Chaguzi za Tanzania na hadithi ya bwana tajiri

Siri ya sifuri

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
2,016
1,501
Salaam!?

Nafuatilia chakuzi za Taifa letu Tanzania, naona jinsi zilivyojaa mazonge kisha nafananisha na hadithi ya bwana tajiri.

Ilikua hivi:

Tajiri mmoja alikua anaoa hivyo akaalika watu wa mji mzima kuhudhuria sherehe ya harusi yake, sharti moja ilikua kila MTU lazima awe na Kadi, hivyo wapambe wake wakaanza kugawa kadi. Watu wakajitokeza kwa wingi kuchukua kadi, kulikua na matatizo madogo madogo ya kiuandishi kama vile, Mohamedi kuandikwa Mwamedi, Ali, Alii, Juma, Jumaa, Rashid kuandikwa Rashad n,k.

Walipouliza vipi kuhusu kukosewa kwa majina yetu? Wakajibiwa msiwe na hofu maadam MNA kadi mtakula, tena CHAKULA ni kingi mtakula na kusaza. Siku ikafika watu wakamiminika ukumbini kwa wingi, Lahaula walichotarajia sichokilichotokea, getini kulikuwa na ulinzi mkali, kadi zikachikuliwa.

Mwenye kadi alipoulizwa we unaitwa nani? Akajibu >Mwamedi, >Akaambiwa kaa kando, hii kadi ni ya Mohammed siyo yako umeiiba wewe, Juma nae akaambiwa kadi ya Jumaa siyo yako huwezi kuingia ondoka!! Mbaya zaidi hata wale waliokua wamechelewa kidogo nao wakazuiliwa nakuambiwa wameshakula wanataka kurudia Mara ya pili. Hata pale walipojitetea nakushauri wanuswe mikono, wakajibiwa >Haiwezekani wajanja nyie, mmeenda kunawa mikono kwa Sabuni. Watu wakabaki na mshangao wasijue lakufanya, kiko wapi hiko CHAKULA tulichoambiwa tutakula na kubakisha!? Hivi ndivyo chaguzi zetu zilivyo, zimejaa ghilba na hadaa.

Na si kwenye siasa tu Bali kwenye kila eneo linalohitaji kufanyika uchaguzi mwendo ni huohuo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom