Chalamila: Wakimvaa Rais Samia nami nitawavaa

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,359
Reaction score
4,814
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema wakati fulani yeye na wenzake wanachukia majukwaani na wakati mwingine hata kuwa na lugha nzito, kwasababu hawapo tayari kuona Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akitukanwa na kurushiwa mawe ambapo ameahidi Watu wakimvaa Rais Samia na yeye atawavaa.

Akiongea Jijini Dar es salaam mbele ya Rais Samia leo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Chalamila amesema “Sisi Mh. Rais unaweza kutuona wakati fulani tunachukia sana majukwaani na wakati mwingine tumekuwa hata na lugha nzito, utuwie radhi kwelikweli lakini tunafanya hivi kwa sababu hatuko tayari kuona ukitukanwa na kurushiwa mawe”

“Hawa Polisi wameimba hapa wakikuvaa tutawavaa, na Mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam naahidi wakikuvaa, nitawavaa, juzijuzi uliona nipo soko la mabibo nilichukia sana, lile soko halijawahi kuleta hata senti moja Serikalini, tumekaa na DC Ubungo mpaka mwisho wa mwaka wa fedha litakuwa limeingiza sio chini ya bilioni 2 ambazo zilikuwa zinaingia kwenye mifuko ya Watu binafsi, hivi katika hali hiyo nicheke au nifanyaje?”

“Nimeamua kuwa mkali, na hiyo ndiyo kamba nitakayoendelea kuinyoosha ili matusi yasiende kwa Mheshimiwa Rais, niendelee kutekeleza maono yake kama Kiongozi aliyeniteua katika Mkoa huu wa Dar es Salaam, namshukuru Waziri wangu wa Mambo ya Ndani (Masauni) ni Mtu mmoja mtulivu sana Mimi moyo huo sina na sijawahi kumuomba hata Mungu anipe hata nusu kwasababu nitafeli kazi na watanionea na ufupi nilionao”
 
Hivi kinachomyima usingizi kiongozi ni matusi au madudu yaliyofanywa kwa nchi? Kama hakuyafanya kwa nini yasijiwe kwa lugha Kali kama ya wapinzani? Kwa nini imechukua miezi mitatu bila majibu?
 
Uzuri Chalamila pia haogopi kukosoa kazi hataki kudhalilika akiwa kwenye nafasi yake, Chalamila chawa promax
 
Nitamwambia Mh RC akasome Biblia na atafakari hasa kuhusu vipengele vyenye ukakakasi vya makubaliano ya kisheria ya awali katika suala la uendeshaji wa Bandari za Tanganyika kwa msaada wa Diipiiwelidi. Asaidie kumshauri kiongozi wake kwa usahihi, kweli na haki, wala asikae kimya akafikiri yuko salama yeye na wa aina yake. Biblia Ester 4:13-14.
 
Back
Top Bottom