CHADEMA yashinda rufaa Sumbawanga Mjini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yashinda rufaa Sumbawanga Mjini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magesi, Oct 8, 2012.

 1. M

  Magesi JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chama cha CHADEMA kimeshinda rufaa iliyokatwa na aliyekua mbunge wa SUMBAWANGA MJINI BW. AESH HILALY BAADA YA RUFAA HYO KUTUPWA NA MAHAKA LEO.

  Update 1:
  By Ngambili Ngenja 18:05
  Yesterday Ndugu zanguni naomba niwasilishe rasmi ninalojua kuhusiana na suala hili la Sumbawanga.

  Kwanza naomba kukiri kuwa mimi nafahamiana kwa Karibu na Mwl. Yamsebo na jambo hili la Rufaa linafahamika vyema kwa wanaharakati wote wanaitakia mema nchi yetu.

  Wiki jana wanaharakati na wanachadema wa Sumbawanga walimchangia Mwl pesa kwa ajili ya safari yake ya Dar ili kwenda kusikiliza
  hukumu hiyo ambayo ilipangwa kutolewa leo. Mnamo mida ya saa 4:15 asubuhi Mwl. Yamsebo mwenyewe alipiga simu akiwa ndo anatoka mahakamani na kutupa taarifa hii nzuri kuwa Mahakama imetupilia mbali rufaa na ushindi ni wetu.

  Habari hii si uzushi na mwenye hofu afuatilie zaidi kwa bidii zake kwani hata vyombo vyetu vya habari mpaka sasa hawana wanalojua husiana na hili.

  Update 2:

  CCM yaanguka tena

  • SASA UCHAGUZI MDOGO WANUKIA SUMBAWANGA

  na Happiness Mnale | Tanzania Daima

  KWA mara nyingine tena, Chama cha Mapinduzi (CCM), kimegonga mwamba baada ya Mahakama ya Rufaa Tanzania, kuitupilia mbali
  rufaa ya aliyekuwa Mbunge wake wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly, aliyevuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Aprili 30, mwaka huu.

  Uamuzi wa kuitupilia mbali rufaa hiyo, umetolewa na jopo la majaji watatu, Januari Msoffe, Edward Rutakangwa na Engela Kileo, baada ya kubaini kasoro za kisheria.

  Hilaly alivuliwa ubunge na aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Bethuel Mmila, kutokana na kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kupitia CHADEMA, Nobert Yamsebo.

  Hata hivyo, Mei 28 mwaka huu, Hilaly alikata rufaa namba 55 ya mwaka 2012, dhidi ya Yamsebo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Justus Kalama na Vitus Kapufi, akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu.

  Rufaa hiyo imebainika kuwa na dosari kadhaa ambazo zimeishawishi Mahakama ya Rufaa Tanzania chini ya jopo la majaji hao kuitupilia mbali jana katika uamuzi uliotolewa jijini Dar es Salaam.

  Dosari hiyo ni kutokuwepo kwa mwenendo wa maombi ya mlalamikaji katika kesi ya msingi ya kuomba mahakama impangie kiwango cha fedha ambacho alipaswa kulipa kama amana ya kufungua kesi hiyo kwa mujibu wa Kifungu cha 111 (3) cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010.

  Katika uamuzi wake uliosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Zahra Maruma, mahakama hiyo ilirejea kifungu cha 111 (3) cha Sheria hiyo ya Uchaguzi.

  Kwa mujibu wa kifungu hicho, Mahakama ilisema kwamba mtu anayefungua kesi ya uchaguzi, ni lazima awasilishe maombi ili mahakama impangie kiwango cha amana anachopaswa kulipa ndani ya siku 14 tangu kufungua kesi na kwamba ndani ya siku 14
  nyingine tangu siku ya maombi hayo, mahakama hiyo iwe imeshapanga kiwango hicho.

  Majaji hao waliongeza kuwa, ni muhimu kwa sababu kuu mbili, moja ni kuipa nafasi mahakama kuona kama maombi yaliwasilishwa ndani ya muda baada ya kesi kufunguliwa na pili kuona kama maombi hayo yaliamuliwa ndani ya muda tangu kuwasilishwa.

