo wakati mwingine bado haisaidii.

Tatu, wizi wa kimtandao. Mfanyabiashara ya kimtandao hulazimika kutoa namba yake ya akaunti kwa wateja mbalimbali kwaajili ya malipo. Hali hiyo humweka katika hatari ya kuibiwa kimtandao. Hii ilishawahi kunitokea mteja nilimpa namba ya simu akanitumia pesa kwaajili ya bidhaa kweli nikaona pesa tuliyokubaliana imeingizwa kwenye simu yangu, nikamtumia mzigo. Baadae nilivyangalia salio nikakuta pesa yote aliyokuwa ameiingiza haipo tena. Nilivyofuatilia kwenye kampuni ya simu nikaambiwa pesa ilitumwa kwangu kimakosa hivyo mhusika alirudishiwa pesa yake. Namba ya mteja haikupatikana tena, nikawa nimeliwa hivyo.

Achilia mbali changamoto za kupigiwa simu na mteja kwamba umpelekee bidhaa lakini ukifika mahali mlipokubaliana hapokei simu au anazima simu au anasema ameghairi kununua au analipa pesa pungufu.

Karibuni tushare changamoto nyingine!
 
Yaani uaminifu ni changamoto kubwa sana. Nafikiri kunawezekana kukawa na ubunifu hapa wa ziada!
 
Badoo ni mtandao gani?, je upo hapa Tanzania? na kuna biashara gani inafanyika huko...? Je? Kuna magroup au page za kuuza na kununua na wana-accept transactions kwa bank au mobile money?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom