Changamoto kwa HESLB : Baadhi ya wanufaika kufikiria kuacha kazi

Binti Msichana

Senior Member
Oct 9, 2016
109
247
Kuna uwezekano kwa HESLB kushindwa kukusanya pesa zake kkutoka kwa wanufaika wa mikopo kwani baadhi yao wameacha kazi baada ya kujikuta wana salio dogo kwenye akaunti zao baada ya makato.

Na waliopo wanafikiria kuacha kazi kwani kipato chao ni kidogo.

HESLB imejiandaa vipi kukabiliana na hali hii ? Ukizingatia chombo hiki kinatekeleza wajibu wake kwa mustakabali wa Taifa ?
 
Popote utakapokwenda kufanya chochote watakupata tu.
 
Kwa kweli ni kuacha tu hamna namna mi nashauri tu wapandishwe watu salary then wakatwe.
 
waongezewe kwa mapato yapi ?Unataarifa halisi za makusanyo baada ya madeni ya kodi kupungua.unajua ufalme unapumulia ICU ?
 
Mimi nimeisha waachia cheki namba yao,maana siwez kuingia darasan na huku eti kwa mwez wameniachia book 20 tu.
 
Dawa ya deni ni kulipa. Lipeni wenngine nao wapate mikopo.
 
Ukiwa kama ni mtmishi unaye katwa hii 15%....huwez kukubaliana na huu unyanyasaji..kwa kweli hali ni mbaya..sikia kwa mwenzako tuu
 
Dawa ya deni ni kulipa. Lipeni wenngine nao wapate mikopo.
Hakuna aliyekataa kulipa, acha chuki. Ng'ombe humlishi majani humpi maji unataka ukupe 20 litres? Ndicho kinachoendelea bongo, miaka 2 hakuna maboresho zaidi ya makato kuongezeka, hata waliomaliza wamebambikiziwa madeni. Tena na penalty juu
 
Duh.....Hatari
 
Hali ni ngumu fanyeni kazi, mnatishia kujamba wakati mna tumbo la kuharisha!! Haya jambeni tuone, Msipolipa wadogo zenu au watato wenu watasomaje??! Acheni u mimi.
 
Back
Top Bottom