CHADEMA yasomba wana-CCM mkoani Pwani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yasomba wana-CCM mkoani Pwani.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, May 18, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wimbi limalotikisa nchini kwa sasa la wanachama wa CCM kukimbilia CHADEMA limeingia Mkoani Pwani ambapo wanachama 250 wa CCM katika kijiji cha Mkoko, kata ya Msata, wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, wamekihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA wakati wa operesheni ya kutembelea vijiji inayofanywa na viongozi wa chama hicho.
  Katibu wa CHADEMA Jimbo la Chalinze Gasper Shoo alisema kuwa wanachama hao wa CCM walijiunga na upinzani Mei 12 wakati wa operesheni hiyo iliyoongozwa na viongozi wengine wa jimbo.
  “Katika operesheni yetu tuliyoifanya Mei 12 mwaka huu wanachama wa CCM 250 wamekihama chama chao na kuingia CHADEMA wakiwa na lengo moja tu la kuunga mkono viongozi wa taifa wanaopambana na ufisadi na kupigania maendeleo katika maeneo mbalimbali hapa nchini,” alisema Shoo.
  Aidha aliongeza kusema kuwa wataendelea na ziara yao hasa maeneo ya vijijini ambayo CCM wamekuwa wakijivunia kupata kura nyingi kutokana na baadhi yake kutofikiwa kwa muda mrefu na viongozi wa CHADEMA.
  Mkoa wa Pwani umekuwa ni ngome kuu ya CCM kwa muda mrefu lakini sasa ngome zake zinaanza kusambaratishwa vibaya na CHADEMA hali inayohatarisha uhai wa chama hicho kwa siku za usoni.

  Source:Tanzania Daima Ijumaa
   
 2. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ukimwambia nape anasema eti si kweli,hakuna kitu kibaya kama uwe hujui,alafu hujui kama hujui
   
 3. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  WanaCCM waliohama kwenda upinzani wenye majina ndani ya CCM kama Diwani n.k. hesabu yao haizidi sita (6) "by Nape"
   
 4. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mpaka kieleweke!
   
 5. Goheki

  Goheki JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 270
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Makamanda hongereni,msisahau na kufungua ofisi pia wapeni wanachama katiba ya chama.
   
 6. B

  Ba'mdgo JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Asante CDM ukombozi unakaribia bado kusini mjafika ni mda muafaka wakufika huko
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Bado familia ya Kikwete maana najua yeye Kikwte ana kadi ya chadema....
   
 8. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hajui na hajui kama hajui,au anajua ila anajifariji badala ya kufarijiwa
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu Molemo, naomba kujuzwa hii pwani iko wapi bila shaka itakuwa kazikazini..
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Makamba kasha mwambia anafanya CCM ya baba yake....
   
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Makamba alitoa ujumbe mzito sana pale
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu Crashwise acha kunichekesha
   
 13. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Akili za nape ni fupi sana, ana akili inayodhani kwamba diwani anapiga kura kama 1,000 hivi. Anatakiwa atambue kuwa hao wanachama wanaowaama ndio wenye impact kwenye kura, kwa hiyo kadiri wanachama wanavyoama ndivyo kura za ccm zinazidi kupungua. Lakini kwa kuwa ana akili fupi kama mwenyekiti wake na mawazo mgando kama Mukama, anaishia kuropoka tu na povu kumtoka...
   
 14. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  umenichekesha mkuu. Kina Rejao watasema uko Arusha
   
 15. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,951
  Likes Received: 1,275
  Trophy Points: 280
  kudos cdm
   
 16. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  "Chemical Ali" wa Tanzania!
   
 17. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Naona sasa 'ADUI ANAPIGA IKULU'... Kwa mwendo huu 2015 ccm ijiandae kisaikolojia kuwa chama cha upinzani... Makamanda kazi nzuri.
   
 18. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 19. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape atuambie tena hao ni wale waliotakiwa kuondoka
   
 20. V

  Vunjavunja Member

  #20
  May 18, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makamba si yule mzee wa degree ya matusi, imeishakula kwao.
   
Loading...