Changamoto nilizopata wakati wa kupokea kupokea Parcel Posta

Changamoto nilizopata wakati wa kupokea kupokea Parcel Posta

byakunu

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
622
Reaction score
1,400
IMG_6650.jpg
Wadau habari zaJioni naomba kuwasema Shirika la Posta kuwa wanacho tufanyia wateja sio haki hata kama wapo kutimiza wajibu wao lakin wakumbuke kuna haki ya mteja coz mteja ndo anawafanya na wao ku survive.

Nimepokea parcel leo niliyonunua online kwa AliExpress parcel gharama yake ni dola 8 lakini wenzangu posta wamenitaka nilipe elfu 11 kama service charge/penalty kwa madai ya kwamba walinitumia Message nije kuchukua mzigo na sikwenda.

Na hapo huo mzigo bado nipelekwe TRA nikalipe na ushuru nikaona hii kwangu ni hasara na gharma ninazolipia ni mara tatu ya gharama ya mzigo nilio nunua nikaamua niwaachie mzigo.

Leo leo tena nimepokea parcel nyingine ilikua ni kioo cha simu, lakini nilichokuta ni kwamba mzigo umefunguliwa yani umechanwa chanwa sana kiasi nikahisi labda walihisi ni madawa ya kulevya yamo ndo wakaamua kufungua mzigo, sasa hapa jamani wadau haki ya mteja iko wapi?

Mzigo unafunguliwa wakati muhusika hayupo, na hata kama mna suspect madawa ya kulevya si mngemuita mteja aje achukue mzigo wake na akifika ndo mfungue package mkague na yeye akiwepo ili kma ana madawa ya kulevya mumkamate pale pale physically?

Hii kitu sio nzuri mnayofanya sio nzuri kwani mzigo wa mtu ukihaaribika kuwajibika hamtokubali, pili mnaharibu trust ya wateja kama sisi wa kununua vitu online sasa tutaacha kununua online na kupitishia posta tutatafuta mashirika mengine au njia zingine na hapo mtakosa makusanyo mnayochukua kwa nguvu bila kujali wateja,

Pia mbali na hapo mnaharibu biashara ya wale wanao ship mizigo kuja kwetu inaonekana mizigo ikifika TZ inakuwa na complain nyingi hiyo itafanya wale dealers nao kutofanya biashara na sisi kwa sababu tuna changamoto za kipuuzi nyingi sana hususani katika ku deliver mizigo. Watu wana dai refund online na mzigo kwenye tracking unaonesha upo held by customs, maana yake kikwazo kipo customs na posta.

Lalamiko langu lingine mmekua na tozo zisizo za wazi na zilizo zidi kiwango kiasikwamba mteja hajui gharama ya kulipia kabla ya kuchukua mzigo wake, na pia ili ku facilitate business kuna vimizigo vingne mnatakiwa mcharge pesa ya service fee tu na iwe constant kama 2000 au 15000 inatosha kuto waumiza wananchi na itawapa nafasi ya kugenerate income zaidi kwani hamsumbui wateja wenu.
 
Mkuu unanipa hofu maana na mm niliweka order yangu mpaka delivery time imekwisha na sijapokea info kama mzigo umefika bongo nahisi ni janja yao na mie wani toze izo penalty ah mm nitawaachia kamzigo kenyewe
 
Mkuu nimekusoma mara ya pili, nimefunduaa huenda hata na mie vi mizigo vyangu vimekwama posta imagine nili wekanorder since december 2020 mpaka leo sijapokea lkn delivery time ya mizigo yote miwili ilishapita nika mwambia yule seller akaongeza protection time ila bado mpaka leo hamna kitu ...najishauri niende posta kuulizia kama kuna mizigo imewasii
 
Back
Top Bottom