Uchaguzi 2020 Chama kikichaguliwa kuiongoza Serikali, kikashindwa kutekeleza Ilani yake ya Uchaguzi, nini kifanyike?

UCL

Member
Aug 18, 2020
8
6
Wanaforum, Amani kwenu!

Ilani ya uchaguzi ni mwongozo unaobeba mambo yote yatakayotekelezwa na Chama husika kwa faida ya wananchi kwa kipindi cha miaka mitano (Tanzania). Kwa maneno mengine, Ilani ya uchaguzi ni dira itoayo mwelekeo na utaratibu wa kutekeleza ahadi za chama kwa wananchi.

Katika kipindi hiki cha kampeni, vyama vya siasa vina kazi moja tu ya kushindanisha Ilani zao kwa wananchi ili wachague Ilani inayowafaa. Hii ndiyo dhana halisi ya kuuza sera. Kuwashawishi wananchi wakuchague kwa sababu yako mambo umeahidi kuwatekelezea kwa faida ya maisha yao.

Cha kushangaza, baadhi ya Wagombea wamekuwa wakiuza sera zisizotekelezeka ili mradi tu wachaguliwe. Wanawaadaha wananchi kwa maneno matamumatamu na yenye kutia moyo. Wakishachaguliwa, hakuna wanachokifanya. Bahati mbaya sana wao hurejeana kuomba tena ridhaa ya wananchi ili waendelee kuiongoza Serikali na kuwatumikia wananchi haohao kwa awamu nyingine.

Swali:
Kwa sababu Chama kimefunga mkataba na wananchi na kwa upande wa wananchi wao wametimiza masharti ya mkataba kwa kukipa chama dhamana ya kuiongoza Serikali, inapotokea chama kwa upande wake kimeshindwa kutimiza masharti yaliyomo kwenye mkataba huo, nini kifanyike wadau?
 
Wananchi wengi ni mazwazwa! Huo ni mtaji mkubwa kwa CCM!Ingekuwa 50% wana elimu ya kujitambua basi vyama vingewaheshimu wapiga kura!
 
Nyoosha tu maelezo ndugu mtoa mada! CCM ni kichaka cha uhalifu nchini. Hivyo kinatakiwa kwa namna yoyote kupotea kabisa, ili watanzania tuishi maisha bora, ya furaha na yenye matumaini.
 
Back
Top Bottom