Chadema yaondoa fitna iringa

Chadema yaondoa fitna iringa

Joined
Apr 29, 2012
Posts
81
Reaction score
4
Chama cha demokrasia na maendeleo chadema leo kimefanya mkutano wa hadhara ambao umehudhuliwa na mamia ya watu,viongozi kadhaa wa chama walikuwepo miongoni mwao ni Mh.Nassari,Mh.Msigwa na kamanda Bananga ambae amejiunga na CDM akitokea CCm yapata miezi mitano iliyopita.Mambo mengi yamezungumzwa na viongozi hawa walipokuwa wakihutubia hapa manispaa ya Iringa katika eneo la Mwembetogwa ambapo ndipo mkutano umefanyika,Viongozi hawa wa CDM wamewataka wana Iringa kutodanganywa na wanaopita mitaani kukitukana chama na kumkashifu Mh.Msigwa,Pia wamelaani vikali mauaji ya muandishi wa habari Daud Mwangosi na wamemshangaa Mh.Rais kwa kushindwa kutoa hata rambirambi kama alivyofanya kwa marehemu Kanumba!Viongozi hawa wamewataka wananchi kutohofia kufa ili ukombozi wa kweli katika nchi hii uweze kupatikana.
 
weka mapicha mkuu, wengine ni kama tomaso
 
weka mapicha mkuu, wengine ni kama tomaso

431688_423470804366905_1317499443_n.jpg Hali kama ivi mkuu
 
Wananchi wanachagua mchele ni upi na makapi ni yapi!!!
 
Back
Top Bottom