Chadema yamtumia Ole Millya kumvaa Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema yamtumia Ole Millya kumvaa Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by commited, Jun 24, 2012.

 1. commited

  commited JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,619
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  SOURCE MWANANCHI LEO TAREHE 24/06/2012


  Na Peter Saramba, Arusha | 24 June 2012

  KAMPENI ya Chadema ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) inayoandamana na kauli mbiu ya vua gamba vaa gwanda leo itatua katika jimbo la Monduli, lililopo chini ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.Chadema itamtumia aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha na mmoja wa maswahiba wa karibu wa Lowassa, James Ole Millya ambaye hivi karibuni alitimkia kwenye chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

  Katika vuguvugu hilo, Chadema itafanya mikutano kadhaa ya hadhara na wa kwanza ndio unaotarajia kufanyika leo na kuhutubiwa na viongozi kadhaa mashuhuri miongoni ni wabunge wa chama hicho wanaohudhuria kikao cha Bunge kinachoendelea Dodoma.

  Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Mchungaji Amani Golugwa alisema kuwa mkutano wa leo ni uzinduzi wa kampeni kubwa inayotarajiwa kundeshwa wilayani Monduli kwa muda wa zaidi ya wiki mbili.

  Alisema kampeni hiyo inalenga kuhamasisha jamii ya wafugaji wa Kimaasai kuunga mkono harakati za kudai mabadiliko kifikra, kiuongozi, kisiasa, kiuchumi na matumizi sahihi ya rasilima za taifa.

  Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mchungaji Golugwa alisema pamoja na Ole Millya, mkutano huo pia utahutubiwa na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Bavicha), Cecilia Ndosi na Alli Bananga; aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM taifa.

  Viongozi wengine wa kitaifa, wakiwamo wabunge wanaohudhuria kikao cha Bunge, mjini Dodoma, alisema wanatarajia kuhudhuruia.

  "Tumetoa mwaliko kwa Wajumbe wa Kamati Kuu (CC) na baadhi ya wabunge wetu wanaohudhuria kikao cha bunge Dodoma kuhudhuria mkutano huo mkubwa," alisema Mchungaji Golugwa

  Alisema mkutano huo utafuatiwa na mikutano mingine katika Wilaya za Arumeru, Longido, Karatu, Ngorongoro pamoja na Arusha mjini.

  Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Ole Millya kwenda kumwaga sera za Chadema katika jimbo la swahiba wake tangu atangaze kung'atuka CCM wakati huo akiwa ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha.


  CCM Monduli wasema

  Akizungumzia ziara ya Chadema wilayani humo, Mwenyekiti wa UVCCM, Wilaya ya Monduli, Julius Kalanga alisema chama chake hakina hofu na oparesheni za Chadema, kwani kina uhakika kinaungwa mkono na wakazi wengi wa wilaya hiyo.

  "Ni haki ya kidemokrasia kwa vyama vyote vya siasa kuendesha shughuli za kisiasa, kujijenga kwa wananchi," alisema na kuongeza:

  "Chadema waje Monduli hata kila siku Wakiweza. Hatuna wasiwasi wala mashaka na ziara zao, kwani tunaungwa mkono na zaidi ya asilimia 95 ya wakazi wa Monduli."

  Lowasa anaonekana kuwa na ushawishi mkubwa katika jimbo hilo kutokana na matokeo ya ubunge mwaka 2010, kuzoa asilimia 98 ya kura zote.

  NAOMBA MAKAMANDA MLIOPO HUKO MONDULI MTUPE UPDATE TAFADHALI.. ILI TUONE MASAI NA NDUGUZETU WENGINE WANAHAMASIKA KIASI GANI... KARIBUNI
   
 2. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Hii nimeipenda sana.........

  Peoples power........
   
 3. b

  blue arrow JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama ccm imekubali m4c kufanya mkutano kule kwa EL basi ujue uchaguzi ujao tutaisiklizia ccm maana kama ninavyoijua wamasai wanamsimamo mkubwa sana
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Millya anakwenda Simanjiro kulikomboa jimbo.
   
 5. t

  tupak Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magwanda wangewasiliana kwanza na daktari wa EL maana alvyoenda ujerumani aliambiwa asipewe habari za kushtua shtua maana mabadiliko yanatakiwa yatokee bila kupoteza uhai wa mtu
   
 6. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Walioko hiko tupeni kinachojiri.
   
 7. T

  Tiger One JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 569
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Olesendeka kapasua miwani baada ya. Kusikia neno ole milya
   
 8. commited

  commited JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,619
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  wakuu hakuna mtu aliyepo huko Monduli atupe ma update ya ukweli, au huko hata network hakuna
   
 9. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Asije akatugeuka kama walivyofanya akina Guninita.
   
 10. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mkutano ni mkubwa sana unafanyika mto wa mbu,wapo mwenykiti wa mkoa,Nanyaro ambaye ni mwenyekiti wa BAVICHA mkoa,na Makamanda wengine
   
 11. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  sasa amepanda NANYARO anaeleza masikitiko yake ya kauli za mbunge wa monduli jinsi anavyolalamika kuwa ajira kwa vijana ni janga la kitaif na bomu litakololipuka mapema, badalay ya kueleza suluhisho naye analamika kama wananchi,Lowasa amekuwa WWaziri mkuu na bado ni mwenyekiti wa kamati ya bunge usalusalama na ulinzi,yupo,bado yupo kwenye nafasi ya kuchukya hatua badala ya
   
 12. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  sasa ni mwenyekit wa chadema mkoa,nanyaro kafunika mbaya namuona na ipad yake pale
   
 13. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  hakuna cha ole millya wala nini hatogombea nahc kutakuwa na jembe lingne
   
 14. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kumbe na we upo dah ndo kitaa hapa karbu
  K
   
 15. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  nipo umekaa kwa wapi,mie nipo huku kwa nyuma,weka picha mkuu maana natumia mchina,kweli huyu Nanyaro kafunika mbaya sana,hasa ujinga wa ccm
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Weka picha.
   
 17. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,296
  Likes Received: 1,216
  Trophy Points: 280
  asante kwa updates,tuweekeeni picha jamani km inawezekana,ili magamba yajionee
   
 18. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mwandishi wa habari hii ni mfitinishi na mchonganishi, nadhani anaweza kuwa mtu wa Bakwata au Uamsho maana watu wa aina hii wote wako CCM .Kichwa habari na yaliyomo huko hayana mahusiano jamani .Nchi hii longo longo eneno ?
   
 19. commited

  commited JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,619
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  endeleeni kutupa update, zaidi picha wakuu tunashukuru kwa hizo info
   
 20. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #20
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  mkuu pamoja sana
   
Loading...