CHADEMA yashinda rufaa Sumbawanga Mjini

Kama ni kweli ccm watahakikisha jimbo la Arusha, Sumbawanga na Igunga uchaguzi unarudiwa kwa wakati mmoja, na hii itakuwa fursa yao nzuri kugawa nguvu ya kampeni kwa upande wa CDM
 
Ndo mchezo wao cku hizi. wanatanguliza kuwafrahisha then wanaumiza zaidi Arusha ili kuweka balance lkn dhamira yao imetimia kwa Lema Arusha. tuwe makini na utangulizi huu wa sumbawanga.

ngoja tuone itakavyo kuwa kaka.
 
Mkuu lakini ujue ule sio mkokoteni wa kawaida. Kwa taarifa yako, lile ni gari la ki-falme na ni wachache mno wanapata bahati ya lifti humo.

Nikuhakikishie tu kuwa huwezi pata lifti ile kama siyo unalegezwa na kupumbazwa ili kuweka sahihi kwenye mikataba mibovu. Haswa kwa mpenda sifa kama ........
Hawakupi bure ile lifti bwana, wacha kuzidi kudanganyika mdanganyika!
 
Hapa nahisi ufisadi wa hali ya juu. Kama wengine walivyokwisha tabiri, hii ni ishara wanaitaka sana Arusha. Viongozi wengi sana wamewekeza AR, na hapo hawataki kuachia. Itakuwa patashika! Lakini hili jimbo litaichafua sana CCM kwenye uso wa dunia. Tusubiri tuone.
 
Magamba hawatapona msimu huu ni mbaya sana kwao hata wafanyeje hatawakichelewesha uchaguzi lakini ukweli unabaki palepale HUWEZI JIKINGA MVUA KWA KUTUMIA NETI UTALOWA TU ............ R.I.P CCM
 
Magamba hawatapona msimu huu ni mbaya sana kwao hata wafanyeje hatawakichelewesha uchaguzi lakini ukweli unabaki palepale HUWEZI JIKINGA MVUA KWA KUTUMIA NETI UTALOWA TU ............ R.I.P CCM

vipi mkuu utakuwepo kwenye mazishi?
561597_466536363390505_1533907023_n.jpg
 
hehe hakukuwa na bahasha kwa makanjanja hivyo huwezi pata habari. kweli jf ni zaidi ya vyombo vya habari. hebu tupia 5000/= kwa jf tafadhali
 
Kwanini ProCHADEMA wengi wangependa kuona Lema anarudishiwa ubunge wake na mahakama, wakati huo huo viongozi wengi wa CCM wanaomba Mungu sana Lema arudishiwe ubunge wake?
 
Leo Sumbawanga hoyeeeee kwa CDM ili Arusha ije kuwa hoyeeee kwa CCM.

Jamani hili ni changa la macho, subirini muone lazima rufaa ya Lema itapigwa kibao. Policcm wajanja mno.
 
