VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Sijui sababu lakini najionea. Kwasasa CCM imepunguza mno kasi iliyoanza nayo katika kampeni zake za Ubunge hapa Chalinze. Mikutano yake sasa haihamasishi,haivutii,haishawishi.Imegeuka sehemu za kusalimiana na kutaniana.Hakuna sera labda hela. Mgombea,Ridhiwani Kikwete, sasa 'anarelax' bila wasiwasi.Nani amemdanganya kuwa tayari ameshajipatia ushindi???
CHADEMA wao wanaongeza kasi siku hadi siku. Wanapita vijijini na mitaani wakimnadi Mgombea wao Torongey ambaye sasa anazidi kupata nguvu na kusikilizwa. Anajinadi kama anayeomba na kutafut kweli. 'Makamanda' wa CHADEMA nao wanaitumia nafasi ya 'kujisahau' kwa CCM kuendelea kumuuza Mgombea wao.
Hadi muda huu, kimaoni CCM iko mbele.Lakini,kiuchaguzi na kikura bado ni 50/50. Kusuasua kwa CCM kwaweza kuonekana kama dharau kwa wananchi na wao wakaamua kugeukia upande mwingine. Kwakuwa siko vyema sana kiafya kwasasa, naishia hapa na mtazamo wangu huu.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Chalinze)