Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka Klabu ya Yanga kujiepusha na Siasa na kurejesha Shilingi milioni 100 zinazodaiwa kuchangia kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia GSM Foundation.
Kupitia taarifa iliyotolewa Agosti 15, 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia, CHADEMA imesema kitendo cha Yanga kuhusishwa na mchango huo ni kuingiza michezo kwenye siasa, jambo linalokiuka kanuni za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) zinazokataza vilabu kujihusisha na siasa
CHADEMA imesema michezo inapaswa kuunganisha watu wa itikadi na mitazamo tofauti, na si kuwa chombo cha kugawa wananchi. Chama hicho kimeongeza kuwa hatua ya Yanga kusaidia chama kimoja cha siasa ni kuwadhalilisha mashabiki na wanachama wasio na itikadi sawa
Aidha, chama hicho kimewataka viongozi wa Yanga kujitathmini iwapo wana uhalali wa kuongoza taasisi inayokusudiwa kuunganisha Watanzania wote bila kujali tofauti zao za kisiasa.