Chalinze: Ridhiwani achafuka

Chalinze: Ridhiwani achafuka

We kibo mbona cdm walikuwa wanatembea kwa chopa huku wapigakura wao kwa miguu hamkusema kitu.Au ndo kuku akinya sawa lkn bata akinya kaharisha?acheni kumshafua ridh1 anahaki ya kushinda kwa kishindo 90%+ mpende msipende.
 
wakati mwingine watu wawe wanaukubali ukweli hata kama unawaumiza
 
Kura za wananchi ndo zitaamua a cha haraka maana hakuna mtu aliewahi kuishi kesho, upo hapo.
 
Acha kumchafua dogo anachukua hapo hata mseme nini?
 
Kila linapoulizwa swali na mwananchi yeyote anayehitaji ufafanuzi wowote kutoka kwake,Ridhiwani amekuwa akikwepa maswali hayo kwa kusemakuwa masuala hayo yatashughulikiwa na watendaji wahusika. Kama mgombea wa Ubunge,hapaswi kusema hivyo.Timu ya Kampeni ya CCM lazima ijipange na kumrekebisha. Anachafuka na kuanza kuepukwa.

Pia,kauli na matendo yake ya hivi karibuni yamemfanya achorwe kama 'mwenye kujiona na mwenye dharau kubwa' kwa wapigakura wake. Kule Lugoba,alikataa kuhutubu kwakuwa kulikuwa na jua alipopaswa kusimama. Akasusia hadi pale alipowekewa kivuli. Na akatamka kuwa yeye ni 'Mgombea Special' kupata kutokea Chalinze. Hii ni dharau kwa Wabunge waliotangulia akiwemo Mkuu wa Nchi. Wananchi wa Chalinze sasa hawampendi kama mwanzo

Ridhiwani pia anasemwa kama Mgombea ambaye hutamba hadharani na pembeni kuwa tayari ameshashinda na hakuna wa kumpoka ushindi wake kwa vyovyote vile. Wananchi wanahoji,uhakika huo anaupata wapi wakati hata kura bado hazijapigwa? Tambo zilimponza Tamba!

Ingawa CCM ina nafasi kubwa ya kushinda hapa Chalinze,matendo na maneno ya Ridhiwani yaweza kupeperusha ushindi huo kwani wananchi ndiyo waamuzi kupitia sanduku la kura.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Chalinze)
R1, hata asipopiga kabisa kampeni, tayari aliishashinda zamani pale tuu alipoteuliwa kuwa mgombea wa Chama Kubwa, Chama Kongwe, Chama Zoefu kilichokubuhu kwa uoza wa rushwa na ufisadi!.

Tuhuma zote ulizo mwaga humu ni tuhuma ndogo ndogo za nyodo na uswahili swahili, wapiga kura wa Chalinze wangekuwa wazungu, hapo ungeweza kusema angeweza kunyimwa kura, lakini wanachalinze ni waswahili, mambo ya uswahili swahili, hapo ndipo kwake!, R1 ni mbunge mteule wa Chalinze anayesubiri kuthibitishwa tuu hiyo tarehe 6 April .
Pasco
 
Back
Top Bottom