Chama cha NCCR mageuzi kimeomba kukutana na Rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama cha NCCR mageuzi kimeomba kukutana na Rais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, Dec 18, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,943
  Trophy Points: 280
  CHAMA cha NCCR- Mageuzi kimeomba kukutana na Rais Jakaya Kikwete kwa nia ya kutoa mawazo yake kuhusu mchakato wa kutungwa kwa Katibu mpya ya Tanzania, kama ilivyoahidiwa kwa wananchi na Rais mwenyewe mwishoni mwa mwaka jana.

  Aidha, Baraza la Taifa la Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (NGOs) limeomba kukutana na kuzungumza na Rais kuhusu mchakato huo.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, Rais Kikwete ameyakubali maombi yote mawili na ameagiza wahusika kupanga mikutano hiyo kati yake na NCCR-Mageuzi na kati yake na Baraza la Taifa la NGOs.

  Tayari Rais amekutana na uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHDEMA) na ule wa Chama cha Wananchi (CUF) kuhusu mchakato huo baada ya kuwa ameomba kukutana na viongozi wa vyama hivyo.

  Mikutano kati ya Rais na viongozi wa vyama hivyo viwili ilimalizika kwa maridhiano na maelewano juu ya namna bora zaidi ya kusukuma mchakato huo kwa namna inavyofaa kwa mustakabali wa nchi.
   
 2. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Toa habari kamili ndg. Wanataka wakamweleze nini mkuu wa nchi?
   
 3. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tayari Mbatia kisha maliza kazi anaenda kuvuta chake kwa mkulu na kupanga mikakati ili jimbo la Kigoma kusini lirudi ccm kama kutakuwa na uchaguzi mdogo.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  awape msaidizi wake mmoja wamalizane nae.......... ni bora huo muda akutane na vijana wa kitaa kuliko nccr
   
 5. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  eboo..! Is this supposed to info?? Bullshit.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,943
  Trophy Points: 280
  relax..read the heading
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,943
  Trophy Points: 280
  nishatoa mzee
   
 8. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  ndo muda huu maana kafulila ndo alikuwa anawabania . kafulila alishasema kuwa NCCR hatawaweza kwenda kumuona raisi kwa swala la katiba ..kwani hiyo ni ajenda ya chadema hawawezi kuwaiga na haina mantiki kwa NCCR. Kwa kutoka nje tu siku ya mjadala wa katiba tayari walionyesha kuwa wanaupinga mswada huo. Kazi nzuri Mbatia kachukue malipo ya kazi
   
 9. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #9
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Mbatia masaburi yanamuwasha.
   
 10. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #10
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=2]NCCR yawataka mafisadi kuomba radhi[/h]


  Na Joseph Mwendapole
  15th October 2009
  [​IMG]
  James Mbatia.  Chama cha NCCR-Mageuzi, kimewataka washiriki wa ufisadi kuomba radhi kwa makosa waliyoyafanya na kurejesha mali walizojipatia kwa njia zisizo halali.
  Aidha, chama hicho kimewamwagia sifa Watanzania waliojitokeza kupambana na ufisadi na kimesema vitendo hivyo vimeathiri maendeleo ya nchi na sasa vinatishia uhai, amani na usalama wa Taifa.
  Akizungumza na waandishi wa habari juzi kuhusu kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Julius Nyerere, Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia, alisema hivi sasa hakuna sekta ya jamii ya Watanzania ambayo haijaguswa na ufisadi.
  Alisema hata tuhuma za kutafunwa fedha za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni ndogo sana kwani fedha zimekuwa zikitafunwa maeneo mbalimbali.
  Mbatia alisema kwa kutambua kuwa taifa la Tanzania sasa liko katika hatari ya kuangamia kutokana na ufisadi haitoshi bali inabidi kutafakari kwa kina sababu zilizosababisha hali ifikie kiwango hicho.
  "Lazima tung'amue chimbuko lake ni nini ili hatimaye tutafute ufumbuzi uliosahihi ..Mchanganuo wa aina hii utatuzuia kukimbiza vivuri vyetu, kujenga hofu miongoni mwa jamii kwa ujumla na kuchanganyikiwa kila mara fisadi mmoja atakapotoroka mkono wa Sheria ulionyooshwa kumnasa," alisema.
  Aliongeza kuwa ni vyema kujua kuwazomea mafisadi kunakofanywa hivi sasa na mtiririko wa hotuba za viongozi wengi wa kisiasa, kidini na taasisi za harakati za wananchi kukemea ufisadi ni jambo jema na linalotia moyo katika harakati dhidi ya ufisadi.
  Mbatia alisema tahadhari pekee kuwa nchi inaelekea pabaya haitoshi ikiwa kwa hakika yanayofanywa kila siku yanaisukuma nchi kuelekea kwenye shimo linaloonekana mbeleni.
  Katika kupambana na ufisadi, Mbatia alipendekeza iwepo tume ya maridhiano na msamaha ili wale wote walioshiriki katika ufisadi wakiwa viongozi na waathirika wa ufisadi waweze kufika mbele ya tume na kueleza ukweli halisi.
  Alipendekeza Tume ya maridhiano na msamaha itokane na watu wenye hadhi na ambao uaminifu wao hautiliwi shaka wakiwemo viongozi wa dini, wanasheria, wanaharakati na watu mashuhuri katika jamii.  CHANZO: NIPASHE
   
