CHADEMA yavuna 960 kutoka CCM Arusha

yegella

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
3,113
1,102
CHADEMA mkoa wa Arusha juzi ilizindua mradi wa maji uliogharimu
40mil, fedha kutoka kwa wananchi na CHADEMA. Uzinduzi huo ulifanywa na
Katibu wa CHADEMA mkoa wa Arusha Amani Golugwa, pamoja na Mwenyekiti wa
BAVICHA mkoa Nanyaro katika kijiji cha Ng'iresi kata ya Oltroto Arumeru magharibi. Mradi huu ni jitihada
za chama pamoja na wananchi hao ambao wapo jirani na vyanzo vingi vya
maji lakini bado wanateseka na kutokuwa na huduma hiyo ya maji

Mradi huo ambao umekamilika utanufaisha zaidi ya wananchi 5,000.
Baada ya uzinduzi huo ndipo wananchi wananchama wa ccm waliporudisha
kadi zao na kujiunga na CHADEMA, zaidi ya 960 za ccm zilirudishwa na
walijiunga na CHADEMA wakiongozwa a mwenyekiti wa kijiji, pamoja na vitongoji vyote
vinne
Umati uliojitokeza kwenye uzinduzi.jpg Umati uliojitokeza kwenye uzinduzi
Katibu wa mkoa,pamoja na mwenyekiti aliyerudisha kadi akiingalia ya CHADEMA kwa umakini.jpg
Katibu wa mkoa pamoja na mwenyekiti aliyerudisha kadi akiingalia ya CHADEMA kwa umakini
Wananchi wakishuhudia maji.jpg
Mradi wa maji uliogharimu 40mil

Nawasilisha
 
CHADEMA mkoa wa Arusha juzi ilizindua mradi wa maji uliogharimu
40mil, fedha kutoka kwa wananchi na CHADEMA. Uzinduzi huo ulifanywa na
Katibu wa CHADEMA mkoa wa Arusha Amani Golugwa, pamoja na Mwenyekiti wa
BAVICHA mkoa Nanyaro katika kijiji cha Ng'iresi kata ya Oltroto Arumeru magharibi. Mradi huu ni jitihada
za chama pamoja na wananchi hao ambao wapo jirani na vyanzo vingi vya
maji lakini bado wanateseka na kutokuwa na huduma hiyo ya maji

Mradi huo ambao umekamilika utanufaisha zaidi ya wananchi 5,000.
Baada ya uzinduzi huo ndipo wananchi wananchama wa ccm waliporudisha
kadi zao na kujiunga na CHADEMA, zaidi ya 960 za ccm zilirudishwa na
walijiunga na CHADEMA wakiongozwa a mwenyekiti wa kijiji, pamoja na vitongoji vyote
vinne
View attachment 45952Umati uliojitokeza kwenye uzinduzi
View attachment 45954
Katibu wa mkoa pamoja na mwenyekiti aliyerudisha kadi akiingalia ya CHADEMA kwa umakini
View attachment 45953
Mradi wa maji uliogharimu 40mil

Nawasilisha

Duh huo ndio UMATI wa watu!!! Kha! Kweli ukipenda, hata chongo utasema ni kengeza!
 
Hongera CDM kwa mradi wa maendeleo hasa uliolenga kuwapunguzia kina mama na watoto adha ya kusaka maji.
 
Sababu za wanachama wa ccm kurudisha kadi na kuhamia chadema ziko wazi na zinaridhisha. BIG UP CHADEMA
 
Mradi wa Sh40 Milioni? Hiyo pesa hata kisima kimoja huwezi kuchimba..

Chadema bana kila siku mnasema Arusha hakuna CCM ni Chadema tu sasa hao watu 960 wametoka wapi?
 
Mradi wa Sh40 Milioni? Hiyo pesa hata kisima kimoja huwezi kuchimba.. Chadema bana kila siku mnasema Arusha hakuna CCM ni Chadema tu sasa hao watu 960 wametoka wapi?
NDANI YA MIAKA 5O YA UHURU CCM WAMESHINDWA KUPELEKA HT MRADI WA MAJI WA 1ML KWENYE KIJIJI HICHO, kama unaakili timamu unaweza kutueleza sababu za kushindwa kufanya hvy?
 
CDM Arusha imeanza kubaini siasa si maandamano wala si Lema pekee yake.I hope hawa watoto si miongoni mwa wanachama wapya 960 ha ha ha ha ha ha ha.
attachment.php
 
Mradi wa Sh40 Milioni? Hiyo pesa hata kisima kimoja huwezi kuchimba..

Chadema bana kila siku mnasema Arusha hakuna CCM ni Chadema tu sasa hao watu 960 wametoka wapi?

Unajua gharama ya kuchimba kisima? Mmezoea kudanganya wananchi kwa gharama za kifisadi, unadhani wote ni mafisadi. Kwa taarifa yako 50% ya gharama za miradi mingi ya halmashauri huishia mifukoni mwa wezi wachache. Mkiambiwa nchi ni tajiri lakini imejaa wezi, hamtaki kukubali.
 
Back
Top Bottom