CCM yaanguka tena
• SASA UCHAGUZI MDOGO
WANUKIA SUMBAWANGA
na Happiness Mnale
KWA mara nyingine tena, Chama
cha Mapinduzi (CCM), kimegonga
mwamba baada ya Mahakama ya
Rufaa Tanzania, kuitupilia mbali
rufaa ya aliyekuwa Mbunge wake
wa Sumbawanga Mjini, Aeshi
Hilaly, aliyevuliwa ubunge na
Mahakama Kuu Kanda ya
Sumbawanga Aprili 30, mwaka
huu.
Uamuzi wa kuitupilia mbali rufaa
hiyo, umetolewa na jopo la majaji
watatu, Januari Msoffe, Edward
Rutakangwa na Engela Kileo,
baada ya kubaini kasoro za
kisheria.
Hilaly alivuliwa ubunge na
aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya
Sumbawanga, Bethuel Mmila,
kutokana na kesi iliyofunguliwa
na aliyekuwa mgombea ubunge
kupitia CHADEMA, Nobert
Yamsebo.
Hata hivyo, Mei 28 mwaka huu,
Hilaly alikata rufaa namba 55 ya
mwaka 2012, dhidi ya Yamsebo,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
(AG), Justus Kalama na Vitus
Kapufi, akipinga uamuzi wa
Mahakama Kuu.
Rufaa hiyo imebainika kuwa na
dosari kadhaa ambazo
zimeishawishi Mahakama ya
Rufaa Tanzania chini ya jopo la
majaji hao kuitupilia mbali jana
katika uamuzi uliotolewa jijini
Dar es Salaam.
Dosari hiyo ni kutokuwepo kwa
mwenendo wa maombi ya
mlalamikaji katika kesi ya msingi
ya kuomba mahakama impangie
kiwango cha fedha ambacho
alipaswa kulipa kama amana ya
kufungua kesi hiyo kwa mujibu
wa Kifungu cha 111 (3) cha
Sheria ya Uchaguzi ya mwaka
2010.
Katika uamuzi wake uliosomwa
na Naibu Msajili wa Mahakama ya
Rufani, Zahra Maruma,
mahakama hiyo ilirejea kifungu
cha 111 (3) cha Sheria hiyo ya
Uchaguzi.
Kwa mujibu wa kifungu hicho,
Mahakama ilisema kwamba mtu
anayefungua kesi ya uchaguzi, ni
lazima awasilishe maombi ili
mahakama impangie kiwango
cha amana anachopaswa kulipa
ndani ya siku 14 tangu kufungua
kesi na kwamba ndani ya siku 14
nyingine tangu siku ya maombi
hayo, mahakama hiyo iwe
imeshapanga kiwango hicho.
Majaji hao waliongeza kuwa, ni
muhimu kwa sababu kuu mbili,
moja ni kuipa nafasi mahakama
kuona kama maombi
yaliwasilishwa ndani ya muda
baada ya kesi kufunguliwa na pili
kuona kama maombi hayo
yaliamuliwa ndani ya muda
tangu kuwasilishwa.
Kwamba kwa mujibu wa Kanuni
ya 96 (1) na (3) za Kanuni za
Mahakama ya Rufani, si jukumu
la upande katika kesi kuamua
kuwa nyaraka fulani ni muhimu
au si muhimu katika rufaa, kama
wakili wa Hilaly, Rweyongeza
alivyodai.
Mbali ya kanuni hiyo, Mahakama
hiyo pia ilirejea katika uamuzi
wake katika rufaa namba 8 ya
mwaka 2008, Fedha Fund
Limited na wenzake wawili, dhdi
ya George T.Varghese, pamoja na
tafsiri ya Kanuni ya 85 (3) ya
Kanuni za Mahakama ya Rufani
ya Kenya za mwaka 1979.
"Kutokana na sababu hizo
tulizokwisha kuzieleza hapo juu,
tanarudia kusema kwamba
kumbukumbu zinazohusiana na
mwenendo wa maombi ya
kupangiwa kiwango cha kulipa
kama amana ni nyaraka muhimu
katika rufaa.
Kutokuwepo kwa nyaraka hizo,
rufaa haina nguvu chini ya
Kanuni ya 96 (1) (k) ya Kanuni za
Mahakama ya Rufani, hivyo rufaa
inatupiliwa mbali," lilisema jopo
hilo.
Hata hivyo, mahakama hiyo
ilisema kuwa haiwezi kuamua
upande wa warufani ulipe
gharama za rufaa hiyo kwa kuwa
kasoro zilizosababisha
kutupiliwa mbali kwa rufaa hiyo
ziliibuliwa na mahakama
yenyewe.
Julai 3, 2012, AG na Kalama, nao
