Chakula bila mazoezi ni sumu, mazoezi ni lazima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chakula bila mazoezi ni sumu, mazoezi ni lazima

Discussion in 'JF Doctor' started by Fadhili Paulo, Oct 18, 2011.

 1. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  UMHIMU WA MAZOEZI KWA AFYA BORA

  Moja ya mahitaji matano (5) mhimu ili kuishi baada ya oksijeni, maji, chumvi, na potasiamu; ni Mazoezi. Mazoezi ni mhimu kwa ajili ya afya zaidi ya kuwa na maumbile ya kuvutia (sex body), burudani au kitu kingine chochote.

  Watu wengi hufuatilia kuhusu chakula tu, hata kama utakula vizuri vipi bila mazoezi mlo haujakamilika, kwa hiyo mazoezi ni mhimu kwa yeyote kama ilivyo kwa maji au chakula.

  Zifuatazo ni moja ya sababu mhimu za kufanya mazoezi kwa afya bora na maisha marefu bila maumivu:


  1. Mazozi yanasaidia kutanua mifumo ya mishipa ya damu ndani ya tishu za mishipa na hivyo kuzuia shinikizo la juu la damu (hypertension).


  2. Mazoezi yanatengeneza mishipa mingi, hivyo kuzuia mishipa kutumika kama chanzo cha nishati.


  3. Mazoezi yanasisimua kazi za vimeng'enya (enzymes) katika kuchoma mafuta ili kuzarisha nguvu kama mahitaji ya kudumu ya shughuri za mishipa.

  Unapofanya mazoezi, unabadili chanzo cha nguvu kwa matumizi ya mishipa toka kutumia nguvu itokanayo na sukari na kutumia nguvu inayotokana na mafuta inayojihifadhi yenyewe kwenye mishipa hivyo kuepukana na unene na uzito kupita kiasi.


  4. Mazoezi yanafanya uunguzwaji wa mishipa kama nguvu ya ziada toka kwenye asidi amino ambazo pengine zingefikia usawa wa kuwa sumu. Asidi amino zinapokuwa zaidi ya usawa wake wa kawaida kama matokeo ya kutofanya mazoezi, baadhi ya asidi amino zinaweza sababisha uharibifu mkubwa na kuzimaliza baadhi ya asidi amino mhimu. Baadhi ya hizi asidi amino mhimu zilizomalizwa, zinahitajika daima na ubongo ili kuzarisha transmita nyurolojia zake, ndiyo maana mazoezi huongeza akili.


  5. Mishipa bila mazoezi inapotea, matokeo yake sehemu ya akiba ya madini ya zinki na vitamini B6 pia inapotea. kufikia kiwango fulani cha upotevu huo, kutapelekea matatizo ya akili na kuvurugika kwa saikolojia.


  6. Mazoezi yanapunguza damu yenye sukari kwa wenye kisukari na hivyo kupunguza mahitaji yao ya insulini na matumizi ya dawa.


  7. Mazoezi yanalilazimisha Ini kuzarisha sukari toka mafuta ambayo linayahifadhi au toka mafuta yaliyomo katika mzunguko wa damu.


  8. Mazoezi yanasababisha urahisi wa kukunjana kwa makutano ya mifupa (joints).


  9. Mishipa ya miguu inafanya kazi kama moyo wa pili!, Inapokunjana na kulegea wakati tunatembea, miguu inahimili nguvu ya mvutano. Inaisukuma kwenda mfumo wa vena damu iliyokuwa imepelekwa miguuni. Sababu ya shinikizo lake na mwelekeo mmoja wa plagi, damu ya miguuni kwenye vena inasukumwa juu dhidi ya nguvu ya mvutano kutokana na kukunjana kwa mara kwa mara kwa mishipa ya miguu. Hivi ndivyo mishipa ya miguu ifanyavyo kazi kama moyo wa pili katika mfumo wa vena mwilini. Hii ndiyo thamani ya mazoezi ambayo watu wengi hawaijui.


  10. Mazoezi yanaimarisha mifupa ya mwili na hivyo kuzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).


  11. Mazoezi yanaongeza uzarishaji wa homoni zote mhimu na hivyo kukuongezea uwezo wa kushiriki tendo la ndoa (positive sex libido).

  Unapotembea kwa miguu bila kusimama mwendo wa lisaa limoja, unakuwa umeiamusha kemikali inayounguza mafuta (lipase) kuchoma mafuta kwa masaa 12, hivyo kama mtu atatembea lisaa limoja asubuhi na lingine jioni, atakuwa ameiamusha kemikali hiyo kufanya kazi kwa masaa 24!!, na kwa faida ya ziada kemikali hiyo huzisafisha pia taka za helemu (cholesterol) kwenye damu.

  Hivi ndivyo ilivyo rahisi kupunguza uzito na unene bila nguvu wala gharama yeyote!. Anza leo, tembea saa moja kutoka kituo A mpaka kituo B bila kupumzika asubuhi na jioni, baada ya wiki mbili pima tena uzito wako kuona namna ulivyofanikiwa kwa muda huo na muda gani uwekeze tena kumaliza tatizo hili linalosumbuwa watu wengi kote duniani. Soma zaidi ‘unene na uzito kupitia maajabu ya maji'.

