Chama cha Mapinduzi (CCM) ni chama cha ajabu sana

Chama cha Mapinduzi (CCM) ni chama cha ajabu sana

Kwa hiyo wahuni wakikuchomea nyumba unakosa sifa za kuongoza?

Au shida ni kesi ya mwanae ambaye naye ameshinda hadi rufaa!

NB: Binti wa Ditopile ni kiongozi mahali, kijana wa Said Mwamwindi pia alikuja kuwa kiongozi huko Iringa.
 
Thomas Ole Sabaya leo Jumatatu Desemba 4, 2023 ameibuka mshindi katika nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha baada ya kupata kura 463 na kuwazidi wapinzani wake watatu.

Sabaya aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti ambae pia ni baba wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amefanikiwa kushinda kiti hicho katika uchaguzi mdogo wa nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Steven Zelothe ambaye alifariki dunia.

Msimamizi wa uchaguzi wa CCM, Anthony Mtaka, amesema walitarajia wajumbe 1,001 wapige kura lakini waliofanikiwa kutumia haki yao ya msingi ni 906.

Alisema kuwa wagombea wanne waliteuliwa na kupigiwa kura ambapo Sabaya ameshinda kwa kura 463 akifuatiwa na Daniel Palangyo aliyepata kura 374 huku Solomon Kivuyo akipata kura 59 na Edina Kivuyo akipata kura 10.

(Imeandikwa na Bertha Ismail)

#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa

Huyu mzee aliwahi kuchomewa nyumba na wananchi Ngaramtoni Arusha kwa roho yake mbaya. Ati leo mwenyekiti.

Huyu ni baba yake na yule alie kuwa Dc wa Hai.

Kwa CCM ya sasa, hasa kuanzia awamu ya 5, ukatili na tabia nyingine za hovyo hovyo, ni mojawapo ya sifa kubwa zinazohitajika katika chama.

Angalia majitu ya hovyo, makatili yalivyopanda katika uongozi wa CCM na Serikali, hasa wakati wa awamu ya 5, na sahizi yanarudishwa ili yawe tegemeo la chama.
 
Back
Top Bottom