 11. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #11
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mbatia apinga Bunge kuandika Katiba mpya
  Na Elizabeth Zaya  5th February 2011
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia  Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amesema suala la uandikaji Katiba mpya, liko mikononi mwa umma na si Bunge.
  Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

  Alisema wananchi wanatakiwa kujua kwamba, hakuna kitu chochote chenye uwezo wa kufanikisha uandikaji Katiba isipokuwa wao wenyewe.
  "Katiba ni kauli ya umma inayotokana na sauti ya umma. Hivyo, upatikanji wake lazima uwahusishe wananchi wenyewe na sio Bunge wala chombo chochote," alisema.

  Mbatia alisema ili kufanikisha upatikanaji wa Katiba hiyo, lazima Bunge liweke sheria ya mchakato wa namna ya kuandika Katiba, ambayo pia itaweka bayana namna ya upatikanaji wake.

  Alisema sheria ya sasa haijaweka bayana namna, ambayo Katiba inaweza kuwa kauli ya umma.
  Alilitaka Bunge kutochukua mamlaka ya kuandika Katiba bila ya kushirikisha wananchi.

  "Tunaomba Bunge litambue kuwa uundaji wa Katiba uko mikononi mwa umma na tunaliomba lisijichukulie mamlaka," alisema.  CHANZO: NIPASHE
   
 12. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #12
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Kafulila kuwasilisha hoja yake bungeni Jumatatu wiki ijayo

  Na Richard Makore

  28th January 2011
  [​IMG]
  Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila  Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, amesema atawasilisha rasmi hoja ya kuitaka serikali kutoa maelezo kuhusu hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) iliyoliamuru Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kuilipa Dowans Tanzania Limited fidia ya Sh. bilioni 94, Jumatatu wiki ijayo.

  Hoja hiyo pia inaliomba Bunge kukubali kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kwa kushindwa kusimamia utekelezaji wa sera ya nishati na madini na mpango kabambe wa usambazaji umeme na hivyo kusimamia migawo mitatu ya nishati hiyo ndani ya miaka miwili ya uongozi wake.

  Akizungumza na NIPSAHE jana wakati akihudhuria semina elekezi ya wabunge inayooendelea jijini Dar es Salaam, Kafulila alisema atawasilisha hoja yake siku hiyo baada ya maandalizi ya msingi kuhusu uwasilishaji kukamilika.

  Wiki hii mbunge huyo alijibiwa taarifa yake aliyoiwasilisha kwa Spika kuhusu kusudio lake la kutaka kuwasilisha hoja binafsi kwenye mkutano ujao wa Bunge unaotarajia kuanza Februari 8, mwaka huu.

  Kafulila alitaja kanuni za Bunge zinazopaswa kuzingatiwa katika hoja yake binafsi kuwa ni ya 53, ambayo inaeleza masharti ya hoja kupokelewa, kupitishwa na kuamuliwa na Bunge na ya 54 inayoeleza utaratibu wa kuandaa hoja.

