Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa ADC, Mwalimu Hamad Azizi, amesema mkutano huo utafanyika tarehe 29 Juni 2025, ukiwa ni sehemu muhimu ya maandalizi ya chama hicho kujipanga kuelekea uchaguzi mkuu, katika kuhakikisha kuwa kinapitisha wagombea imara na wenye uwezo wa kushindana katika nafasi mbalimbali wanazoshiriki
"Tutapitisha wagombea kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kwa nafasi zote za uongozi, ili kuhakikisha tunashiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi na kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi," amesema Mwalimu Azizi
Hamad amesema kuwa hadi kufikia leo, Juni 26, 2025, jumla ya wagombea watatu wamechukua fomu za kutia nia kugombea nafasi ya Urais kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar kupitia chama cha hicho. Bara, waliotia nia ni Muttamwega Mgaywa na Wilson Mulumbe, huku kwa upande wa Zanzibar, aliyechukua fomu ni Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho, Ahmad Rashid
Chama cha ADC kimeeleza kuwa mchakato wa uteuzi wa wagombea hao utafanyika kwa kuzingatia misingi ya uwazi, demokrasia ya kweli, na wa haki. Lengo ni kuhakikisha kuwa kila mgombea anapewa nafasi sawa ya kushindanishwa kwa haki, na kwamba chama kinatoa mfano bora wa uendeshaji wa siasa za kistaarabu