Jimmy George
JF-Expert Member
- Nov 28, 2016
- 1,733
- 1,648
Habari wana-JF
Uchaguzi wa 2015 tumeona ulikuwa na changamoto zake tuliowataka hawakupita na wengine waliowataka walipita. Kila mtu husema chama chake akipendacho iwe CCM au CHADEMA kuwa ndiyo bora lakini kila chama hupewa kasoro zake mara ooooho CHADEMA wanalea fisadi(ingawa hatuna uthibitisho maana hajashtakiwa) na wengine utasikia CCM ndiyo imetusababishia matatizo mengi kama mikataba mibovu,ufisadi na wamesababisha maisha kuwa magumu(hasa awamu hii).
Mi nadhani uchaguzi wa 2020 ni vyema tukachagua chama chochote kidogo mfano ADP,TLP,APPT-MAENDELEO,UDP na vinginevyo ili tuone na wao watafanya kitu gani maana vyama vikubwa tunaona vikiwa na kasoro mbalimbali zinazosemwa na watu mbalimbali kulingana na mitazamo yao.
Tusiogope kwamba nchi itakuwa kama inaanza kwa sababu chama ni kidogo na inabidi kijipange hii sababu sidhani kama ni sahihi maana mpaka wanagombea ni kuwa wamejipanga na wanajua kuongoza. Magufuli mwenyewe kaingia kana kwamba ni chama kipya kimechukua nchi sasa kinasahihisha makosa yaliyopita hivyo tutakuwa tumeshachukua uzoefu wa jins chama kipya kitakavyoongoza.