CHADEMA yapinga mpango wa mabaraza ya Katiba

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,458
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeeleza kuwa muundo na utaratibu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba namna ya kuwapata wajumbe wa mabaraza utarudisha nyuma jitihada za kujenga muafaka wa kitaifa wa Katiba mpya.

CHADEMA imewasilisha maoni na mapendekezo kwa tume hiyo kwa ajili ya utaratibu unaofaa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya, mamlaka za serikali za mitaa na uendeshaji wake.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika, ilieleza kuwa CHADEMA haikubaliani na muundo wa mabaraza hayo ya wilaya kuwa na wawakilishi walioteuliwa na ngazi ya kata.

“Tumependekeza kuwa wajumbe wote waliochaguliwa kuwakilisha vijiji au mitaa au shehia waingie moja kwa moja kwenye mabaraza ya wilaya,” ilieleza taarifa hiyo.

CHADEMA wamependekeza kwa upande wa Tanzania Bara, ngazi ya kuwapata wajumbe wa mabaraza hayo isiwe ngazi ya kata bali wajumbe wapigiwe kura ya kuchaguliwa kwenye ngazi za kijiji na mitaa.

“Kwa upande wa Zanzibar, katika mikoa yote ngazi ya kupata wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya iwe ni Shehia kwa wajumbe kupigiwa kura kwenye ngazi za Sheria,” ilieleza.

Aidha walieleza kuwa muundo na utaratibu huo ni muhimu katika kurekebisha upungufu katika mchakato uliotangazwa kukamilika wa ukusanyaji wa maoni ya wananchi binafsi uliofanyika kwa awamu nne mwaka 2012 ambapo tume ilifanya mikutano 1776 na wananchi wachache kutoa maoni kutokana na sababu mbalimbali.
 
Pia kata ambazo hazina madiwani zifanye uchaguzi kwanza ili kila kata iwe na uwakilishi sawia
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeeleza kuwa muundo na utaratibu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba namna ya kuwapata wajumbe wa mabaraza utarudisha nyuma jitihada za kujenga muafaka wa kitaifa wa Katiba mpya.

CHADEMA imewasilisha maoni na mapendekezo kwa tume hiyo kwa ajili ya utaratibu unaofaa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya, mamlaka za serikali za mitaa na uendeshaji wake.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika, ilieleza kuwa CHADEMA haikubaliani na muundo wa mabaraza hayo ya wilaya kuwa na wawakilishi walioteuliwa na ngazi ya kata.

"Tumependekeza kuwa wajumbe wote waliochaguliwa kuwakilisha vijiji au mitaa au shehia waingie moja kwa moja kwenye mabaraza ya wilaya," ilieleza taarifa hiyo.

CHADEMA wamependekeza kwa upande wa Tanzania Bara, ngazi ya kuwapata wajumbe wa mabaraza hayo isiwe ngazi ya kata bali wajumbe wapigiwe kura ya kuchaguliwa kwenye ngazi za kijiji na mitaa.

"Kwa upande wa Zanzibar, katika mikoa yote ngazi ya kupata wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya iwe ni Shehia kwa wajumbe kupigiwa kura kwenye ngazi za Sheria," ilieleza.

Aidha walieleza kuwa muundo na utaratibu huo ni muhimu katika kurekebisha upungufu katika mchakato uliotangazwa kukamilika wa ukusanyaji wa maoni ya wananchi binafsi uliofanyika kwa awamu nne mwaka 2012 ambapo tume ilifanya mikutano 1776 na wananchi wachache kutoa maoni kutokana na sababu mbalimbali.
chama makini,viongozi makini wanatoa mapendekezo makini,lakini ccm wataweka mawazo yao ya hila kama ya kutokuonyesha bunge live
 
Back
Top Bottom