  Kwamba kwa mujibu wa Kanuni ya 96 (1) na (3) za Kanuni za Mahakama ya Rufani, si jukumu la upande katika kesi kuamua kuwa nyaraka fulani ni muhimu au si muhimu katika rufaa, kama wakili wa Hilaly, Rweyongeza alivyodai.

  Mbali ya kanuni hiyo, Mahakama hiyo pia ilirejea katika uamuzi wake katika rufaa namba 8 ya mwaka 2008, Fedha Fund Limited na wenzake wawili, dhdi ya George T.Varghese, pamoja na tafsiri ya Kanuni ya 85 (3) ya Kanuni za Mahakama ya Rufani ya Kenya za mwaka 1979.

  "Kutokana na sababu hizo tulizokwisha kuzieleza hapo juu, tunarudia kusema kwamba kumbukumbu zinazohusiana na mwenendo wa maombi ya kupangiwa kiwango cha kulipa kama amana ni nyaraka muhimu katika rufaa.

  Kutokuwepo kwa nyaraka hizo, rufaa haina nguvu chini ya Kanuni ya 96 (1) (k) ya Kanuni za Mahakama ya Rufani, hivyo rufaa
  inatupiliwa mbali," lilisema jopo hilo.

  Hata hivyo, mahakama hiyo ilisema kuwa haiwezi kuamua upande wa warufani ulipe gharama za rufaa hiyo kwa kuwa kasoro zilizosababisha kutupiliwa mbali kwa rufaa hiyo ziliibuliwa na mahakama yenyewe.

  Julai 3, 2012, AG na Kalama, nao walikata rufaa namba 65 ya mwaka 2012 dhidi ya Yamsebo wakipinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga.

  Kutokana na rufaa hizo dhidi yake, Yamsebo kupitia kwa Wakili wake Victor Mkumbe, aliweka pingamizi la awali (PO) pamoja na mambo mengine akidai kuwa Hilaly hakuwa amelipia ada ya kufungua rufaa hiyo ya Sh 2000.

  Hata hivyo, siku ambayo Mahakama ya Rufani ilipanga kusikiliza rufaa hiyo, iliamua kuziunganisha rufaa hizo mbili, ambapo Hilaly aliunganishwa na AG pamoja na Kalama wakawa waomba rufaa dhidi ya Yamsebo.

  Kabla ya kuanza kusikiliza pingamizi la Yamsebo dhidi yarufaa ya Hilaly, mahakama hiyo ilibaini kutokuwepo kwa mwenendo huo wa maombi ya Yamsebo kupangiwa gharama za kufungulia kesi hiyo ya msingi.

  Kutokana na kasoro hiyo, mahakama ilihoji na kutaka maoni ya mawakili wa pande zote kuhusiana na kasoro hizo.

  Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mwema Punzi alijibu kuwa wao walimwandikia barua Msajili wa Mahakama ya Rufani Kanda ya Sumbawanga kumuomba mwenendo wa kesi hiyo pamoja na vielelezo vingine na kwamba walipopewa, mwenendo wa maombi ya gharama za kesi haukuwemo.

  Wakili wa Yamsebo, Mkumbe, alidai kuwa kutokana na kutokuwepo kwa mwenendo huo, kunaifanya rufaa hiyo iwe batili, na akaiomba mahakama hiyo iitupilie mbali.

  Hata hivyo Wakili wa Hilaly, Richard Rweyongeza, alidai kuwa kukosekana kwa mwenendo huo hakuwezi kuifanya rufaa hiyo iwe ni batili, badala yake aliiomba mahakama hiyo itumie mamlaka yake chini ya Kanuni ya 2 ya Kanuni za Mahakama ya Rufani, ili iweze kuendelea.

  Wakili Rweyongeza aliongeza kwamba hata ikibainika kuwa hizo gharama za kufunulia kesi hazikulipwa, anayeathirika ni mjibu rufaa, hoja ambayo iliungwa mkono na Wakili wa Serikali, Punzi.

  Katika kesi hiyo ya msingi namba 01 ya mwaka 2010, Yamsebo alikuwa akipinga ushindi wa Hilaly, akidai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi na hivyo kusababisha uchaguzi huo kutofanyika kwa haki na uhuru.

  Pia, alikuwa akimtuhumu Hilaly na wafuasi wake kutoa rushwa kwa wapiga kura mbalimbali ili wamchague.

