CHADEMA yataka kada wake kuachiwa huru au kufikishwa mahakamani

CHADEMA yataka kada wake kuachiwa huru au kufikishwa mahakamani

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetaka kuachiwa huru au kufikishwa mahakamani kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Wilaya ya Kibamba, Ernest Mgawe ambaye kimedai anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini.

1759569208635.png
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo, chama hicho kimeeleza kuwa awali kiongozi wao huyo aliitikia wito wa Jeshi la Polisi na kufika Kituo cha Polisi Gogoni Oktoba 1 mwaka huu na kisha baadae kufikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay ambako anashikiliwa hadi leo kwa tuhuma za kuhamasisha fujo kwenye magari ya Mwendokasi na kuhamasisha maandamano.

Soma: Mwenyekiti wa CHADEMA Kibamba, Ernest Mgawe akamatwa kwa tuhuma za kuhamasisha Maandamano na Fujo Vituo vya Mwendokasi

"Jeshi la Polisi linamtuhumu kwa makosa mawili kuhamasisha maandamano na kuhamasisha fujo kwenye vituo na magari ya mwendokasi .Makosa hayo ni ya kudhaminika kisheria, hivyo hatua ya kumshikilia kwa mua mrefu bila utaratibu ni kinyume cha Sheria na Katiba ya nchi" imeeleza sehemu ya barua ya CHADEMA.

1759569193761.png
 
Attachments

  • 1759569191363.png
    1759569191363.png
    568.2 KB · Views: 15
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetaka kuachiwa huru au kufikishwa mahakamani kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Wilaya ya Kibamba, Ernest Mgawe ambaye kimedai anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo, chama hicho kimeeleza kuwa awali kiongozi wao huyo aliitikia wito wa Jeshi la Polisi na kufika Kituo cha Polisi Gogoni Oktoba 1 mwaka huu na kisha baadae kufikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay ambako anashikiliwa hadi leo kwa tuhuma za kuhamasisha fujo kwenye magari ya Mwendokasi na kuhamasisha maandamano.

"Jeshi la Polisi linamtuhumu kwa makosa mawili kuhamasisha maandamano na kuhamasisha fujo kwenye vituo na magari ya mwendokasi .Makosa hayo ni ya kudhaminika kisheria, hivyo hatua ya kumshikilia kwa mua mrefu bila utaratibu ni kinyume cha Sheria na Katiba ya nchi" imeeleza sehemu ya barua ya CHADEMA

1759569051698.png
 
Back
Top Bottom