Chadema yashida arumeru mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yashida arumeru mashariki

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Nagoya, Apr 2, 2012.

 1. N

  Nagoya Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chama cha Demokrasia na maendelo Chadema Kimetangazwa kuwa mshidi wa Jimbo la Arumeru Mashariki, kupitia Mgombea wake Joshua Nassari, kwa ushindi wa haki.

  Kwa Mara ya kwanza Jeshi la Police Mkoa wa Arusha Limeonyesha kutenda haki na pia tume ya uchaguzi kwa kupitia Mkurugenzi wa uchaguzi jimbo la Arumeru.

  Pia kulikuwa na matukio ya hapa na pale TBC iliripoti msaidizi wa Mkurugenzi wa uchaguzi alikuwa akijaribu kuchakachua matokeo na kusababisha kupata kipigo kikali kutoka kwa mbunge wa arusha Godbless Lema na kuokolewa na Police kwa kumshika lema na kumpeleka mtuhumiwa kituo cha police usa river.

  Arusha sasa ni shwari na hakuna fujo ni furaha tu kila mahali, Mkutano wa hadhara utafanyika saa saba mchana ambapo Mbunge mteule atakuja kuwashukuru wanchi kwa kumchagua kuwawakilisha katika bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania na katika maendeleo yao ya jimbo.

  Shukrani za pekee ni kwa Jeshi la police ambao walionyesha kutenda haki kwa sehemu kubwa.

  Matokeo haya yatakuwa fundisho kwa chama cha mapinduzi CCM katika uchaguzi ujao 2015, baadhi ya makambi ya ndani ya chama na mitandao ya ndani ya chama ivunjwe na nguvu yao iende kwa mtu anaekubalika na sio kama makosa waliyoyafanya arumeru kwa Kumuacha Sarakikya na kumpitisha Sioi Kimizengwe.
   

  Attached Files:

 2. N

  Nelkon Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera kwa kuchambua vizur na ni kweli yote uliyosema. Ushauri: jaribu kupitia maneno yako yote kabla ya kupost coz yana makosa mengi ya kiuandishi.
   
Loading...