  Uamuzi huo wa Kafulila unapingana na kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwamba, hoja yake haiwezi kupelekwa bungeni kwa madai kwamba, suala hilo liko mahakamani.

  Kafulila alimjibu Pinda kuwa hana mamlaka ya kuzuia suala hilo na kwamba, mwenye mamlaka hayo ni Spika wa Bunge.
  Awali, Spika Makinda alisema Kafulila anaruhusiwa kuandaa hoja yake binafsi, ambayo itapitiwa na Kamati ya Sheria ya Bunge iwapo inakidhi masharti hayo au la kabla ya kupangiwa kuwasilishwa bungeni.  CHANZO: NIPASHE
   
 13. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #13
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=2]Mbatia apinga ushindi wa Mdee[/h]


  Na Hellen Mwango  26th November 2010
  [​IMG]
  Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema)  Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia amefungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akiomba mahakama kutengua ushindi wa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), baada ya kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) baada ya kupewa ushindi isivyo halali.
  Kesi hiyo namba 101 ya mwaka huu, ilifunguliwa mahakamani hapo mwanzoni mwa wiki hii ambapo inasubiri kupangiwa jaji wa kuisikiliza.
  Katika pingamizi la msingi, Mbatia anadai kuwa vitendo vya Mdee kutumia lugha ya matusi na kashfa kwa mgombea kuwa ndicho kigezo cha kuchaguliwa kimesababisha kupoteza haki yake ya msingi na katika kuchaguliwa na hivyo kupoteza ushindi.
  Aidha, Mbatia anadai kitendo cha mlalamikiwa kudai kuwa ananyanyasa wanawake kimesababisha kufanya watu wamchague Mdee kwa kigezo cha jinsia. Anadai kuwa Mdee alitoa kauli zisizo na ukweli kuwa mgombea Mbatia analipwa na CCM na kuwa ni mamluki aliyetumwa kudhoofisha upinzani.  CHANZO: NIPASHE
   
 14. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #14
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=2]Kafulila :NCCR-Mageuzi yaunga mkono maandamano ya Chadema
  [/h]


  Na Waandishi wetu
  3rd March 2011

  [​IMG]
  Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na baadhi ya wabunge wa chama hicho, wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe (katikati) na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa (wa tatu kushoto), katika maandamano ya amani ya chama hicho mjini Bukoba jana.  Chama cha NCCR-Mageuzi kimesema kuwa kinaunga mkono harakati za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) za maandamano yanayoendelea nchini ya kupinga malipo ya Dowans na hali ngumu ya maisha.
  Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
  Alisema kuwa hakubaliani kabisa na kauli ya Rais Kikwete kuwa Chadema kinachochea wananchi waichukie Serikali, na kudai kuwa tatizo si chama bali ni Serikali kutotimiza wajibu wake kwa wananchi.
  Alifafanua kuwa, sababu hiyo ndiyo inayopelekea wananchi kushindwa kuvumilia na kuchukua hatua za kufanya maandamano ya amani ambayo Serikali inaona kama ni shinikizo la vyama vya siasa.
  "Tunaunga mkono harakati za Chadema na sisi NCCR mageuzi tupo tunajipanga kuwasha moto kuamsha Watanzania waiwajibishe Serikali yao inaposhindwa kutatua matatizo bila sababu,"alisema Kafulila.
  Aliendelea kusema kuwa kama Serikali itashindwa kutatua matatizo ya wananchi ni lazima kuwe na migogoro kwani tatizo lililopo si umasikini, bali ni waliokalia madaraka kutowajibika.
  Hata hivyo aliitaka Serikali kuachana na mikataba mibovu ya kukodisha mitambo na badala yake ifikirie kununua mitambo mipya, jambo ambalo alisema linawezekana.
  Wakati huo huo, Kamati ya Nishati na Madini imetoa mapendekezo kati ya 30 kwa serikali kuhusu kukabiliana na matatizo ya umeme.
  Mwenyekiti wa Kamati hiyo, January Makamba, aliyataja kuwa ni kuibana migodi iachie angalao megawati 50.
  Pendekezo lingine ni kutaka mtambo wowote uliopo nchini uwashwe.  CHANZO: NIPASHE
   
