Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia Tanzania sha Shangazwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia Tanzania sha Shangazwa

Discussion in 'JF Doctor' started by babuwaloliondo, Mar 18, 2011.

 1. babuwaloliondo

  babuwaloliondo JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Chama cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asilia Tanzania (Chawatiata), kimedai kushangazwa na viongozi wa Serikali kupanga foleni mchana kweupe kupata huduma ya dawa kwa Mchungaji Ambikilile Mwasapile wakati wanapoenda kwa waganga wengine wa kienyeji, huenda kwa kujificha.

  Kauli hiyo imekuja, siku chache baada ya vigogo wengi serikalini kwenda kwa mchungaji huyo maarufu kwa jina la 'Babu' wakiwamo Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustino Mrema na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa. Dawa ya mchungaji huyo imejizolea umaarufu wa kutibu magonjwa sugu kiasi cha kuwafanya hata wagonjwa kutoka nje ya nchi kuja nchini kutibiwa.

  Akizungumza na gazeti la Mwananchi Katibu Mkuu wa Chawatiata, Mittam Magombeka alisema waganga wa tiba asilia wamekuwa wakidharauliwa na hata kuonekana kuwa ni aibu kupata tiba kwao.Jambo hilo alisema limekuwa likiwafanya baadhi ya wale wanaoamini tiba hizo kwenda kwao kwa siri ili wasionekane na watu.
  SUMAYE ATINGA LOLIONDO - Global Publishers
   
 2. mimi05

  mimi05 Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo ya gizani hufanywa gizani na ya nuruni hufanywa nuruni.
   
 3. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Full of ambiguity. Hao hao wanaokwenda gizani ndo hao hao wanajifanya wanakwenda nuruni, tena kwa mbwembe!
   
 4. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mi nashangaa ukigeugeu wetu. tumekuwa tukilaumu na kukebehi watu wanaoamini nje ya sayansi kwa kuwaita watu ambao wanaendekekeza mila potufu na kuwa hawajaendelea. lakini leo watu wanamiminika kwa babu kama nini. Pamoja na msaaada wa babu wa kutibu watu, nampongeza kwa kuweza kutuumbua na majigambo yetu mara ooh, watu wanapenda mitishamba, ooh, elimu haijatukomboa. Tuache unafiki na tuelewe kuwa mgonjwa yeyote anapokosa tiba hawezi kukaa tu afe wakati angeweza kujaribu njia mbadala. Kejeli hizo huja kwakuwa wanao zitoa halijawafika. Leo tumeona kumbe wote ni wanadamu wenye hofu ya kufa na wenye kusaka matumaini kwanjia yoyote. Kwa hili asante babu kutufungua macho. Tuache kejeli kwa wenzetu na lazima tujue sayansi haina majibu yote katika maisha.
   
Loading...