Chadema yamuundia tume Shibuda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yamuundia tume Shibuda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by palalisote, Jul 19, 2011.

 1. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo kimeunda tume itakayoongozwa na Profesa Abdallah Safari kumhoji Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu zinazomkabili. Wajumbe wengine wanaounda kamati hiyo ni Edson Mbogoro, Said Mzee, Lazaro Masey na Ester Daffi ambaye si mjumbe wa kamati, bali atafanya kazi kama mratibu wa kamati hiyo akitokea Ofisi ya Katibu Mkuu. Hatua ya kuunda tume kwa ajili kufanya kazi ya kupitia tuhuma hizo imetokana na madai ya mlalamikaji kuwa na mantiki.Msingi wa malalamiko hayo hautokani na kile kilichotokea bungeni, bali kitendo cha mbunge huyo kukaririwa na vyombo vya habari akitoa tuhuma dhidi ya viongozi wa chama hicho hadharani kinyume na utaratibu.
   
 2. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  WANATIANA VIDOLE VYA MACHO NA KUTUHUMIANA...
  Wote wanatumia vyombo vya habari....
  wanatafuta ni nani baina yao anajua kusema sana...
  wapo wanaoshuka ili amani ipatikane...
  wapo ambao amani haipatikani mpaka kwa ncha ya upanga...
  siyashangai haya.... hakika hayaishangazi, kwa sababu yamepengwa yawe hivyo...
  ni malengo ya makusudi kabisa na ni mithili ya yai viza... kwa nje ni yai lakini kilichomo ndani....
  ila kwa mapambo na nyimbo ni lulu yenye thamani.... zinavutia masikio na kuteka nyoyo....
  kila unakotazama akuna tofauti na kule kwingine!!! ndipo unapokumbuka 1992 na ukiipata picha hiyo aaah...
  Ya Ngoswe unamuachie mwenyewe na walio wake.....
  bado tuna safari ndefu...
   
 3. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Haya mashairi yametungwa na ustadh gani............
   
Loading...