  Tuhuma nyingine alikuwa akizieleka kwa Msimamizi wa Uchaguzi kuwa alibadilisha baadhi ya vituo vya kupigia kura kupelekwa mbali zaidi kati ya kilomita tano hadi nane, jambo ambalo ilichangia kuathiri matokeo ya uchaguzi huo.

  Katika uamuzi wake, Mahakama Kuu ilikubaliana na baadhi ya hoja zilizotolewa na mlalamikaji na hatimaye kutengua ushindi wa Hilaly.

  Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mfawidhi Betwell Mmila, alisema kuwa baada ya kupitia hoja zote, anashawishika kusema kuwa uchaguzi katika jimbo hilo ulikuwa si wa haki na huru.

  Jaji Mmila alieleza kuridhika kuwa kulikwepo na mazingira ya rushwa na kutokuwapo kwa mazingira huru katika kampeni kwa baadhi ya maeneo.

  Katika uchaguzi huo, Hilaly alitangazwa kuwa mshindi kwa kupata kura 17,328, huku Yamsebo akipata kura 17,132.

  Kwa uamuzi huo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), itapaswa kuitisha upya uchaguzi ndani ya siku 90 ikiwa Hilaly hatakata tena rufaa kupinga uamuzi huo wa jopo la majaji hao.
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Magamba kwishney! Viva CDM! 2015 kiama chao. M4C hakuna kulala.
   
 3. k

  kwamagombe Senior Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hongereni sana, sasa ni muda muafaka wa kujipanga kwa ajili ya uchaguzi
   
 4. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #4
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Imekatwa lini hiyo rufaa na majaji wepi waliokuwa wakiisikiliza?
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mkuu, tupatie source na habari kamili!
   
 6. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,873
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  Mhnnn...wasije tanguliza matokeo haya kupima furaha zenu na ya Arusha yakawa tofauti hata kama L anastahili kushinda.
   
 7. M

  Magesi JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  source ni mimi mwenyewe rufaa imetupwa na mahakama
   
 8. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Safi sana haki ilikuwa mechezewa na kucheleweshwa... twende kwa Uchaguzi magamba muone shughuli yake Viva CHADEMA!!
   
 9. B

  Bhavick JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nina wasiwasi kama wewe!hii inaweza kuwa changa la macho!
   
 10. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwenye maamuzi haya Mahakama INAAMINIKA au bado inatumiwa na MAGAMBA??
   
 11. W

  WildCard JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  AH! Kodi zetu ziendelee kuteketea tu huku wanetu wakiendelea kukaa sakafuni!
   
 12. J

  JICHO MTANZANIA New Member

  #12
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 9, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haya sasa uchaguziii huo rushwaaa adui wa haki, haki imecheleweshwa kwa rushwa sasawamekiona.
   
 13. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  na huku jk akiendelea kuzurula hovyo ulaya na amerika, na kuvutwa na mikokoteni
   
 14. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  wewe ni nani na ni mahakama gani imetoa uamuzi, lini na mahali gani, jaji aliyesoma ni nani akishirikiana na nani.....

  hivi ndivyo habari inapaswa kuwa ama sivyo ondoa c.rap na uuupupu wako humu
   
 15. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Nimeongea na mtu aliyeko mahakamani, ni kweli Yamsebo ameshinda.
   
 16. K

  Kibagata JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 773
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Ndo mchezo wao cku hizi. wanatanguliza kuwafrahisha then wanaumiza zaidi Arusha ili kuweka balance lkn dhamira yao imetimia kwa Lema Arusha. tuwe makini na utangulizi huu wa sumbawanga.
   
 17. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #17
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kama ni kweli basi kuna maeneo mengine humu nchini ni mbali na Tanzania!!!
   
 18. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,758
  Likes Received: 6,062
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwani tangu lini Mahakama ya Tanzania iliacha kuaminika?
   
 19. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hbr hii ni njema! Ila haina source kamili!

  Magesi!
  Hebu funguka kwa kina!
   
 20. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #20
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180

  Magesi hizo ni tetesi ama? Lini hiyo rufaa imekatwa? Kama umepotoshwa na magamba usitupotoshe na sisi tupe source ya habari yako!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...