CHADEMA Yazindua operesheni maalum dhidi ya Mafisadi

CHADEMA Yazindua operesheni maalum dhidi ya Mafisadi

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA kimetangaza operesheni kubwa kote nchini ya kudai uwajibikaji na urejeshwaji wa mali za umma zilizoporwa hapa nchini.

Akitangaza operesheni hiyo kubwa na ya aina yake wakati akihutubia mikutano ya hadhara huko Rukwa na Singida Naibu Katibu Mkuu wa chama Salum Mwalim aliwataka wananchi kuunganisha nguvu katika operesheni hiyo.

Kiongozi huyo alisema imekuwa ni kawaida kwa kashfa kushfa kubwa kutokea hapa nchini na hakuna lolote linalotokea hasa baada ya wahusika kujiuzulu.

Alitaja kashfa kadhaa zikiwemo za Richmond,IPTL,bomba la gesi na nyinginezo nyingi zilizopoteza mabilioni ya walipa kodi.

Salum Mwalim amesema watahakikisha fedha zote za umma zilizoporwa zinarejeshwa.

CHADEMA kimekuwa chama cha kwanza kutangaza operesheni maalum ya kudai kurejeshwa kwa umma fedha zote zilizoporwa katika kashfa mbalimbali kuwahi kutokea nchini.

Nukuu ya alichosema Naibu Katibu Mkuu:

""Alisema wahusika watatajwa. Kujiuzuru haitatosha. Wananchi watadai fedha zirudishwe. Wahusika wafilisiwe. Mali zitaifishwe. Fedha zikahudumie wananchi; kujenga maabara, kuchimba visima-maji, kulipia elimu ya juu, hospitali hazina dawa; n.k.""
 
duh!! wanaenda kwa matukio sio!!?? operesheni m4c, delete ccm.........
 
Sasa ndio watanzania wataelewa kwanini tulisema delete futa ccm kabisa
 
Duh hii imekaa poa sana, haya ndio mambo tunayoyataka. CHADEMA katika hili tuna imani sana nanyi, go go salum mwalimu, go go CHADEMA
 
Bring back our power...
Wachinjiwe national stadium...
 
Huyu kijana ni hazina kubwa sana ya TAIFA hili , sijui alikuwa wapi siku zote aisee !
 
At last time has come. God be with us, God be with Tanzanians.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA kimetangaza operesheni kubwa kote nchini ya kudai uwajibikaji na urejeshwaji wa mali za umma zilizoporwa hapa nchini.

""Alisema wahusika watatajwa. Kujiuzuru haitatosha. Wananchi watadai fedha zirudishwe. Wahusika wafilisiwe. Mali zitaifishwe. Fedha zikahudumie wananchi; kujenga maabara, kuchimba visima-maji, kulipia elimu ya juu, hospitali hazina dawa; n.k.""
 
Attachments

  • attachment.jpeg
    attachment.jpeg
    11.3 KB · Views: 389
Duh hii imekaa poa sana, haya ndio mambo tunayoyataka. CHADEMA katika hili tuna imani sana nanyi, go go salum mwalimu, go go CHADEMA

Chadema hawana utani na ufisadi na mafisadi..
 
Back
Top Bottom