CHADEMA yazidi kuitesa CCM Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yazidi kuitesa CCM Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Noti mpya tz, Jun 17, 2012.

 1. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  HARAKATI za mabadiliko zinazoendeshwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kaulimbiu ‘Vua Gamba Vaa Gwanda' imezidi kushika kasi mkoani hapa baada ya wanachama 70 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Arumeru kuamua kukikimbia.

  Wanachama hao walipokelewa jana na Katibu wa CHADEMA mkoani hapa, Amani Golugwa kwenye ofisi zao za mkoa zilizopo maeneo ya Ngarenaro, ambapo viongozi mbalimbali wa mkoa walishiriki hafla hiyo, akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), Ephata Nanyaro, Mwenyekiti wa BAVICHA, Ceccilian Ndossi na Mwenyekiti wa CHADEMA, Arumeru Magharibi.

  Walipatiwa kadi za uanachama huku kiongozi wao, Vivian Lebulu akikabidhiwa katiba ya CHADEMA na bendera ambapo mwenyekiti wa BAWACHA alimvisha skafu yenye rangi za chama hicho.

  Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Lebulu alisema kuwa wameamua kuachana na CCM baada ya kuona kwa kipindi kirefu imekuwa madarakani, huku ikishindwa kutatua kero za wananchi, akitolea mfano kwenye jimbo lao ambako asilimia 35 ya wanafunzi wa shule za msingi hukaa chini kwa kukosa madawati.

  Alisema waliamua kujiunga CHADEMA, ili kushiriki kikamilifu harakati ya kuing'oa madarakani CCM kupitia sanduku la kura mwaka 2015 kutokana na imani kubwa waliyonayo kuwa chama hicho makini kina sera nzuri za kuwakomboa wanyonge.

  Kwa upande wake, Katibu wa CHADEMA Mkoa, kabla na baada ya kuwapatia wanachama hao kadi, aliwasomea haki na wajibu alionao mwana-CHADEMA popote alipo huku akiweka msisitizo umuhimu wa kupinga uonevu na kupigania haki na kulinda utu wa watu wote kwa gharama yoyote.

  Aidha, alisema operesheni hiyo itahamia wilayani Monduli Juni 24, wanakotarajia kuvuna wanachama wengi, hasa kutokana na maombi ya muda mrefu ya wananchi wa maeneo hayo.


  Source: TZ Daima

  Mzee EL kaa tayari M4C iko mlangoni kwako....
   
 2. Martin Mwila

  Martin Mwila Member

  #2
  Jun 17, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanx m4c
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mungu awape nini tena masikini wanyonge wa nchi hii? Amewapa zawadi ya CDM
   
 4. D

  Danho Member

  #4
  Jun 17, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana M4C
   
 5. mashami

  mashami Senior Member

  #5
  Jun 17, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  habari njema sana izi..!
   
 6. Mlitika

  Mlitika JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 458
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nape umebakiza wanachama wangapi Arusha?
   
 7. b

  blue arrow JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mpaka wamasai wamekubali awamu hii,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
  kazi kweli kweli
   
 8. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  "oil chafu hizo" nape
   
 9. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hana kitu kabaki yeye peke yake kama alivyosema
   
 10. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ukiona Paka amekubali kulala chali chukua jembe ukalime siku zitakuwa ukingoni....
   
 11. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hapa tunasubiri kwa hamu sana

   
Loading...