 15. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #15
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=2]Mbatia apewa siku 21 kujieleza NCCR[/h]


  Na Muhibu Said  6th November 2011
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia


  HalmashauriI Kuu(NEC) ya Chama cha NCCR-Mageuzi, imempa Mwenyekiti wake, James Mbatia, siku 21 kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake na baadhi ya wanachama kwamba, ni pandikizi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndani ya chama hicho.
  Agizo hilo ni miongoni mwa maazimio kadhaa ya NEC yaliyofikiwa kwa kauli moja na idadi kubwa ya wajumbe wa halmashauri hiyo, katika kikao chake kilichofanyika jijini Dar es Salaam jana.
  Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe 50, lakini kinyume cha kawaida, waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuhudhuria.
  Azimio hilo dhidi ya Mbatia lilisomwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Samuel Ruhuza katika kikao hicho na limezingatia kanuni za chama zinazotoa fursa kwa mwanachama mtuhumiwa kujitetea.
  Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zinaeleza kuwa hoja kuhusu tuhuma hizo, iliwasilishwa katika kikao hicho na Mjumbe wa NEC kutoka Tanga, Mbwana Hassan.
  Hoja hiyo imesainiwa na wajumbe 28 wa halmashauri hiyo, ambao kwa kauli moja wanataka Mbatia ajiuzulu uenyekiti wa chama hicho kutokana na tuhuma zinazomkabili.
  Kwa mujibu wa habari hizo, kati ya wajumbe waliohudhuria kikao cha jana, ni wajumbe 10 tu ndio wanaodaiwa kumuunga mkono Mbatia kuendelea kuwa mwenyekiti wa chama hicho, huku wengine waliosalia wakiwa hawana upande.
  Kutokana na agizo hilo, Mbatia sasa anatakiwa kujibu tuhuma hizo na kuwasilisha majibu hayo kwa Katibu Mkuu. Katibu Mkuu baada ya kuyapokea, atawasilisha kwa Kamati ya Maadili ya Chama na kisha kupelekwa katika kikao cha NEC kitakachofanyika Februari, mwakani kwa ajili ya maamuzi.
  Habari hizo zinasema kuwa baada ya azimio hilo kupitishwa na NEC, Mbatia aliomba kutendewa haki kwa kupewa muda wa kutosha kujibu tuhuma zinazomkabili.
  Imeelezwa kuwa awali, viongozi waliokuwa wamekaa meza kuu walijaribu kuzuia hoja inayohusu tuhuma dhidi ya Mbatia kujadiliwa katika kikao hicho. Hata hivyo, idadi kubwa ya wajumbe walipinga hatua hiyo na kushinikiza ijadiliwe.
  Mvutano kuhusu suala hilo uliendelea baada ya Mbatia kugoma kujibu tuhuma zinazomkabili.
  Jambo lingine lililotaka kulipua kikao hicho, ni madai kwamba, kulikuwa na mabaunsa waliokuwa wamekodiwa na baadhi ya wanachama kwa lengo la kutisha wajumbe na kuleta vurugu.
  Hali hiyo ilimfanya Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali, kutishia kuwasiliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema, ili alete askari kwa ajili ya kuwashughulikia mabaunsa hao.
  Mkosamali, ambaye ni mjumbe wa NEC, alifikia hatua hiyo baada ya baadhi ya wajumbe kutaka mabaunsa hao waondolewe, huku baadhi ya viongozi wakipinga suala hilo.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 16. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #16
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=2]Kafulila avuliwa uongozi NCCR-Mageuzi[/h]


  Na Muhibu Said  13th December 2011
  [​IMG]
  Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila


