kilindi yetu
Member
- Dec 4, 2015
- 7
- 1
Huo mjipu ni wa kutumbua kwa kutumia sululu... yani hicho chma kinachefua sana.. mfxxxxxx!Ningekua na uwezo ningetumbua gujipu hugu haraka. Lkn amini ninawaambia ninyi wababe wachache mnaoendelea kuwakandamiza walimu wa nchi hii pamoja na mishahara duni yao, ipo siku mtatumbuliwa tu. Chama gani hakina kuopt out au in? Uanachama gani wa kulazimishana? Babangu tangu aanze ualimu mbona Cwt hamjawahi msaidia chochote? Hata kudai nyongeza ya mshahara serikali imewatia kwapani??? Shame on you
Nimependa Post yako. Na mshahara unaotoka hazina unakatwa na nani na je ukitaka kuzuia makato TTA kwa sasa ambayo mshahara unaotoka wizarani unafanyaje? Mbona kama kuwa TTA siyo optional?Hakuna mtu yeyote au chombo chochote chenye mamlaka ya kukata na kuchukua sehemu ya mshahara wa mtu bila idhini yake.
Mimi baada ya kugundua huu ni wizi nilimuandikia mkurugenzi kumjulisha kuwa SEHEMU YA mshahara wangu unaelekezwa CWT bila idhini yangu na huu ni kama wizi.Nikawaomba CWT makubaliano tuliyoyafanya baada ya kuitwa kwa mkurugenzi,wakadai hawana.
Nikafatilia ndani ya miezi kama mitano ndo mshahara ukaachwa kukatwa.
Wanao ruhusu huu wizi ni halimashauri zetu,kuruhusu mshahara wa mtu kukatwa bila ridhaa ya mtumishi.
CWT hapa Arusha sitaki hata kuwasikia.
Kama chama kimeshindwa kujiendesha,basi viongozi watumie mishahara yao.
Wana hela hadi wanakopesha vyama vya siasa.Walimu sijui nani katuroga jamani majengo kila mkoa yamejengwa benki zimeanzishwa bado mwalimu anakatwa asilimia 3% sijui ya nini jamani walimu inatosha tuamke.chama kwa sasa kinahela nyingi inayonufaisha wachache.
Hivi ni lazima kujiunga ni chama cha walimu CWT au ni hiari maana naona kila mwalimu huwa analalamika juu ya uendeshwaji wa hiki chamaWalimu jitambueni na hiki chama chenu cha walimu Tanzania.jiulizeni kimewanufaisha nini?. na je wale walio staafu umewaona wamefaidika nini na uanachama wao?.michango ya uanachama kila mwezi inakwenda wapi? na je unataarifa gani juu ya miradi ya chama chako hiki?..je chama hiki kimewai kaguliwa mara ngapi?.pia ujiulize uanachama huo ni wahiyari au walazima?????. ukijiuliza maswali hayo utapata jibu kuwa cwt ni jipu uchungu na dhuluma ya dhahiri kwa walimuuu akyeeeeeeeeeeeeeeeee.....JITAMBUE EWE MWALIMU
wakishakukata bila ridhaa yako,wewe unachukua hatua gani?au unaishia kulalamika?mshahara wako ni jasho lako na hakuna mahala katika mkataba wako na mkurugenzi wako kuwa mshahara utakatwa kupewa mtu mwingine bila wewe mwenyewe kutoa taarifa au idhini. sasa kosa mnalofanya walimu ni hili,mkishakatwa mnanyoosha miguu.inabaki kulalamika tu. Ila ukiwasha moto kwa mwajiri wako basi dakika sifuri tu hiyo hela haitakatwa tena.Wanalazimisha kujiunga ukikataa wanakukata kilazima kwenye mshahara wako bila idhini yako.