Kamanda Francis
JF-Expert Member
- Nov 30, 2013
- 834
- 140
Kwa kauli yake mwenyewe ZZK alias MM na kwa mujibu wa takwimu rasmi za matokeo ya uchaguzi mkuu 2010,Dr Slaa alipata kura nyingi kuliko alizopata Zitto katika jimbo lake la uchaguzi huko Kigoma.Wewe, acha kujishaua, wataondoka kweli, halafu saccos yenu uone kama itapata hata mwekiti wa kijiji nje ya huki Kaskazini! Acheni kiburi!
Mkuu nakupa pole sana lema hajaenda bungeni ili kuwahamasisha wananchi atown wasiende mkutano wa amani matokeo yake wananchi wamemchoka wanataka amani asubiri kilio 2015
Hivi nyinyi watoto wa Mtei akili zenu mmefungia kwenye mabegi unaandika hovyohovyo tu alafu unataka great thinker wasapoti utumbo,inaonyesha hata shule hukwenda wewe unamawazo mgando kabisa.
Sawa sisi watoto wa Mtei na wewe mtoto wa Wassira ambae amewajengea mawazo potofu kuwa Chadema ni cha kikabila huku yeye akiwashauri wanawe wajiunge na chama anacho kiita ni cha kikabila.
Shida yako wewe ni kukubali kutumika km Sindano inayowekwa uzi kwa nyuma halafu yenyewe inashona kwa mbele.
Chadema hakitakufa kwa maneno yenu ya propaganda ktk mitandao ya kijamii na magazeti ya kufungia maandazi km uhuru,mzalendo,Dira ya Mtanzania nk.
Endeleeni kujipa matumaini humu mitandaoni huku Chadema kikiendelea kusonga mbele.
Sasa chaga development manifesto itawezaje kuingia ikulu kwa kutumia tu hao watu wachache wapenzi wa mbege!
CCM ni majangili ukiwazuia they take your life.Ni nchi amabayo kujitambulisha nje ni ngumu maana wote tumekuwa mazezeta.
Sasa mkibaki wachaga peke yenu itawasaidia nini?au wachaga wenzenu ndio watawaingiza ikulu? Hii ndio faida ya kuanzisha uzi wakati mbege imekolea kichwani.
Mimi ni wa kiume bwana na sio km wewe unaetumika km Sindano inayowekwa uzi kwa nyuma halafu yenyewe inashona kwa mbele. Kwa hiyo siwezi kujishaua. Huu ndio ukweli km unajua ni Sakos na kwamba itakufa wakiondoka si muachane nayo ife na kwanini utoe ushauri!?
Ni ajabu wewe ambae ni mwana CCM kuionea Chadema huruma badala ya kufurahia kifo chake[Kama ni kweli]. Huu ni ujinga na ni Unafiki kwa kuwa huwezi kuipenda Chadema wakati unaiponda.
Wanatumia Uzezeta wetu kujinufaisha na familia zao kwa rasilimali za nchi kwa manufaa yao.
Fikiri ingekuwa nguvu hii inayotumika kumtetea Zitto na kuikosoa Chadema kwa uwamuzi wake wa kumvua madaraka, ingekuwa inatumika kuikosoa serikali na kuwatetea Watanzania ambao maisha yao yamekuwa ya shida na ya mashaka kwa kutokuwa na uhakika wa milo miwili kwa siku si tungekuwa mbali sana?
Leo serikali inabariki Tanesco kupandisha bei ya umeme.lakini mijitu mingine haioni hayo badala yake wamebakia tu kuhangaika na CHADEMA Kama vile ndicho chenye kuongoza serikali. Uzuri mmoja hata hawa wanaoitetea ccm humu wengi wao nao wanapigika tu km sisi kwa kununua na kulipia bidhaa kwa bei ileile km wengine.