Chain Of Command: Dkt. Mpango hajui mipaka yake

Waacheni wasaidiane kuongoza nchi si kazi ndogo.

ndio maana Katiba inatakiwa kuwa reviewed.
 

Hakika.

Na Rais akimuagiza VP wake kufanya kazi yoyote ile au kufuatilia jambo lolote lile, hautangazii ulimwengu kuwa amefanya hivyo!
 
Nadhani siku anamuapisha kasema pamoja na majukumu yake ya kikatiba lakini anamtaka akamsaidie katika ukusanyaji wa mapato na kubana matumizi ya serikali ingekuwa ushauri tu wala asingesema ila kampa majukumu nje majukumu ya kikatiba.
Heija,
Nakuelewa vema hata mimi niliisikia hiyo kauli ya mama na niwazi kuwa mama anatarajia ushauri wa Mpango linapokuja swala la kifedha na uchumi ila kwakua mama bado hajamahishia docket ya wizara ya Fedha katika ofisi ya VP naamini ushauri wa VP unatarajiwa kuwa behind the closed door na sio otherwise.
 
Makongoro yuko smart?

Kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake.
 
JK aliwahi kusema urais ni wangu na sina ushirika na mtu yoyote yule.
 
Duh tungeisoma hiyo sehemu ya Makamu wa Rais tungejua km ni kweli haruhusiwi kusema lolote mpaka Rais
Mimi nijuavyo bado ana Mamlaka ya kutoa amri za kazi pasipo kusubiri Rais
Mfano juzi kawaambia Wakuu wa Mikoa waache ULEVI,UZINZI na kujifanya vinuri
na kwa vile Bara anapajua kuliko Mama yeye ndiye mshauri Mkuu wa Seriklali huenda faili la Ole Sabaya ndio amelisimamia ndio maana wengi sasa wanamuogopa wakijua anaona wasiofaa km kina Makonda kutosogelea utawala huu
 
Kwa Kumbukumbu Kawawa alikuwa Waziri Mkuu. Hata kama alivikwa cheo cha Makamu wa Pili wa Rais bado alikuwa na Authority kama Mkuu wa Shughuli za Utendaji Serikalini. Lakini Makamu wa Rais sidhani kama Chain of Command inampasa afanye
Wewe unataabika na nini juu ya hilo? Kuwa wewe unajua kuliko yeye?
Au unadhani amepata nafasi hiyo kwa kubahatisha?
Muache afanye kazi zake, hutaki, hama nchi.
 
Sasa wewe unaejua vifungu njoo na hivyo vifungu tuone Umahili wako Mkuu. Majukumu ya VP kwenye Muungano yako Mahsusi Kikatiba. Sasa wewe unaetaka kuhalalisha Maajukumu mengine kiutendaji njoo na Hivyo Vifungu
mngetuwekea hiyo Chain of Command au Katiba inayomuwekea VP mipaka kwanza ndipo tuendelee
km haipo muacheni Makamu wa Rais awakemee hawa wazinzi na wala Rushwa wanaotamani Ukuu wa Mikoa na Wilaya kujifanya Marais huko waliko
 
Kumbe humu jamvini kuna watu vilaza kweli2! MR ana mamlaka makubwa kumfuatia Rais sema wengi huwa ni wapole, lakini anaweza kuchukua hatua kwa kiongozi yoyote kasoro boss wake. Kama mambo hamyajui ulizeni siyo ujinga kufanya hivo!
 

Nikweli anapenda sana matamko
 
Hesabu iko hivi, kuna kitu CCM wa bara wanafanya kwa kuwa hawakudhania mambo yangekuwa yalivokuwa - disobedience!! Ilianza siku Dr. Mpango alipopewa nafasi ya kushukuru na kuaga Bunge. Yeye akatumia nafasi hiyo kueleza misimamo ya serikali na huku hata Rais hajapata nafasi ya kulihutubia Bunge.

a) Huko Bungeni kuna wengine wanadai wafanyiwe vitu majimbo mwao.
b) Wengine wanakiri uonevu wa wafanyabiashara na makundi mengine ya wananchi.
c) Wengine wanapinga chanjo.
d) Mara matatizo ya Tanesco, Bandarini nk.

2025 kutakuwa na watia nia wa kutosha!!
 
Makongoro yuko smart?

Kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake.
Ukiachana na kwamba anapiga mvinyo Jambo ambalo sio dhambi maana iyo ndo burudani yake naomba unipe mapungufu mengine ya Mackongoro ,mtu kua smart sio kwamba alazima asiwe na mapungufu KWA 100%, Binafsi nauona uongonzi mzuri ndani yake tena wa kiwango Cha juu kuliko watu mnavyomchukulia katika Mambo madogo madogo ya kijamii, tunao viongozi wapo tu KWA sababu ya bahati, au kubebwa lakin nakwambia mtu kama hujampa nafasi ya kutenda hutojua uwezo wa mtu, hivyohivyo kwenye jamii tunao watu bora Sana tatizo kupata nafasi kuonyesha uwezo wao ndo shida
 
Mpango ni makamu kutoka bara
Ni kweli na hapa katika Katiba ya 1977 inakubali lkn baada ya Muundo wa Vyama vingi naona ilibadilika ndio tunayoitafuta na tunayoizungumzia, je ni kweli Mkamu haendi Visiwani Kikazi?
na je haruhusiwi kufanya kazi zozote isipokuwa kwa kuagizwa na Rais? na ile ya Mazingira?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…