Chama Cha Mapinduzi (CCM) tusaidieni

Ngaliwe

Senior Member
Dec 30, 2015
161
364
1. Nchi imegawanywa katika makundi makubwa mawili. Kundi la kwanza linaongozwa na Viongozi wenye kuona kuwa JPM hakua mtu sahihi. Hawa wengi ni majeruhi wa Uongozi wa JPM kwa namna moja ama nyingine, wengi miradi yao haramu ilikufa. Kundi la pili linaunganisha wananchi wengi walioguswa na uongozi wa JPM. Hawa wanaona hospitali zimejengwa na huduma za afya zimesogea, watoto wanasoma bure, wanapata maji, umeme, barabara zinafikika, masoko, uhuru wa biashara. Wanaona kwa macho miradi mikubwa imejengwa ikikamilika itawasaidia na mambo mengine mengi. Nchi inakwaruzana CCM kimya, ipo kama haioni, haiwaonyi viongozi wake wala kutoa muongozo wowote.

Utaratibu huu ukiendelea nchi itapasuka, wananchi hawatakubali kwa namna yoyote miradi iliyoasisiwa na JPM isifike mwisho kama anavyoshauri Muhongo, wananchi hawatakubali kunyanyaswa tena na wawekezaji kwa kisingizio cha kuwavutia kama ambavyo imeanza kutokea, Machinga na Mamantilie hawakubali shuruba katika biashara zao, nk.

Ushauri kwa CCM.

Nimekwishashauri, nashauri tena. CCM iitishe Kamati Kuu ya dharula isingoje Mkutano Mkuu wa April 30. Iitishe Kamati Kuu itoe kauli na muongozo, iwapige marufuku Viongozi wake kuendeleza mjadala huu hasa Bungeni. Serikali hii ni ya CCM, kuendelea kujibishana huku tutatofautiana kauli. Endapo Viongozi wakishinda kwa sababu ya madaraka yao wananchi tutaisubiri CCM ifikapo 2025 tuiadhibu. WanaCCM wengine tutaungana na Wananchi kuiadhibu CCM kwa sababu itakua imetaka yenyewe. JPM anaweza kuwa sababu ya CCM kufa au kubadilika, na kuimarika zaidi. Hakuna shortcut, CCM tusaidieni.

2. Serikali imekubali kuendelea kujitukana yenyewe. Bunge linaikashifu Serikali, CCM yenye Serikali na Bunge ipo kimya. Spika wa Bunge kusema kuwa Rais Magufuli hakushauriwa vizuri kuhusu mradi wa Bagamoyo maana yake Bunge limesema Rais hakushauriwa vizuri. Washauri wa Rais ni Makam wa Rais, Waziri Mkuu na Baraza la Mawaziri. Kwa kauli ya Ndugai (Bunge) maana yake ni kwamba aliyekuwa Makam wa Rais wakati wa Rais Magufuli hakutimiza wajibu wake sawasawa, aliyekua Waziri Mkuu wakati wa Rais Magufuli na Baraza lote la Mawaziri hawakutimiza wajibu wao.

Huku ndiko kunaitwa kutokua na imani na Serikali kwa mujibu wa Katiba. Maana yake kwa kauli hiyo Bunge halina imani na Serikali na Serikali inapaswa kuanguka. Aliyekuwa Makam wa Rais ndie Rais sasa, aliyekua Waziri Mkuu ndie Waziri Mkuu sasa na karibia lililokua Baraza la Mawaziri lote ndilo Baraza la Mawaziri sasa. Kwa kauli ya Ndugai (Bunge) watu wote hawa hawafai, hawastahili kuwepo kwa sababu hawawezi kutumiza wajibu wao ipasavyo. Kwa nchi ya watu wastaarabu Serikali ilipaswa kuvunjika yote tangu kauli ya Spika ilipotoka au Spika wa Bunge alipaswa kuwajibika kwa kuichafua Serikali. CCM inaona vyombo vyake vinachafuana ipo kama haipo.

Ushauri kwa CCM.

CCM ivunje Serikali yake au imuwajibishe Spika wa Bunge. Ni rahisi mno, CCM iwaelekeze Wabunge wake kupiga kura ya kutokua na imani na spika kwa kuichafua Serikali au kama Spika yuko sahihi CCM iwawajibishe Wanachama wake Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Kassim Majaliwa na Waziri wa fedha wa wakati huo (Makam wa Rais wa sasa) kwa kushindwa kumshauri vizuri Rais wa Nchi na kwa uzembe huo Serikali inaweza kupata hasara kubwa. CCM ikiwawajibisha watu hawa, kwa kuwaondolea Uanachama, Serikali itaanza upya. Tume itaitisha uchaguzi mpya!! Tunafunga mjadala.

CCM ikiendelea kulea tatizo hili litakapokuwa sugu ijiandae kupata hasara kubwa mbele ya safari. Nchi haiwezi kwenda kwa namna hii ikizozana asubuhi hadi jioni, marehemu akichafuliwa bure. Nchi inajua Magufuli amefanya mambo makubwa kwa kipindi kifupi mno kuliko yeyote na haitarajiwi mwingine yeyote kumfikia. CCM ilinde heshima hii isiharibiwe. Aliyekuwepo na aliyepo wote ni CCM, Bunge na Serikali vyote ni CCM. CCM ndio yenye wajibu na Nchi hii hivyo ni lazima tuchukue hatua mapema za kudhibiti dalili hizi zenye kujenga uhasama katika Nchi. Imeandikwa; Usipoziba UFA utajenga UKUTA.

Veronica France

Screenshot_20210407-213308_Instagram.jpg
 
Viongozi wanaotaka kuleta hicho kitu unachokiita mgawannyo ni wachache sana dhidi ya kundi kubwa la wenye nchi.
Hii inatusaidia tu kujua ni nani alikuwa amepunguziwa 'mrija' kwa maslahi ya wengi.
Mkuu siku zote ukimya nalo huwa ni jibu zuri tu.
 
Hayana budi haya kutokea ili taifa hususani ccm waone umuhimu wa taifa kuwa na mifumo na taasisi imara.
 
Chama chako kilikumbatia propoganda kuliko ukweli hayo ndio matokeo yake sasa
 
CCM iwatambue waliopingana na magufuli kule jimboni.

Wengi aliwasweka lumande kwa uhujumu uchumi.

Hadi Leo wapo lupango, tiss mwbieni DPP au maza awaachie huru.

Hayati alikuwa mbabe sana.
 
Back
Top Bottom