CWT ni tawi la CCM! Hivyo usitegemee maajabu. Hiyo 2% ya makato kila mwezi, ni wizi tu. Kuna sababu gani ya kuwakata wanachama kwa mtindo wa asilimia?
Na wakati wanatofautiana mishahara! Yaani mwalimu huyu anakatwa elfu 30, mwingine elfu 10! Mwingine elfu 15!! Kama siyo wizi ni nini hiki!! Haishangazi kuona viongozi wa hiki chama wakitumia fedha za walimu kwenda kuangalia mpira wa Taifa Stars kule Cape Verde! Ni kwa sababu wanalindwa na kulelewa na Serikali ya CCM!
Lakini pia hicho chama kinatakiwa kiwatetee wanachama wote kwa usawa! Sasa kwa nini wanachama wote wasikatwe makato yanayo fanana? Yaani flat rate? Naamini aliyepitisha aina hii ya sheria ya kuwakata walimu ada ya hicho chama kwa mfumo wa asilimia, basi alikuwa ni Mchawi au ni mwendawazimu!
Chama kina wanachama lukuki nchi nzima, kina vitega uchumi vya majengo ya kupangisha kila Mkoa! Kina jengo la Mwalimu House Dar es salaam! Kuna Benki ya Walimu! Lakini vyote hivi havitoshi!
Na chakushangaza zaidi, hiyo benki ina matawi Dar es salaam tu kama sikosei! Na wakati wana majengo karibia kila Mkoa nchini! Riba iko juu! Kiasi cha kuwafanya walimu kukimbilia benki za kibiashara kama CRDB, NMB, nk.