walikata rufaa namba 65 ya
mwaka 2012 dhidi ya Yamsebo
wakipinga uamuzi wa Mahakama
Kuu Kanda ya Sumbawanga.
Kutokana na rufaa hizo dhidi
yake, Yamsebo kupitia kwa Wakili
wake Victor Mkumbe, aliweka
pingamizi la awali (PO) pamoja
na mambo mengine akidai kuwa
Hilaly hakuwa amelipia ada ya
kufungua rufaa hiyo ya Sh 2000.
Hata hivyo, siku ambayo
Mahakama ya Rufani ilipanga
kusikiliza rufaa hiyo, iliamua
kuziunganisha rufaa hizo mbili,
ambapo Hilaly aliunganishwa na
AG pamoja na Kalama wakawa
waomba rufaa dhidi ya Yamsebo.
Kabla ya kuanza kusikiliza
pingamizi la Yamsebo dhidi ya
rufaa ya Hilaly, mahakama hiyo
ilibaini kutokuwepo kwa
mwenendo huo wa maombi ya
Yamsebo kupangiwa gharama za
kufungulia kesi hiyo ya msingi.
Kutokana na kasoro hiyo,
mahakama ilihoji na kutaka
maoni ya mawakili wa pande
zote kuhusiana na kasoro hizo.
Wakili wa Serikali Mwandamizi,
Mwema Punzi alijibu kuwa wao
walimwandikia barua Msajili wa
Mahakama ya Rufani Kanda ya
Sumbawanga kumuomba
mwenendo wa kesi hiyo pamoja
na vielelezo vingine na kwamba
walipopewa, mwenendo wa
maombi ya gharama za kesi
haukuwemo.
Wakili wa Yamsebo, Mkumbe,
alidai kuwa kutokana na
kutokuwepo kwa mwenendo
huo, kunaifanya rufaa hiyo iwe
batili, na akaiomba mahkama
hiyo iitupilie mbali.
Hata hivyo Wakili wa Hilaly,
Richard Rweyongeza, alidai kuwa
kukosekana kwa mwenendo huo
hakuwezi kuifanya rufaa hiyo
iwe ni batili, badala yake aliiomba
mahakama hiyo itumie mamlaka
yake chini ya Kanuni ya 2 ya
Kanuni za Mahakama ya Rufani, ili
iweze kuendelea.
Wakili Rweyongeza aliongeza
kwamba hata ikibainika kuwa
hizo gharama za kufunulia kesi
hazikulipwa, anayeathirika ni
mjibu rufaa, hoja ambayo
iliungwa mkono na Wakili wa
Serikali, Punzi.
Katika kesi hiyo ya msingi namba
01 ya mwaka 2010, Yamsebo
alikuwa akipinga ushindi wa
Hilaly, akidai kuwa kulikuwa na
ukiukwaji wa Katiba na Sheria ya
Uchaguzi na hivyo kusababisha
uchaguzi huo kutofanyika kwa
haki na uhuru.
Pia, alikuwa akimtuhumu Hilaly
na wafuasi wake kutoa rushwa
kwa wapiga kura mbalimbali ili
wamchague.
Tuhuma nyingine alikuwa
akizieleka kwa Msimamizi wa
Uchaguzi kuwa alibadilisha
baadhi ya vituo vya kupigia kura
kupelekwa mbali zaidi kati ya
kilomita tano hadi nane, jambo
ambalo ilichangia kuathiri
matokeo ya uchaguzi huo.
Katika uamuzi wake, Mahakama
Kuu ilikubaliana na baadhi ya
hoja zilizotolewa na mlalamikaji
na hatimaye kutengua ushindi
wa Hilaly.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji
Mfawidhi Betwell Mmila, alisema
kuwa baada ya kupitia hoja zote,
anashawishika kusema kuwa
uchaguzi katika jimbo hilo
ulikuwa si wa haki na huru.
Jaji Mmila alieleza kuridhika kuwa
kulikwepo na mazingira ya
rushwa na kutokuwapo kwa
mazingira huru katika kampeni
kwa baadhi ya maeneo.
Katika uchaguzi huo, Hilaly
alitangazwa kuwa mshindi kwa
kupata kura 17,328, huku
Yamsebo akipata kura 17,132.
Kwa uamuzi huo, Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC), itapaswa
kuitisha upya uchaguzi ndani ya
siku 90 ikiwa Hilaly hatakata tena
rufaa kupinga uamuzi huo
wa jipo la majaji hao.
juu
Habari Mpya | Matangazo | Bei
zetu | Wasiliana nasi | Tuma
habari | Webmaster
Copyright 2012 FreeMedia
 
Back
Top Bottom