  Mazoezi yafuatayo ni mazuri sababu ya thamani yake ya baadaye na hayasababishi maumivu kwenye maungio, nayo ni; kutembea, kuogelea, baiskeli, tenisi, gofu, kukwea, kudansi na kadharika.

  Unatumia chumvi ipi? Ya unga iliyopita kiwandani au ya mawe ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt)? Ipi nzuri?,je chumvi ni hatari?
  ,
  http://maajabuyamaji2.artisteer.net/chumvi/
   
 2. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,562
  Likes Received: 1,072
  Trophy Points: 280
  Mdau nashukuru kwa mchango wako mzuri. Kama kuna uwezekano naomba
  utuorodheshee mazoezi mazuri na namna ya kuyafanya kwani kuna mtu aliniambia
  si vizuri kufanya mazoezi chini ya dakika 45 naomba ufafanuzi kuhusu hilo!
   
 3. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Kaka asante
   
 4. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  asante mkuu naungana na gazeti maana kuna mazoezi mengine yanafanya maungo yawe makubwa sasa unawezakujikuta unaongeza maungo amayo mmh! kwakweli siyo msaada zaidi tafadhali
   
 5. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Useful bandiko, thanks buddy!!!
   
 6. florence

  florence JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 405
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  thanks a lot. Hiki kitambi cha kike kinaniboore
   
 7. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ahsante kwa kutukumbusha mkuu.
   
 8. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  watakufa wengi! ahsante kwa ukumbusho
   
 9. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  dankie,umenisaidia kunikumbusha katika suala zima la kufanya mazoezi.
   
 10. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Gazeti nashukuru kwa muda wako, kama nilivyoyaorodhesha hapo juu, na mfalme wa yote ni KUTEMBEA. Katika kuchaguwa aina ipi ya zoezi ufanye, kwanza inabidi ujuwe thamani au uwezo wa zoezi hilo katika kuunguza mafuta, tunafanya mazoezi ili kuunguza mafuta na kupata nguvu. Jambo la pili la kuangalia ni thamani ya zoezi hilo katika miaka ya baadaye (uzeeni) na tatu ni zoezi hilo kutokugharimu maungio (joints na uti wa mgongo).

  Nimewahi kuwa na KITAMBI kwa muda kama wa miaka miwili, kilinisumbuwa sana, nilifanya kila aina ya mazoezi, kuinuwa vyuma, kuruka kichurachura, pushapu n.k lakini kitambi hakikunitoka!, sikuwa na raha kabisa. Watu wengi hawajuwi kuwa kitambi au unene kupita kiasi ni ugonjwa au ni chanzo cha magonjwa mengi. Nilipokuja kuelewa kuwa kutembea ni zoezi zuri nilianza mara moja asubuhi na jioni, ndani ya wiki 2 niliona mabadiliko makubwa na hatimaye sina kitambi na sitakaa niuguwe kitambi kwakuwa miguu yangu yote miwili ipo salama!.

  watu wengi ukiwambia kutembea mara moja wanajibu ''Mi natembea sana, naenda sokoni, dukani, bombani kuteka maji n.k''. UNATAKIWA UTEMBEE BILA KUSIMAMA KWA MUDA WA SAA MOJA TOKA KITUO A HADI B ndipo lipase huamushwa kuchoma mafuta kwa masaa 12 mfululizo!. Tembea tu spidi ya kawaida, ikiwa huwezi anza kidogokidogo, leo dakika 10, kesho 15, keshokutwa 20 hivyo hivyo mpaka utaweza kutembea dk 60.

  kwa wale ambao huwa bize sana wanaweza kununua ile mashine ya umeme ya kutembea na kuifunga chumbani kwao hivyo muda wowote wanapokuwa free nyumbani wanaweza kutembea juu ya mashine hii kwa lisaa limoja.

  Ikiwa unene au uzito limeshakuwa ni tatizo kubwa, unashauriwa ufanye hivi kwa matokeo ya haraka, acha kabisa soda ya aina yeyote au juisi yeyote ya kiwandani, acha chai ya rangi na kahawa, acha kupika vyakula katikati ya mafuta mengi staili ya chipsi au maandazi vile, kula zaidi matunda na mboga za majani (ikiwa kuna mtu anahitaji namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vya mbogamboga yaani vegetable dishes, atanyoosha mkono nimtumie baadhi ya recipes), mhimu kumbuka kunywa maji kabla ya kiu na kutumia chumvi ya baharini ambayo haijasafishwa.

  maajabuyamaji2.artisteer.net
   
 11. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  rahisi sana mkuu, lisaa limoja asubuhi na jingine jioni, utakuja kuniambia, hakuna kitambi tena, kutembea tu wala hauinuwi vyuma vizito!!
   
