CHADEMA yataka bei ya ukumbi Ikulu ili wengine nao wakiwa na vikao vyao wasisite kwenda

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka Serikali kuweka wazi utaratibu unaosemwa kwamba ulifuatwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), kufanya mkutano wao wa Chama Ikulu jijini Dar es salaam, ili kila mmoja ajue iwapo atahitaji kwenda kufanya mkutano hapo.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bwana John Mrema, amesema kama ukumbi huo wa Ikulu unaruhusiwa kifanyika mkutano na mtu yeyote, basi waweke wazi utaratibu wa bei ili wengine nao wakiwa na vikao vyao wasisite kwenda ili kuongeza pato la Taifa.

Chanzo: East Africa Television
 

Huu mtego ! Yaani CDM ionekane Magogoni??. Kwa hilo CCm watafute kauli nyingine. Habari ya eti na wengine wanaruhusiwa itakuwa ngumu kiuhalisia.
 
Ikulu ni mahali patakatifu alisema babu si mahala pakufanyia vikao vya vyama. Ni mahali pa dhifa za kitaifa.
Pako neutral ni sawa na vyama visivyo weza fanyia mikutano makanisani au misikitini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…