Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) waunga mkono juhudi za Waziri Kangi Lugola kuhusu dhamana

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
TAMKO KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI JUU YA HAKI YA MTUHUMIWA KUPEWA DHAMANA KATIKA KITUO CHA POLISI

Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) ni chama cha Wanasheria Tanzania Bara kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 307 ya mwaka 1954. Kazi kuu za chama ni pamoja na kutetea na kulinda mazingira ya kazi kwa wanataaluma ya Sheria, kutoa ushauri wa masuala ya kisheria kwa Serikali na Mahakama pamoja na kuwasaidia umma wa watanzania katika masuala yote yanayohusu sheria.

Kwa niaba ya Baraza la Uongozi wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika, Rais wa Chama Wakili Fatma Amani Karume anapenda kumpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Kangi Lugola kwa muongozo alioutoa kwa Polisi nchini Tanzania Jumapili ya tarehe 30 Septemba 2018.

Katika mkutano huo wa hadhara, Waziri alieleza msimamo wa Sheria juu ya haki ya mtuhumiwa kupata dhamana akiwa kituo cha polisi, msimamo huo umekuwa ukikiukwa kwa miaka mingi na baadhi ya Polisi hapa nchini kwa visingizio mbalimbali.

Chama cha Wanasheria kinaunga mkono msimamo wa Waziri wa kusimamia, kutetea na kuishi msingi wa sheria na kinawashauri viongozi wengine wa serikali kuiga mfano huo mzuri. Kwa mujibu wa misingi ya kimataifa ya sheria za jinai haswa nchi za jumuiya ya madola makosa ya jinai ambayo hayana dhamana ni yale yenye adhabu ya kifo au kifungo cha maisha. Hata hivyo kutokana na mabadiliko mbalimbali ya sheria za jinai hapa nchini makosa yasiyokuwa na dhamana yameongezeka ni pamoja na uhaini, mauaji, unyanganyi wa silaha, uhujumu uchumi, utakatishaji wa fedha chafu, ugaidi na uasi ndani ya jeshi la wananchi.

Aidha Chama Cha Wanasheria kiko tayari kumuunga mkono Waziri wa Mambo ya Ndani katika kutoa mafunzo kwa watendaji wa Jeshi la Polisi iliwaweze kutekeleza majukumu yake kwa ueledi huku wakizingatia haki za binadamu na miongozo ndani ya jeshi hilo haswa Police General Orders ambazo zinajieleza vizuri tena kwa kuzingatia haki za binadamu jinsi ya kumkamata mtuhumiwa, kumweka mtuhumiwa kizuizini, kufanya upekuzi na uchunguzi.

Chama cha Wanasheria kimekuwa kikiendesha mradi unaolenga kufanya maboresho ya sheria na kanuni za polisi kwa lengo la kuendesha jeshi la polisi kwa uhuru, ueledi na kwa misingi ya kidemokrasia na kwa kufuata haki za binadamu. Pamoja na mambo mengine Chama kimefanya tafiti na kuandaa machapisho mbalimbali yakiwemo ni pamoja na; Jeshi la Polisi na Serikali Kuu Tanzania: Muundo Madhubuti, Uwajibikaji Ndani ya Jeshi la Polisi, Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya: Mamlaka, Majukumu na Uwajibikaji.

Mwisho, pamoja na kumpongeza Waziri kwa muongozo huo mzuri juu ya haki ya mtuhumiwa ya dhamana akiwa kituo cha polisi, Chama cha Wanasheria kinamshauri Waziri kutoa Waraka wa Serikali juu ya haki hiyo dhamana kwa Polisi wote ili kukazia hitaji hilo muhimu la sheria ambalo limekuwa likikiukwa na baadhi ya watendaji wa wizara yake kwa miaka mingi sasa.

LIMETOLEWA NA

………………………………..
FATMA AMANI KARUME
RAIS CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA
IMG_6506.JPG
 

Attachments

  • TAMKO KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI JUU YA HAKI YA MTUHUMIWA KUPEWA DHAMANA ...pdf
    87.4 KB · Views: 24
Nitakuwa wa mwisho kuamini kama jiwe amekubaliana na msimamo wa Lugolla.
Hana shida kiongozi wetu, kila lililo jema laufurahisha moyo wake na kila lililo baya laukera moyo wake na ndio maana amekua akiomba tumuombee kwani na yeye ni mwanadamu, ana moyo wa nyama kama sisi.
 
Hayo mawili namuunga mkono Lugola
1.Dhamana kutolewa siku zote za wiki
2.kufuta dhana ya kuingia bure na kutoka pesa
 
Kwanini miaka yote hawakwenda kuyapigania mahakamani ili haki ipatikane? au walisubiri tamko la lugola ili wapongeze? Haya bwana chama cha wanasheria..
 
Back
Top Bottom