tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa wito kwa Watanzania wote kushiriki maombi ya Novena Takatifu yanayofanyika chini ya Kanisa Katoliki, ambayo yanahitimishwa tarehe 23 Agosti 2025, kwa lengo la kuliombea taifa amani, haki na mshikamano wa kitaifa.
Katika taarifa kwa umma iliyosainiwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Tanganyika), John Wegesa Heche siku ya Ijumma, chama hicho kimewataka wanachama wake na Watanzania wote kwa ujumla kushirikiana na waumini wa Kanisa Katoliki katika maombi hayo ya kitaifa.
Soma pia: Rais TEC atangaza maombi ya kufunga kuombea haki na amani katika uchaguzi mkuu
“Tukitambua kuwa tarehe 23 Agosti ndio siku ya kuhitmisha maombi haya, Chadema inawaomba Watanzania wote tuungane na waumini wa Kanisa Katoliki, katika maombi ya Novena Takatifu tarehe 23 Agosti 2025, katika kuombea Taifa letu juu ya haki na amani huku tukijua kama kitabu Kitakatifu Biblia inavyosema; Isaya 32:17: "Na kazi ya haki itakuwa ni amani; na matunda ya haki yatakuwa utulivu na tumaini daima”, amesema Heche.
Aidha, Heche amerejea historia ya mapambano ya kisiasa yaliyosimamiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akieleza kuwa Nyerere alihusisha hata nguvu za Mungu katika kudai uhuru wa Tanganyika. Amekumbusha changamoto za kisiasa zilizojitokeza kwenye chaguzi zilizopita, ikiwemo za mwaka 2019, 2020 na 2024, ambapo chama hicho kimesema kulikuwa na ukiukwaji wa utu na haki za kidemokrasia.
“Kati ya mwaka 1955 hadi 1959 Mwalimu J. K Nyerere alianza kuwahamasisha Watanganyika kudai uhuru wa kisiasa dhidi ya Mkoloni Mwingereza. Aliwaambia Watanganyika kuwa tutamdai Mkoloni Mwingereza atuachie uhuru wetu. Kama atakataa tutaenda Umoja wa Mataifa nao wasipotukubalia tutaenda kulalamika kwa Mungu”.
Kwa mujibu wa Heche, chama hicho kinaamini kuwa maombi ya pamoja yatawajengea Watanzania ujasiri, hekima na mshikamano, akisema: “huu ni wakati wa kuungana kama familia moja ya Watanzania mbele za Mungu, tukimuomba atufungulie njia ya haki, uhuru, na kuheshimu utu wa kila mmoja wetu”.