Changamoto makazini (sekta binafsi na serikalini)

Changamoto makazini (sekta binafsi na serikalini)

Medicci

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2016
Posts
553
Reaction score
917
Nilipata Bahati ya kuajiriwa, na Nina miaka sita kazini.
Toka nimeanza kazi nilikutana na changamoto nyingi kweli.
Ya kwanza kabisa nilikutana nayo kabla hata sijapata kibarua.

1.UNDUGU.
Kipindi natafuta kazi sikuwahi kuwa na Godfather(MTU wa kunikingia kifua). Kuna wengi walikosa hichi kibarua sababu tu hawamjui yeyote pale. Namshukuru Mungu nikapata kibarua changu.
Lakini Mengi yakabadilika baada ya Magufuli kuingia madarakani, fairness ikawepo kwenye interview na upendeleo kuonekana kupungua au kuisha kwa kiasi chake.

2. KUKATALIWA.
Hili Mara nyingi huwatokea wale ambao waliingia kimiujiza au kibahati, nikimaanisha wale wasiokuwa na Godfathers. Huwa Mara nyingi wanajituka wakitengwa na wale waliowakuta, hao hujiita wahenga\wakongwe

3. NETWORK ZA MADILI.
Hapa pia waajiriwa wengi hujikuta wakitengwa na waliowakuta makazini huku kwetu private sectors sidhani kama lipo hili.
Ila hapa ndio pale unakutana na wafanyakazi wanakikundi chao ni wanapiga dili mwanzo mwisho na hutaweza kuwashtukia kwa lolote.
Lakini solution ya hili nikufanya reshuffle kila baada ya muda Fulani.

4.NGONO au RUSHWA YAKE.
Hii huwatokea sana Dada zetu kuanzia muda wa usahili mpaka wanakuwa kibaruani, muda wa kupandishwa vyeo nk.

5. OVERWORKING
Kuna mashirika yanawafanyisha kazi wafanyakazi wake mpaka masaa 14 kwa siku, kinyume na sheria ya Ajira na Kazi bila ya kuwalipa nyongeza.

NAWAKARIBISHA WADAU TUJADILI HIZI CHANGAMOTO NA KUZITAFUTIA MAJIBU
 
Back
Top Bottom