VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Kila linapoulizwa swali na mwananchi yeyote anayehitaji ufafanuzi wowote kutoka kwake,Ridhiwani amekuwa akikwepa maswali hayo kwa kusemakuwa masuala hayo yatashughulikiwa na watendaji wahusika. Kama mgombea wa Ubunge,hapaswi kusema hivyo.Timu ya Kampeni ya CCM lazima ijipange na kumrekebisha. Anachafuka na kuanza kuepukwa.
Pia,kauli na matendo yake ya hivi karibuni yamemfanya achorwe kama 'mwenye kujiona na mwenye dharau kubwa' kwa wapigakura wake. Kule Lugoba,alikataa kuhutubu kwakuwa kulikuwa na jua alipopaswa kusimama. Akasusia hadi pale alipowekewa kivuli. Na akatamka kuwa yeye ni 'Mgombea Special' kupata kutokea Chalinze. Hii ni dharau kwa Wabunge waliotangulia akiwemo Mkuu wa Nchi. Wananchi wa Chalinze sasa hawampendi kama mwanzo
Ridhiwani pia anasemwa kama Mgombea ambaye hutamba hadharani na pembeni kuwa tayari ameshashinda na hakuna wa kumpoka ushindi wake kwa vyovyote vile. Wananchi wanahoji,uhakika huo anaupata wapi wakati hata kura bado hazijapigwa? Tambo zilimponza Tamba!
Ingawa CCM ina nafasi kubwa ya kushinda hapa Chalinze,matendo na maneno ya Ridhiwani yaweza kupeperusha ushindi huo kwani wananchi ndiyo waamuzi kupitia sanduku la kura.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Chalinze)