CHADEMA yashinda kesi ya ubunge Kagera | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yashinda kesi ya ubunge Kagera

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 2, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  na Sitta Tumma, Biharamulo

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Bukoba, mkoani Kagera, juzi ilitupilia mbali kesi ya madai ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Dk. Anthony Mbasa (CHADEMA).


  Kesi hiyo namba 5/2010, ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kupitia CCM jimbo hilo, Oscar Mkasa.

  Mkasa alikuwa akiiomba mahakama hiyo itengue ushindi wa Mbasa kwa kile alichokuwa akidai alishinda kwa mazingira tata.


  Miongoni mwa madai katika kesi hiyo ni kuwa ushindi wa Dk. Mbasa ulichangiwa na watoto 2,325 walio chini ya miaka 18 waliokuwa wameandikishwa katika daftari la wapiga kura kinyume cha sheria.


  Mbali na mahakama hiyo kupitia kwa Jaji Richard Kibela kutupilia mbali madai hayo, imeamuru mlalamikaji kulipa gharama zote za uendeshaji wa kesi hiyo.


  Jaji Kibela alianza kusoma hukumu hiyo kuanzia majira ya saa 10:35 jioni hadi alipohitimisha na kutoa hukumu majira ya saa 3 usiku kwa kutangaza kwamba Mbunge Mbasa wa CHADEMA alishinda kihalali, hivyo ni mbunge halali.


  Akizungumza mara baada ya ushindi wa kesi hiyo, Dk. Mbasa alisema: “Nashukuru sana kwamba mahakama imetenda haki, haikumuonea mtu.”


  Alisema kimsingi mlalamikaji huyo hakuwa na ushahidi wa kile alichodai na alishindwa kuwasilisha ushahidi mahakamani.


  “Mlalamikaji alishindwa kuwasilisha hata ushahidi mahakamani. Alidai baadhi ya watoto waliopiga kura ni raia wa Burundi, lakini alishindwa kuwaleta kutoa ushahidi wao mahakamani,” alisema Dk. Mbasa kwa furaha.


  Aidha aliwashukuru wananchi wa jimbo lake la Biharamulo Magharibi kwa kufuatilia kwa karibu kesi hiyo na aliwaahidi kuendelea kushirikiana nao kwa mambo yote ikiwemo kuwapelekea maendeleo.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,668
  Likes Received: 17,723
  Trophy Points: 280
  Heeeeh, inamaana hii kesi imerudiwa na leo kama penati iliyofungwa kimakosa. Unajidhalilisha kamanda
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Ngu007,

  Mbona unakuwa na akili za matope wewe?
  Tumechoka na post zako za kila mara ambazo zimekwisha jadiliwa humu.
  Acha upumbavu bana watu tunajadili mambo mengi.
   
 4. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mkuu unaharibu mjadala
   
 5. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Naona una misuse JF, Unarudia uzi wa tangu 30 may 2012. Kama vipi soma kwanza post za wadau wengine... Issue si kuwa na post nyingi, bali kuwa habari muhimu.
   
 6. escober

  escober JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  huyu jamaa ana akili ya tope kweli kila saa yeye ni kucopy na kupaste issue ambazi zimejadiliwa kitambo
   
 7. GIB

  GIB JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  stein unamaanisha 30 may 2012? Mbona bado sana. Du umenishua nilidhani tumesha anza mwezi june. Edit please
   
 8. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  We upo shimoni mererani nini.
   
 9. Bosco Ntaganda

  Bosco Ntaganda JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 551
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  wacha utoto wewe
   
 10. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,791
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.
  Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu. (Mambo ya Walawi 11:07-08)
   
 11. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #11
  May 2, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Umetumwa ku 'neutralize'?
   
 12. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #12
  May 2, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Na weweeh, hapo kwenye green mmmh, utata
   
 13. GIB

  GIB JF-Expert Member

  #13
  May 2, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamaini na wewe umetoka wapi tena. I think it is wrong destination
   
 14. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #14
  May 2, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Sawa mzee wa tende na pilau!
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145


  Ina Maana Post zangu zote zimesha jadiliwa? au una chuki na mimi, na kuniita mpumbavu, kuna sababu ya kutukanana?

  Haunijui sikujui kwanini unitukane? Sasa kama ninaweka mambo ya kipumbavu kwanini wengine wana penda?

  Una Wivu na haunijui... na nimepekeka jina lako kama abuser wewe na hao wanaokufurahia matusi yako
   
 16. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #16
  May 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wewe una akili gani? kuna umuhimu ya kutukanana ? Au unajiona bora?
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  May 2, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Huyu Nngu007 nadhani ana ligazeti lake fulani ambalo linatoka mara 1 kwa wiki. likishatoka na hiyo habari ana copy na kupaste humu.
  Jf ni kama supu ya moto watu hatutaki maviporo humu
   
 18. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #18
  May 2, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Acha mambo ya kitoto
   
 19. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #19
  May 2, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Unatuchosha na hizo post zako zilizopitwa na wakati,kila siku unarudia hayo hayo,unachosha na post zako za viporo vilivyojadiliwa
   
Loading...