proffesa issa
Senior Member
- Jan 6, 2015
- 118
- 51
wadau.wasomi kutoka chuo cha stanford univesity,california wamegundua betri mpya za simu ambazo zitajaa chaji ndani ya dakika moja tu.
================
================
Chanzo:millardayoSasa hivi teknolojia inatuletea hii.. simu yako itajaa chaji kwa dakika moja tu !
![]()
summer-camper-low-battery
Kwa sababu ninahitaji mawasiliano lazima niwe na simu.. Kwa kuwa nahitaji mawasiliano bora nay a kisasa najikuta nalazimika kuwa na smartphone.. Watu wengi wanatumia smartphone, inarahisisha vingi.. Facebook, Twitter, Whatsapp natumia kiurahisi kabisa.
Baada ya hapo ikaja teknolojia ya kifaa cha kutunzia umeme ili kama mtu ukiishiwa chaji kwenye simu yako na uko mbali basi Power bank inasaidia simu yako kuendelea kuwa hewani kwa muda mrefu zaidi.
GOOD NEWS kwako, huenda muda mfupi ujao usihitaji sana kutembea na Power bank yako.
Utafiti umefanyika Stanford University California ambapo wamebuni betri aina nyingine ambayo hii unaambiwa inaingia chaji kwa dakika moja tu.. ni rahisi zaidi na salama kuitumia hii.
Wanasayansi wanasema hii betri itakuwa salama zaidi kwa kuwa hailipuki kama ambavyo ziko betri nyingi zinazotumiwa sasa hivi ambazo zimetengezwa kwa lithium.
Utaenjoy sana hii kwa sababu inajaa chaji kwa haraka zaidi, japo uishaji wake pia ni wa haraka ukilinganisha na betri hizi za kawaida.. ila hautohitaji kukaa muda mrefu kusubiri simu yako ijae.
[video]https://youtu.be/i5fukKMvjOo[/video]