Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) aliyefanya upasuaji nyumbani hakuwa muuguzi

Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) aliyefanya upasuaji nyumbani hakuwa muuguzi

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
352
Reaction score
1,033
Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kimekanusha taarifa zinazomhusisha muuguzi na tukio la kumpasua mgonjwa nyumbani juu ya makochi mkoani Tabora, kikibainisha kuwa mhusika hana sifa wala taaluma ya uuguzi.

Katika taarifa yake kwa umma, TANNA imeeleza kushtushwa na taarifa iliyotolewa hivi karibuni na vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii juu ya taarifa iliyotolewa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akielezea juu ya tukio la mtu anayedaiwa kuwa ni muuguzi aliyemchukua mgonjwa na kwenda kumfanyia upasuaji nyumbani kwake juu ya makochi. Chama hicho kimesema kimefanya ufuatiliaji wa haraka mkoani Tabora na kubaini ukweli tofauti.

Uchunguzi wa awali wa TANNA umebaini kuwa mhusika wa tukio hilo la hatari ni mtumishi wa Idara ya Afya katika Wilaya ya Urambo, anayefanya kazi katika Zahanati ya Kamsekwa. Hata hivyo, imebainika kuwa mhusika huyo anahudumu kwa nafasi ya Mhudumu wa Afya (Health Attendant) na si muuguzi kama ilivyoripotiwa awali.

Soma Mwigulu: Muuguzi Tabora aliyemfanyia mgonjwa upasuaji nyumbani kwake afukuzwe kazi, afikishwe kwenye mkono wa sheria na kufutiwa leseni

“Imethibitika kuwa mhusika aliyefanya kitendo hicho siyo muuguzi na hana sifa wala taaluma yoyote ya uuguzi… kutokana na utambulisho huo, tuhuma hizo hazihusiani na Muuguzi yeyote wala hazioneshi taswira ya utendaji wa Taaluma ya Uuguzi nchini”, imeeleza taarifa hiyo ya TANNA ikieleza kuwa nafasi ya Mhudumu wa Afya ni nafasi inayojitegemea kitaaluma kama ilivyo kwa madaktari na wauguzi wenyewe kwenye sekta ya afya.

Kufuatia mkanganyiko huo wa taarifa, TANNA imetoa wito kwa mamlaka zinazokusanya na kutoa taarifa kwa viongozi wa juu wa kitaifa kujiridhisha kwa kina kuhusu taaluma na nafasi za watuhumiwa kabla ya kuziweka hadharani. Chama hicho kimesisitiza kuwa kuripoti taarifa zisizo na usahihi wa kitaaluma kunadhalilisha wauguzi walio wengi wanaofanya kazi kwa weledi na uzalendo mkubwa.

TANNA imelaani vikali kitendo hicho ikikitaja kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya utabibu na sheria za nchi, kwani kimehatarisha maisha ya mwananchi. Chama hicho kimehimiza mwajiri na mamlaka za kisheria kuchukua hatua stahiki dhidi ya mhusika huyo kwa mujibu wa sheria za nchi.

Aidha, chama hicho kimewasihi wauguzi wote nchini kuendelea kuzingatia miongozo ya utumishi wa umma na kuhakikisha huduma za afya zinatolewa katika maeneo rasmi pekee ili kulinda usalama wa wagonjwa
 
Mwigulu ni mropokaji!
Screenshot_20260216-115515~2.png
 
Waziri anapokea taarifa ambayo Hana uhakika nayi then anatoa hukumu !? Mtu kama huyu hatouza Nchi kweli !?
 
uuguzi~medical attendant, enrolled nurse, registerd nurse, nurse officer utabibu~ clinical assistance, clinical officer, assistance medical officer(hii imefutwa japo baadhi yao wapo vituoni) , medical doctor......
 
PM alipewa taarifa za kukurupushwa na yeye akakurupuka.
Kimsingi aliingizwa chaka. Anatakiwa awashughulikie waliomdanganya then ajifunze kuwa na subra.
Inawezekana mhudumu wa afya alimsaidia mgonjwa ajifungulie nyumbani kwake, kama ambavyo wengi husaidiwa vijijini katika hali ya dharura (pengine kituo cha afya kiko mbali, au mhudumu alikuwa anajua hali ilivyo pale kama vile kutokuwepo kwa nurse/mganga wa zamu) kwa hiyo kaamu kuokoa maisha ya mama na mtoto kwa namna hiyo.
 
💥💥💥Na Hili Linafanyika Sana Kwenye Mazingira Mengi Ya Mbwinde Huko(Vijijini),Na Wanawasaidia Sana Wananchi,,Huyo Wakupita Na Kula Bure Hawezi Elewa Adha Za Namna Hiyo....Unamfuta Mtu Kazi Badala Ya Kutatua Chanzo Kikuu Cha Uboreshaji Zaidi Wa Huduma Za Afya Na Miundombinu Yake Kwa Wananchi Haswaa Vijijini...Kumfuta Kazi Mtu Si Utatuzi Wa Tatizo Husika..Amebwatuka Bila Ufuatiliaji Yakinifu,TANNA Wamemuumba...Yale Yale Ya Mzee Paschal Mayalla...
 
Kwa hio kwa mujibu wa taarifa hii ni kwamba waziri mkuu si mkweli ama ameambia isiyo kweli?
Kama kawaida... Wamemchafua PM
Ukusanyaji na uchakataji wa taarifa ni wa hovyo sana.
 
PM alipewa taarifa za kukurupushwa na yeye akakurupuka.
Kimsingi aliingizwa chaka. Anatakiwa awashughulikie waliomdanganya then ajifunze kuwa na subra.
Inawezekana mhudumu wa afya alimsaidia mgonjwa ajifungulie nyumbani kwake, kama ambavyo wengi husaidiwa vijijini katika hali ya dharura (pengine kituo cha afya kiko mbali, au mhudumu alikuwa anajua hali ilivyo pale kama vile kutokuwepo kwa nurse/mganga wa zamu) kwa hiyo kaamu kuokoa maisha ya mama na mtoto kwa namna hiyo.
Upo sawa inatemegea mazingira ya mgonjwa kaokoa Maisha
Nashauri apandishwe daraja!
 
Kwa hio kwa mujibu wa taarifa hii ni kwamba waziri mkuu si mkweli ama ameambia isiyo kweli?
Uko diplomatis sana.NI kwamba Waziri Mkuu amekurupuka kwa kiherehere cha kujipatia sifa za kisiasa. Ndivyo ulivyopaswa kusema
 
Kuhudumu kwa nafasi ya muhudumu wa afya maana yake ni Nini wataalam wa afya?
Hawa ndiyo wale wanaitwa Health Attendants. Wanasoma kww miezi 6 au mwaka kisha wanaenda kufanya zile kazi za kusaidia hapa na pale.

Sasa kuna wengine unakuta wanakaa mahali, wanapata skills za hapa na pale ambazo zinawahusu wale wenye Professional zao kama Madaktari na Wauguzi.

Sasa sio kitu kibaya kupata skills za hapa na pale, ubaya unakujaga wanapoanza kutoka nje ya sheria na taratibu za ufanyaji kazi hizo.

Na kwa kuwa hawako licensed kama wataalamu wengine wa afya, basi mara nyingi ndiyo huwa wanajificha kwenye kichaka cha "WAUGUZI".
 
Back
Top Bottom