  Mbinge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, amevuliwa Ukuu wa Idara ya Uenezi na Uhamasishaji ya Chama cha NCCR-Mageuzi, kwa kile kilichodaiwa naye kuwa ni kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo mgogoro unaoendelea ndani ya chama hicho.
  Habari zilizopatikana jana, zinaeleza kuwa uamuzi huo ulichukuliwa na Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza, ambaye amethibitisha suala hilo.
  Kafulila alithibitisha jana kupokea barua ya kuvuliwa wadhifa huo ndani ya chama hicho.
  Alisema anaamini uamuzi huo umechukuliwa dhidi yake kutokana na mgogoro unaoendelea ndani ya NCCR-Mageuzi kati ya wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia. Wajumbe hao wa NEC wanataka Mbatia ajiuzulu kwa kutokuwa na imani naye.
  Kafulila alisema pia anaamini uamuzi huo unatokana na baadhi ya watu ndani ya NCCR-Mageuzi kutokufurahishwa na hatua yake ya kuungana na wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kususia mjadala wa muswada wa mabadiliko ya Katiba bungeni.
  Alisema sababu nyingine inatokana na kauli yake kwamba, haoni sababu kwa Chadema na Rais Jakaya Kikwete kukutana na kuzungumza kwani hakuna kitakachotokea katika mazungumzo yao, kwani utamaduni wa NCCR-Mageuzi ni kuzungumza na si kususia.
  Hata hivyo, Kafulila alisema hana tatizo na uamuzi uliochukuliwa dhidi yake kwani nafasi hiyo haikuwa kwake ni jukwaa la kisiasa kulinganisha na ubunge alionao.Alisema pamoja na uamuzi huo, kuna tetesi zinazowahusisha baadhi ya watu ndani ya NCCR-Mageuzi za kutaka kumsukia ajali na kumnyang'anya uanachama. Hata hivyo, alisema hawahofii watu hao kwa vile ni NEC pekee ndiyo yenye mamlaka ya kumvua mwanachama uanachama.
  Kikao cha NEC-NCCR-Mageuzi kinatarajiwa kufanyika Februari 3, mwakani, ambapo Mbatia anatakiwa kujieleza kuhusiana na tuhuma kadhaa dhidi yake zilizomo kwenye waraka uliosainiwa na wajumbe 28 wa NEC.
  Ruhuza alipoulizwa jana na NIPASHE, alisema amechukua uamuzi huo kwa mujibu wa ibara ya 22 (7) ya katiba ya NCCR-Mageuzi, ambayo alisema inampa mamlaka ya kuteua mjumbe wa sekretarieti itakavyompendeza na kumvua na kwamba, amefanya hivyo ili kumpa Kafulila fursa nzuri ya kuwatumikia wapigakura wake.  CHANZO: NIPASHE
   
 17. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #17
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [h=2]Harakati za kumng`oa Mbatia NCCR zakolea[/h]


  Na Muhibu Said  10th September 2011
  [​IMG] Uasi sasa ni dhahiri, ajibu kuwa ukubwa ni jalala  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Chama NCCR-Mageuzi, James Mbatia


