Chaguzi za ndani za CCM - Yanayojiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chaguzi za ndani za CCM - Yanayojiri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dudus, Mar 25, 2012.

 1. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,101
  Trophy Points: 280
  Wakuu heshima;

  Leo nimebahatika kuhudhuria mkutano wa CCM uliofanyika katika mtaa wetu na kusimamiwa na viongozi na wahamasishaji mbalimbali katika ngazi ya kata ambapo mambo mbalimbali kichama na kitaifa yalijadiliwa. Kwa taarifa iliyotolewa mkutanoni ni kwamba mikutano ya aina hii inaendelea nchi nzima na mimi binafsi nilifanya uchunguzi na kugundua katika kata yetu mitaa yote ilikuwa na mikutano ya aina hii kwa siku ya leo. Kwa uchache, baadhi ya yaliyojiri na/au kujadiliwa ni kama ifuatavyo:-

  (i) Kwanza mbinu iliyotumika ni kuwatangazia watu kwamba ungekuwa mkutano wa wananchi wote ambapo kwa ngazi ya eneo letu naweza kusema ulifurika sana na mada zilikuwa "hot" wahudhuriaji (wanachama na wasio wanachama wakitoa changamoto mbalimbali za kukikosoa chama na nini kifanyike ili kuboresha).

  (ii) Wananchi walielezwa kwamba serikali iliyoko madarakani ni ya CCM hivyo vyama vingine vyote kupitia wawakilishi wao (wabunge na madiwani) wanatekeleza sera za chama tawala.

  (iii) Ilielezwa kwamba mjumbe wa shina anazo kofia mbili, ya chama na ya serikali. Ya chama kwa maana kwamba anasimamia utekelezaji wa maagizo ya chama katika eneo lake na ya serikali kwa maana kwamba kuna baadhi ya majukumu ya kiserikali yanatekelezwa naye. Kwa mfano, kutoa barua na/au fomu mbalimbali za utambulisho pale mwananchi anapohitaji huduma fulani ya kiserikali kama kufungua akaunti za benki, n.k.

  (iv) Ilielezwa pia kwamba wajumbe wa mashina ni watekelezaji wakuu wa mipango ya mandeleo katika maeneo yao kama kufuatilia upatikanaji wa huduma za barabara, shule, hospitali, ulinzi na usalama, n.k.

  (v) Wajumbe wote wa mashina waliaswa kuhakikisha lengo kuu la chama - yaani KUSHIKA DOLA - linafanikiwa na hasa tunapoelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015.

  (vi) Wanachama wote wa CCM waliaswa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika mchakato tarajiwa wa Katiba Mpya ya nchi.

  (vii) Wanachama wote walihimizwa kuhakikisha wanatoa michango yao ya uanachama (T.Shs. 1,200/=) ili kukiimarisha chama chao.

  (viii) Mwisho, wanachama waliagizwa kutokubali kumchagua yeyote katika ngazi ya uongozi endapo unachama wake una walakini au una mashaka. Kimsingi, kwa mujibu wa Katiba ya CCM, ili mwanachama aruhusiwe kugombea uongozi katika ngazi yoyote ni lazima awe na uanachama hai kwa angalau miaka mitano.


  MAONI YANGU (kama mtu huru nisiyefungamana na upande wowote):

  (a) Kwa niliyoyaona kwenye kikao kile na hamasa iliyokuwepo, wapinzani wana kazi ya ziada kukamata dola na hasa wasipoelekeza nguvu zao kwenye maeneo ya chini (grass roots); yaani kwenye mashina ambapo kimsingi ndipo wapiga kura walipo.

  (b) Hapo kwenye (iii) na (iv) kuhusu mjumbe wa shina kuwa na kofia mbili ambapo kimsingi ndivyo ilivyo huku chini kwenye mashina - Mjumbe anatazamwa kama mtendaji fulani wa serikali wakati kimsingi ni nafasi ya chama. Mara kadhaa tumewahi kutakiwa "kupeleka barua ya mjumbe" pale tunapohitaji huduma fulani ambayo sio ya kichama. Nadhani Katiba Mpya izungumzie hili.

  Haya wakuu, hoja ndio hiyo iko mezani.
   
 2. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mbona hujatuambia ni kata ipi na nani alikuwa anatoa maelekezo hayo? ukijibu hapo ntarudi.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nadhani hapa CCM wanajimilikisha viongozi wa serikali za mitaa na mabalozi wa nyumba 10. Wakati wa chama kimoja ndio walikuwa wanashikilia kofia mbili lakini kwa sasa sio sahihi na hapa CHADEMA inabidi watoe elimu. Ni hivi. Yapo maeneo yamechagua Diwani toka vyama vya upinzania je huyo diwani, na kila diwani alikuwa na list ya mambo aliyosema atayafanya. Sasa leo CCM wanataka kutuaminisha hao madiwani wanawakilisha CCM hata kama ni diwani toka upinzani?

  Pili, mipango/miradi ya maendeleo ipo regardless ni chama gani kiko madarakani. Na miradi yote imepitishwa na bunge hivyo serikali za mitaa au mabalozi wanasimamia miradi iliyopitishwa na chombo cha wananchi yaani bunge. CCM kwa sababu ndio wako serikali kazi yao ilikuwa ni kuandaa bajeti lakini hata wakati wa kuandaa wabunge wote wanashiriki kupitia kamati za bunge.

  Huu mkakati wa kujimilisha mabalozi ni kuanika asubuhi na mapema.
   
 4. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kwa taarifa iliyotolewa mkutanoni ni kwamba mikutano ya aina hii inaendelea nchi nzima na mimi binafsi nilifanya uchunguzi na kugundua katika kata yetu mitaa yote ilikuwa na mikutano ya aina hii kwa siku ya leo.

  siyo kweli. ninakoishi hakuna mkutano wa aina uliofanyika leo.
   
 5. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,101
  Trophy Points: 280
  Inawezekana ni kweli huko uliko hakuna mkutano uliofanyika. Ila niliko mimi mikutano ilikuwepo mitaa yote. Wakuu mie natoa taarifa tu ya kilichofanyika mtaani kwetu (niko Jimbo la Ubungo). Mkiamua kuchukulia kwa uzito chukulieni la sivyo mnaweza kupuuza vile vile.
   
 6. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,101
  Trophy Points: 280

  Haswa mkuu wangu; ndicho kilichoongelewa na ndivyo inavyofanyika kila siku katika maeneo yetu hasa huku chini kabisa kwa wapiga kura. Tatizo ni kwamba, pamoja na upotoshaji huu wa makusudi ambapo wananchi wa kawaida wasioweza kupambanua mambo vizuri kutokana na elimu duni ya uraia, hakuna jitihada za makusudi kurekebisha hali hii hasa KUTENGANISHA KAZI ZA VYAMA NA ZILE ZA SERIKALI katika ngazi za chini.
   
Loading...