Changa English Medium primary school(Tanga mjini)

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
8,263
13,552
Wakuu heshima kwenu?

Wote tunakumbuka serikali imesema itatoa elimu BURE kuanzia kindergarten mpaka kidacho cha nne kuanzia Januari 2016.
Kuna shule inaitwa Changa English Medium Primary School ambayo ipo kata ya Chumbageni,jijini Tanga,nina rafiki zangu wana watoto wanasoma hapo na wanatakiwa kuendelea kulipa ada ya mwaka ambayo ni 250,000/= na michango mingine 28,000/= kwa kila mtoto.

Sasa tukajiuliza inakuwaje hii shule inayomilikiwa na serikali bado kutaka kulipisha ADA?

Pia kuna idadi ya shule 11 za serikali nilisikia hazita husika na kufutwa kwa ada na michango mingine,JE CHANGA ENGLISH MEDIUM PRIMARY SCHOOL NI MOJAWAPO,mwenye maelezo zaidi atujuze.

Nimeuliza mapema isije ikawa nayo ni "JIPU"

ASANTENI NA HERI YA MWAKA MPYA 2016.
 
Wala usipoteze muda wako kutaka kujua hilo, ukweli ni kwamba hakuna Elimu ya Bure, kitu bora kinataka gharama. Serikali isipolipa, mzazi unawajibika kulipa.
Elimu bure ni siasa tupu.
 
Back
Top Bottom