  Shinikizo la mkakati wa kumng'oa madarakani Mwenyekiti wa Chama NCCR-Mageuzi, James Mbatia, linaonekana bado ‘bichi', baada ya makada waandamizi wa chama hicho ‘kushikilia bango' msimamo wao wa kumtaka kiongozi huyo kujiuzulu pasipo shuruti.
  Safari hii makada hao wakiongozwa na Kamishna wa NCCR-Mageuzi Mkoa wa Tanga, Mbwana Hassan, wameueleza kinagaubaga uongozi wa chama hicho taifa kuhusu msimamo wao wa kumtaka Mbatia kujiuzulu nafasi hiyo katika chama kwa hiari yake.
  Msimamo wao huo wameuweka wazi kupitia barua ya Septemba 5, mwaka huu, waliyoamwandikia Katibu Mkuu wa Chama hicho, Samuel Ruhuza.
  Barua hiyo iliyosainiwa na Mbwana, yenye kichwa cha habari: "Yahusu: Tuhuma za kuchafua jina la mwenyekiti taifa", iliandikwa kujibu barua ya Katibu Mkuu huyo wa NCCR-Mageuzi yenye Kumbukumbu NCCR-M/MM/KNU/11/01 ya Septemba 2, mwaka huu.
  Ruhuza amethibitisha kuifahamu barua hiyo iliyosainiwa na Kamishna huyo wa NCCR-Mageuzi Mkoa wa Tanga.
  Mbwana katika barua hiyo ya kurasa tatu, anamtaka Mbatia kujiuzulu kwa madai kwamba, amepoteza uhalali wa kuwa mwenyekiti wa chama taifa.
  Anasema kuna vikao vimeshafanyika kumwomba Mbatia ajiuzulu kutokana na kupoteza imani ya wananchi na uhalali wa kuwa kiongozi mkuu wa chama.
  Mbwana anasema yeye ni miongoni mwa wazee waliowahi kukutana na Mbatia na kumshauri ajiuzulu kutokana na sababu hizo.
  Anasema kipindi walichokutana na Mbatia, Ruhuza hakuwapo. Anadai alikuwa mkoani Kigoma.
  Mbwana anasema akiwa na mzee mwingine, walijibiwa na Mbatia kwamba, wajadili suala hilo mbele ya viongozi wengine wa chama.
  Anasema kutokana ushauri huo, walikutana kwenye kikao cha pamoja katika Chuo Kikuu cha Bagamoyo, ambako walikutana na viongozi wakuu wa chama isipokuwa Ruhuza.
  Mbwana anasema kinachomponza Mbatia ni matamko yake mwenyewe na jinsi ambavyo amekuwa akishindwa mfululizo katika chaguzi za ubunge katika majimbo aliyopata kugombea nchini.
  "Labda nikukumbushe tu kuwa huyu mwenyekiti ndiye, ambaye amekifikisha chama hiki mahala kinawatatiza wananchi kutokana na misimamo yake ya kuwa wakili au mtetezi wa CCM na mafisadi," anasema Mbwana akijibu aliyoandikiwa na Ruhuza.
  Kwa mfano, anasema wakati Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa na Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, walipotangaza orodha ya mafisadi mwaka 2007, Mbatia aliibuka na tamko kuwa Watanzania wote ni mafisadi isipokuwa wanatofautiana tu viwango vya ufisadi.
  "Huu ni ushahidi wa kutetea mafisadi wa CCM kwa kutaka kupunguza hasira za wananchi dhidi ya mafisadi," anasema Mbwana.
  Katika barua hiyo pia anasema mwaka 2000 Chama cha Wananchi (CUF) kilikataa kumtambua Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, kufuatia uchaguzi uliotangazwa duniani kote kuwa haukuwa huru na wa haki, lakini Mbatia aliibuka na tamko kuwa kitendo cha CUF kutomtambua Karume kilikuwa ni uhaini.
  "Hii inadhihirisha kuwa mtu huyu alikuwa anafanya kazi ya kutetea ushindi wa CCM," anasema Mbwana.
  Anadai kwenye kikao kimojawapo cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya NCCR-Mageuzi, aliyekuwa mgombea urais kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, Hashim Rungwe, alikijulisha kikao hicho kuwa wakati wa kampeni, Mbatia alimkataza kuisema vibaya CCM anapohutubia mikutano katika Jimbo la Kawe.
  Rungwe, ambaye ni mwanasheria maarufu nchini, alithibitisha madai hayo ya Mbwana, alipohojiwa na NIPASHE jana.