 12. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Kwa kuongezea, sio kweli lazima ufanye mazoezi zaidi ya dk 45. Kikubwa kinachotakiwa ni kuwa na muda wa kupasha joto mwili na misuli (warm up) na kila unapomaliza mazoezi kuwa na cool down time. Minimum warm up na cool down period ni 5 minutes na max ni 10 minutes. Hii ni muhimu sana ktk kujenga kuujenga mwili, misuli na kikubwa kuondoa uwezekano wa injuries.
  Kama unatembea au kimbia, pasha joto mwili kwa ku stretch kidogo kwanza ili usiishtukize misuli kwa kuanza kutoka baruti right away. Same way kama una lift weights, basi unaanza na weight ndogo kupasha misuli- mikono- mabega, bicepts na tricepts, na miguu- hamstrings through. Mgongo pia ni muhimu sana- both lower and upper kupasha moto.

  Kuhusu trend, mwili lazima upate muda wa kupumzika. So kwa kuanzia, jipangie week ya kwanza at least 3 times a week- tembea kiasi (minimus 30 minutes) then kadri week zinavyoongezeka unaweza ongeza distance na ndani ya week 3-4 utaanza kuona mabadiliko, na hata kuweza kuanza kukimbia aka jogging.
   
 13. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,562
  Likes Received: 1,072
  Trophy Points: 280
  Fadhili ni kweli nimefanya mazoezi muda mrefu, nimekuwa mwepesi
  mikono imejazia na kifua kimetanuka kwelikweli lakini bado kitambi
  hakijaondoka, kwa hiyo haya ya kukimbia niache?
   
 14. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #14
  Oct 19, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Gazeti, kukimbia kama unaweza kukimbia kwa mwendo wa taratibu lakini kwa lisaa lizima ni vizuri zaidi, lakini kutembea tu kwa spidi ya kawaida masaa 2 kwa siku inatosha, cha msingi uwe na saa kabisa mkononi ili ujuwe dk 60 zikitimia toka uanze kutembea basi unaweza kupumzika. kumbuka kikombe kimoja au viwili vya maji kila nusu saa kabla ya mlo, ukifuatisha vizuri thread hii utafaulu tu, unaweza kujinyima baadhi ya vitu kwa muda kama soda, chai ya rangi na kahawa, pia punguza vyakula vinavyopikwa katika mafuta mengi. lolote tujulishane.
   
 15. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  kwamaelezo yako inaonyesha unaweza ukafanya mazoezi hata 800yrs lkn hiyo ndambi yako isiishe.
  Unajua wa2 wengi wanajua kufanya mazoezi ndiyo kuondoa kitambi na kusahau kuwa chakula ndiyo mpango mzima na ndiyo kinacho leta kitambi.

  Kwenye swala la chakula nazan kuna mambo 2 yakuzingatia.Kwanza ni mda wa kula chakula lzma uzingatiwe wengi huwa wanakula chakula usiku nakushiba full na mda huo huo wanaingia kulala na huku wataalam wanashauri inabidi ukae hata 2-3hrs ndiyo uingie kulala baada ya kula na vilevile mro wa usiku ndiyo unatakiwa uwe mlo mdogo kupita yote.Na itakuwa vizuri zaidi usiku ukila vyakula vilaini vinavyo yeyushwa haraka tumbon.

  Na pili aina ya vyakula unavyo kula inatakiwa upunguze sana kula vyakula vyenye mafuta xana.Mfano unakuta mtu katoka kufanya zoezi akifika mezani au anapitia kwanza kwenye banda la chips na kuagiza chips mayai na nyama ya kuku nusu au anaagiza kitimoto kilo nzima na kuila peke yake akimaliza hapo unakunywa na bia 2,3 na kuingia kulala.
  Sasa utaona hapo matatizo aliyo yaingiza mwilin ni makubwa zaidi ya yale anayoyatoa kwa kufanya zoezi sasa unafikiria kwa stlye hiyo hicho kitambi kitatoka mwaka gani??

  Unaweza kutoa kitambi kwa njia ya kupunguza ulaji wa vyakula vya aina fulani.
   
 16. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ngoja nianze mazoezi..
   
 17. kimbendengu

  kimbendengu JF-Expert Member

  #17
  Nov 13, 2015
  Joined: Jun 7, 2013
  Messages: 2,146
  Likes Received: 1,071
  Trophy Points: 280
  mimi naomba kujua kwa kizungu ( zoezi la kichurachura) tafadhali wadau
   
 18. n

  nosimo JF-Expert Member

  #18
  Nov 13, 2015
  Joined: Jul 13, 2015
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mhhh!! Asubuhi mimi nikiamka tu nasimama pembeni ya kitandani changu, naanza mchakamchaka nusu saa, naoga nakula matunda huyoooo kwenye basi. Nina uzito aa wastani kabisaaaa! Je kukimbia huku kunaweza niletea athari uzeeni??? Shukrani.
   
 19. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #19
  Nov 13, 2015
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,207
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  mgonjwa wa rhomatoid arthritis(huambatana na multiple joint pain and swellings) je anaruhusiwa kufanya mazoezi? na je kama jibu ni NDIO,Je ni aina gani ya mazoezi?
   
Loading...