Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,604
- 1,704
TANU kilikuwa ni chama cha Kitaifa. Kirefu chake cha Tanzania African National Union kilikuwa na maana ya 'Chama cha Kitaifa cha Muungano wa Waafrika'. Hakika Chama hiki kilikuwa na wanachama na viongozi kutoka kila pembe ya Tanzania/Afrika.
Suala hili la utaifa wa chama lilizingatiwa wakati tunaingia kwenye mfumo wa vyama vingi. Lakini cha ajabu vigezo vililegezwa maana badala ya kusema ili chama kisajiliwe lazima kiwe na wanachama kadhaa kutoka katika kila mkoa, sheria ikasema iwe ni mikoa kadhaa tu. Naamini kuna hitaji la kuirekebisha sheria hii.
Msiniulize kwa nini nimeleta uchambuzi huu wa kihistoria. Kilicho muhimu ni kujenga vyama vya kitaifa. Huu ndio wakati wa kuwa na chama cha kitaifa kinachosimamia demo-krasi-a.