  "Huu ni ushahidi mwingine wa namna mwenyekiti (Mbatia) anavyofanya kazi za CCM," anadai Mbwana.
  Mbatia aliwania ubunge kupitia NCCR-Mageuzi katika Uchaguzi Mkuu jimbo la Kawe mwaka jana, lakini akaangushwa na aliyegombea kiti hicho kwa tiketi ya Chadema, Halima Mdee.
  Mbwana anasema hivi karibuni Mbatia pia alikaririwa na vyombo vya habari akiunga mkono mtazamo wa CCM kuwa wabunge vijana bungeni ni tatizo, hawaelewi walichowatuma na kwamba, inaonyesha hawakuandaliwa kuwa viongozi.
  "Kwa mantiki hizo zote, naendelea kusimamia msimamo wangu kwamba, kwa busara za kawaida, tena pasipo shuruti, James Mbatia angejiuzulu. Kwani amepoteza uhalali wa kuwa mwenyekiti wa chama taifa kwa matamko yake mwenyewe, lakini zaidi kwa namna anavyoshindwa mfululizo katika chaguzi za ubunge," anadai Mbwana.
  Kuhusu kushindwa mfululizo katika chaguzi za ubunge, Mbwana anasema tangu Mbatia achaguliwe kuwa mwenyekiti, hajawahi kushinda hata uchaguzi mmoja aliopata kugombea.
  Anasema kwa mfano, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000, aligombea ubunge katika Jimbo la Vunjo na mwaka jana aligombea Kawe, lakini kote alishindwa.
  "Kila jimbo, ambalo aligombea, watu walikuwa na imani na upinzani, lakini hawakuwa na imani na James Mbatia. Ndio sababu walichagua TLP Vunjo mwaka 2000 na Chadema Kawe mwaka 2010," anadai Mbwana.
  Anasema katika uchaguzi wa Kawe, Mbatia hakutoa ushindani mkubwa, badala yake alishindwa kwa tofauti ya kura zaidi ya 33,000 na Mdee.
  Mbwana adai pia katika uchaguzi wa Kawe, wanawake wa upinzani walionyesha wanaweza kiasi kwamba, kwa mara ya kwanza walitengeneza historia ya kushinda jimbo ndani ya jiji la Dar es Salaam tena kwa kumshinda mwenyekiti wa chama taifa.
  "Hicho ni kielelezo cha uwezo wa mwanamke," anasema Mbwana.
  Anadai katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, wenyeviti wanne wa vyama vya upinzani; John Cheyo (UDP), Augustine Mrema (TLP), Freeman Mbowe (Chadema) na Mbatia (NCCR-Mageuzi), waligombea ubunge, lakini ni Mbatia peke yake ndiye aliyeshindwa uchaguzi.
  Mbwana anasema uamuzi wa Mbatia wa kufungua kesi dhidi ya mpinzani mwenzake katika Jimbo la Kawe, unakinzana na misingi ya maamuzi ya chama kukataa kuweka mgombea katika Jimbo la Igunga ili kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni.
  KAULI YA MBATIA
  Kutokana na madai hayo, NIPASHE jana iliwasiliana na Mbatia, ambaye kwanza alipingana na utaratibu uliotumiwa na Mbwana wa kuendesha chama kupitia vyombo vya habari.
  Alisema iwapo atajibu lolote kuhusiana na madai hayo kupitia vyombo vya habari, atakuwa anatenda kosa alilosema kuwa limetendwa na Mbwana.
  Hata hivyo, alisema kawaida mwenyekiti katika taasisi yoyote huchukuliwa kama jalala, hivyo iwapo atazungumzia lolote kuhusu madai yaliyotolewa na Mbwana dhidi yake, ataonekana anajitetea.
  "Kwa hiyo, ili kutenda haki, nakuomba uwasiliane na Katibu Mkuu," alisema Mbatia.
  KAULI YA KATIBU MKUU
  NIPASHE iliwasiliana na Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Ruhuza, ambaye kwanza alithibitisha kuifahamu barua hiyo ya Mbwana.
  Hata hivyo, alisema yanayoelezwa na barua hiyo ya Mbwana yanatofautiana na yale aliyotakiwa kuyajibu kwenye barua aliyomwandikia.
  "Barua aliyoandikiwa inazungumzia tuhuma dhidi yake, alichozungumza yeye kwenye barua yake ni tofauti," alisema Ruhuza.
  Alisema viongozi wa chama hawajawahi kukaa kikao chochote kumjadili Mbatia na kwamba, madai yote yaliyotolewa na Mbwana, hawezi kuyajibu kupitia vyombo vya habari, badala yake alisema: "Tutakutana kwenye kikao."
