Chakula Cha Dagaa na ugali

Chakula Cha Dagaa na ugali

JEJUTz

Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
75
Reaction score
199
Safisha dagaa na uwaweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia dagaa wakaange kidogo kisha tia chumvi, pilipili, curry powder, turmeric, na nyanya chungu, koroga vizuri mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri kisha tia nyanya na ufunike. Pika mpaka nyanya iive kisha kamulia limao,na pia hakikisha nyanya chungu zimeiva kidogo(usiache mpaka ziive sana manake zitavurugika pindi utakapotia tui la nazi) kisha malizia kwa kutia tui la nazi na uache lichemke mpaka rojo ibakie kidogo. Hakikisha nyanya chungu na zimeiva ndo uipue. Na hapo dagaa wako watakuwa tayari kwa kuliwa na ugali.
 

Attachments

  • IMG-20240823-WA0007.jpg
    IMG-20240823-WA0007.jpg
    69.7 KB · Views: 42
Sema kupika kwa kutumia mafuta na nazi kwa pamoja binafsi sipendezwi na chakula cha hivyo.
Na kiafya sio vizuri .
 
Wee angalia Hata kwenye hotel zenye hadhi ndani na nje ya nchi vyakula vyao vitunguu na veggie huwa hawaviivishi sana, sio kwa kupenda bali ni kwa mijibu wa kanuni za kiafya ili kutunza nutrients mlaji azipate.
 
Mie huwa nakaanga dagaa kwanza mpaka waanze kuwa wa brown bila kuungua kisha naweka vitunguu haviivi sana ukipenda nyanya waweka,hoho,karoti. Kisha limao.

Dagaa la limao tamu sana. Na vitunguu ambavyo havijaiva vizuri
 
Dagaa wa Kigoma na ziwa Nyasa ni watamu sana lakini hadi uwajulie kuwa andaa na kupika sivyo huwali.
Wanakuwa wagumu balaa.

Lakini ndio wanaongoza kwa ubora na utamu kuliko wengine wote
 
Dagaa wa Kigoma kilo inafikaga hadi shilingi 45,000 -50,000 bei ya kilo moja hiyo.

Tena kwa shimoni Kariakoo.

Nje ya hapo ni zaidi
 
Dagaa wa Kigoma kilo inafikaga hadi shilingi 45,000 -50,000 bei ya kilo moja hiyo.

Tena kwa shimoni Kariakoo.

Nje ya hapo ni zaidi
Shimoni kariakoo mwaka gani huo?
Soko la zamani limekarabatiwa na pale shimoni pamefumuliwa na kuwekwa mjengo mpya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom