CHAN 2014: Hakuna mwenye muda nayo...

CHAN 2014: Hakuna mwenye muda nayo...

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,356
Nilifikiri ningekuta uzi wenye updates humu, lakini matarajio yangu yamekuwa sivyo. Pamoja na vyombo vya habari kujitahidi kutangaza kwa usawa michuano hii inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ndani ya bara la Afrika, bado mwitiko wa washabiki umekuwa mdogo ukilinganisha na uzito wa mashindano yenyewe.

Tatizo halipo hapa tu, kwani hata mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya michuano hii inayofanyika nchini Afrika Kusini, Sipho Sithole alikiri kuwa walikuwa na muda mchache wa kuitangaza vya kutosha, kama miezi tisa hivi baada ya kumalizika kwa michuano ya Mataifa ya Afrika 2013 ambayo ilifanyika hapo hapo Afrika Kusini.

Si mara ya kwanza kwa CAF kufeli katika kuitangaza na kuleta hamasa katika mashindano yanayoandaliwa nao, kwani takwimu zinaonesha kuwa kadiri muda unavyosonga, ndivyo mashindano ya soka ya ndani ya Afrika yanavyopungua umaarufu, kuanzia Afcon, Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho na sasa CHAN.

Lipo jukumu kubwa mbele yao, pamoja na kuendeleza soka katika ngazi ya bara, lakini pia kuhakikisha kuwa msisimko wa mashindano ya ndani unarudi kabla haujamezwa kabisha na soka la kigeni ambalo licha ya kuwatoa watu kwenye soka lao, limekuwa chanzo kingine cha mapato kwa vilabu vya Ulaya kutoka kwetu Afrika.
 
Matokeo ya jana Januari 15,
Nigeria 4-2 Msumbiji
Mali 1-1 Afrika Kusini
 
Jana Alhamisi

Zimbabwa 0-0 Uganda

Burkina 1-1 Morocco
 
Jana niliangalia mechi ya zimbabwe na uganda lakin niliishia kukereka tu maana wachezaj wanakosa magoli mpaka inatia hasira. Lakin Uganda ni wazur sana haswa sehemu ya kiungo na niligundua kwamba walistahili kuitoa taifa starz kabisa
 
mchuano hii ni saizi yetu.kwanza tujiakikishie nafasi ya kwenda huku baadae tuitafute nafasi ya michuano mingine
 
Half time: Burundi 1-1. Utamu wa uzi ni pale wachangiaji wanakuwepo, kwa kuwa hawapo nami na-sign out!
 
Tatizo wengi wetu hatupendi kuangalia mpira tunataka kuangalia majina...hili kombe kuna akina Kaseja tu hakuna Demba Ba, hakuna Obi Mickel wala hakuna Yahya Toure nani akae kutizama majina ya ukweli..ndo kinachoendelea
 
Burundi 3 Mauritania 2
mpira umeisha.
Kesho Nigeria vs S.Africa
mechi kali sana hizi
 
Back
Top Bottom