  Alisema jedwali la makosa na adhabu kwa mujibu wa kanuni za nidhamu na usuluhishi namba tano na sita za chama, limeweka utaratibu kwamba, tuhuma dhidi ya kiongozi wa chama au mwanachama, zijadiliwe ndani ya utaratibu wa vikao vya chama na si kwenye vyombo vya habari.
  Ruhuza alisema kanuni hizo zimewekwa baada ya kujifunza kutokana na migogoro iliyowahi kukikumba chama katika miaka ya 1990 na kukiathiri chama.
  Alisema kwa kiasi kikubwa migogoro hiyo ilichangiwa na watu kuwa na tabia ya kuzungumzia masuala ya chama kwenye vyombo vya habari.
  "Hivyo, Mbwana kuongelea kwenye magazeti mambo ya chama anavunja kanuni. Alichokifanya ni makosa kwa sababu chama chetu kina utaratibu wa vikao. Pia kumtuhumu kiongozi au mwanachama nje ya vikao ni kashfa na adhabu yake ni karipio au kufukuzwa uanachama," alisema Ruhuza.
  Hata hivyo, Mbwana alipingana na kauli ya Ruhuza, akisema Katiba ya NCCR-Mageuzi, haijampa haki Katibu Mkuu wa chama kumtuhumu au kumuadhibu.
  Alisema yeye (Mbwana) ni mjumbe wa NEC, hivyo kama Ruhuza ameona ana makosa, anachotakiwa kukifanya ni kumshtaki NEC na si vinginevyo.
  Mbwana alisema anachokifanya ni kutekeleza haki yake ya kimsingi ya kidemokrasia, ambayo inazingatia uwazi unaohimizwa na chama chake siku zote.
  Alisema amelazimika kuzungumzia masuala ya chama kwenye vyombo vya habari, kwa kuwa suala la kumtaka Mbatia ajiuzulu alitumwa na wanachama, hivyo ameona awarudishie majibu kuhusu maendeleo ya kazi aliyotumwa kuifanya.
  Mbwana alisema kitendo cha Ruhuza kumwandikia barua hakileti tafisiri nyingine zaidi ya vitisho ili abadili msimamo wake, kitu ambacho alisema hawezi kukifanya.
  KAULI YA RUNGWE
  Naye Rungwe alipoulizwa kuhusu madai kwamba, aliwahi kukatazwa na Mbatia kuisema vibaya CCM anapohutubia mikutano katika Jimbo la Kawe, alisema suala hilo alikwisha kuripoti kwenye kikao cha NEC kilichofanyika kati ya Februari na Machi, mwaka huu.
  Alisema kila mjumbe analifahamu vema suala hilo, ingawa alisema halikujadiliwa kwenye kikao hicho cha NEC.
  "Huyu bwana (Mbwana) anaquote (ananukuu) tu nilichoripoti kwenye kikao cha NEC.
  Makada kadhaa wa chama hicho wanadaiwa kuunda mpango wa kumng'oa Mbatia kwa madai kuwa ni pandikizi la CCM.
  Makada hao wanasema Mbatia amepoteza mvuto wa kisiasa na amekuwa akitofautiana na wanamageuzi wenzake katika mambo ya msingi yanayokihusu chama hicho kitaifa.  CHANZO: NIPASHE
   
 18. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #18
  Dec 19, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160


  Hapo Mbatia anaenda kumweleza m/kiti wa chama chao kwamba wanaweza kuendelea na mada yao ya cameron maana yule "Kichomi" aliyekuwa anawasumbua amesha"fulia!"
   
 19. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #19
  Dec 19, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Duh! Masikini Daudi Kafulia!
   
 20. w

  wabusara Member

  #20
  Dec 19, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika unaonekana kufikiri kwa kutumia masaburi,tafuta hoja nyingine kwani tayari kafulila ameshaondoka na maji,na inajulikana kuwa wewe ndiye ulifanywa kuwa kinara wa kuripoti tarifa ktk gazeti la nipashe zinazohusu nccr kama sehemu ya kumwezesha kafulila ambaye ni kibaraka wa ccm ili afanikishe ujio wa wale wana ccm wenzake,mwehu weweeeeeeee,sasa kafulila kfulia na wewe utafulia na utamrejeshea kila kitu alichokupatia,ondoka na masaburi yako
   
Loading...