Changamoto kwa vyombo vya Habari Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Changamoto kwa vyombo vya Habari Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MtuKwao, Mar 23, 2009.

 1. M

  MtuKwao Senior Member

  #1
  Mar 23, 2009
  Joined: Oct 7, 2006
  Messages: 190
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Watanzania tunashambuliwa kwa mengi, vyombo vya habari ni mojawapo ya zinazotumika. ...

  Magazeti mawili ya The Citizen na The East African yanaandika habari kwa mtazamo na ushabikiaji wa Kenya. Ni vigumu kukuta habari yoyote yenye kuonyesha kwamba Tanzania au Watanzania wana uwezo wa kufanya chochote cha maendeleo. Yanatoa mtazamo wa kuelekea kusema kwamba Tanzania inahitaji msaada kutoka kwa washirika wake wa EAC lakini hasa Kenya! Kila kilicho kizuri kipo, kinafanyika Kenya au na Mkenya au Taasisi ya Kenya.

  Mfano:
  • Prof. Tibaijuka alisoma Upssala (hakitajwi taasisi yoyote ya tanzania);
  The Citizen, East African
  • Wahandisi wa Kampuni pekee Afrika Mashariki iliyotunikiwa ISO 9001:2000 wamesoma nje ya Tanzania (Ghana), The Citizen

  • Meli ya uvuvi haramu ilikamatwa kwa msaada wa wanabaharia wa Kenya, Msumbiji na Afrika Kusini (Watanzania wala hawatajwi) The East African

  • Wanaoua maalbino wamejulikana kirahisi kwa kutumia Interpol

  Mengine nimesahau ...

  Magazeti haya yana mkakati wa kuitangaza na kuiuza Kenya kwenye vichwa vya Watanzania.

  Wanafanikiwa!

  Nenda hoteli za wageni, wanafungulia CNN, nk, ni vigumu kupata habari za kitanzania kupitia luninga ndani ya hoteli hizi...

  We are being brain washed fast!

  Vyombo vyetu vya habari vina majibu kwa maana ya kuweka mtazamo wa Ki-Tanzania?

  Je, hatuhitaji kuzuia upotoshaji wa habari (kwa malengo ya mpotoshaji) k kuwa na waandishi Watanzania (wazalendo) kuandika habari za Tanzania katika gazeti lililosajiliwa Tanzania ....

  ????
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni changamoto nzuri, lakini mifano uliyoitoa ni michache sana ukilinganisha na kazi nyingi zinzofanywa na vyombo vya habari. hayo mengine ambayo hujayatolea mfano (mabyao ndiyo mengi) hayawezi ku-counter balance hoja yako?
   
 3. M

  MtuKwao Senior Member

  #3
  Mar 23, 2009
  Joined: Oct 7, 2006
  Messages: 190
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Inawezekana mazuri yaka-conterbalance hoja yangu! Na vyombo vya habari vinafanya kazi nzuri tu!

  Nilichotaka mimi ni kwa vyombo vya habari kuwa imara kusimamia hoja zetu, hasa kwenye ulingo wa hoja mbalimbali za EAC.
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Ili kuwa na a solid press ya kuweza kujenga magazeti thabiti yatakayoweza sio tu kujibu mapigo hayo, bali pia kuitangaza Tanzania aggressively tunahitaji sio tu waandishi wa habari waliokomaa, bali hata waalimu wa vyuo vikuu waliokomaa.

  Kama hujasikiza nakualika usikilize press conference ya Dr. Mwakyembe, ambaye ni profesa wa siku nyingi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, aliyofanya majuzi.

  Kuanzia profesa mpaka hao waandishi wa habari utaona wote ni wababaishaji tu, ulimbwende mwingi usomi mchache.

  Kama tunataka kushindana inabidi tupandishe kiwango cha elimu.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Mar 23, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Sasa huyo Mwakyembe aliipataje PhD. yake? Si inabidi uitetee mbele ya jopo la mabingwa?
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Nchi ikiwa na Chuo Kikuu kimoja hata standards za kupata PhD zinakuwa lax ili kuhakikisha wanapatikana hao wachache.

  Halafu Mwakyembe naye hata kama anajua ku defend thesis, kutokana na standards za mawasiliano nchini mwetu zilivyo ndogo, hataki/ hawezi kuongea with precision, ndiyo maana anatoa kauli potovu kama "nilikuwa mkurugenzi wa kwanza NBC" bila kuogopa na hakuna hata muandishi mmoja anayeweza kumuuliza kuhusu hilo.

  Kwa hiyo as a nation hatuna zero tolerance na vitu vilivyo substandard, hata ma profesa wetu substandard, waandishi wa habari sub standard, wanafunzi sub standard, mifumo ya elimu sub standard, maji substandard, umeme substandard, marais sub standard, hata mitandao sub standard!

  Na kama rais wetu tunacheka cheka tu.
   
Loading...