CHADEMA yamshukia Mkulo - Inakuwaje Serikali Inakopa Benki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA yamshukia Mkulo - Inakuwaje Serikali Inakopa Benki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bobby, May 24, 2010.

 1. B

  Bobby JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemtaka Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, kuacha kutoa kauli za kujichanganya na badala yake aeleze wazi sababu za kushuka kwa mapato ya serikali kwa asilimia sita, ambayo ni sawa na sh bilioni 347.

  Chama hicho kimesema kauli ya Mkulo aliyoitoa jana, anayodai kuwa kauli yake ya mwanzoni mwa wiki inastahili kupuuzwa na wananchi ni ishara ya kujichanganya katika kauli zake.

  Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mnyika, alisema Mkulo anapaswa awaeleze wananchi ukweli kuwa fedha za wahisani kwa serikali tegemezi yenye udhaifu wa uongozi chini ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni sehemu ya matarajio ya mapato ya bajeti.

  Alisema dola 250 milioni ambazo serikali inataka kukopa kutoka Benki ya Stanbic ni mzigo kwa walipa kodi ambao ni wananchi, zitakazolazimika kulipwa huku zikitumika katika masuala yasiyo na manufaa kwa wananchi.

  “Fedha hizo wanazotaka kukopa zinaishia katika ziara za Rais Jakaya Kikwete, mkewe na matumizi mengine ya anasa au ubadhirifu, huku wakishindwa kuzielekeza katika ukarabati wa barabara,” alisema Mnyika.

  Alieleza kuwa Mkulo anapaswa akiri udhaifu uliotajwa na wahisani, ikiwa ni pamoja na kushindwa kusimamia serikali vizuri pamoja na rasilimali na maliasili zilizopo nchini.

  Wakati huohuo, Mnyika amemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Tawala za Mikoa wa Serikali za Mitaa (Tamisemi), Celina Kombani na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni kutoa tamko la kuthibitisha iwapo kata za Kibamba, Mbezi na Kimara zimegawanywa kutoa kata mpya za Kwembe, Msigani na Sangara.

  Mnyika ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kinondoni, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, alitoa kauli hiyo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Mtaa wa Kwembe Mpakani, Kata ya Kibamba.

  Alisema katika ziara yake katika maeneo hayo amebaini kuwa mapendekezo ya kuzigawa kata hizo yalipelekwa na Halmashauri ya Kinondoni kwa Tamisemi tangu mwaka 2008 na 2009, lakini mpaka sasa hawajaeleza uamuzi uliofanywa na wizara husika.

  Hata hivyo, alisema wananchi wanawasikia wana CCM wakisema wazi kuwa kuna kata mpya zimeanzishwa na tayari kuna wagombea wanatajwa kuonyesha nia ya kugombea katika kata hizo.

  “Nyaraka za serikali zinaonyesha pia katika Jimbo la Kawe ilipendekezwa pawe na kata mpya za Mbezi Juu, Makongo, Mabwepande na Wazo Hill. Wakati Jimbo la Kinondoni litakuwa na kata mpya ya Mzimuni. Serikali isipotoa tamko itathibitisha kuwa kuna hujuma ya kuchelewesha kutoa taarifa, kwani tayari CHADEMA imeshaanza kutoa fomu za wagombea udiwani huku mipaka ya kata ikiwa haijulikani bayana.

  Pamoja na hayo, alitoa onyo kwa mabalozi wa CCM ambao wameanza kupita wakikusanya kadi za wapiga kura, ambalo ni kosa la jinai.

  “Wananchi wanapoona matukio ya aina hiyo, watoe taarifa kwa vyombo vya dola, ofisi za chama ama kupitia simu 0784 222 222,” alisema.


  Source: Tanzania Daima la leo tarehe 24 Me 2010

  Sorry wakuu ninaomba msaada wenu kwenye hili katika haya:

  (i) Sababu ya uhaba wa huu wa fedha na matumizi mabaya na kushindwa kusimamia resources ndio maana wahisani kama vile wametoa adhabu kwa serikali, so kitendo cha serikali kukopa its obvious kwamba lengo la wahisani halifaikiwa na isitoshe serkali inahamisha hiyo adhabu kwa walia kodi ambao ndio tutakaolipa huo mkopo na riba yake. Sasa kwenye what can we do kama wananchi kustop hili?

  (ii) Inakuwaje serikali inaishiwa moaka inakwenda kukopa bank kwanini isikope kutoka kwa public thru Governement Bonds

  (iii) Kama ipo haja ya kukopa kwanini ni Stanbic na sio say NMB ambako Serikali still inahold some share ili tuwe sehemu ya hiyo ya faida ya interest?

  (iv) Halafu pesa yetu ni Tsh kwanini wakope US $ au ndio pesa ya safari hii jamani mbona wanatuonea kiasi hiki?
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,345
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  mwacheni rais akope nauli kwa ajili ya tuziara twake twa marekani kuomba misaada na kuwa wa kwanza kuonana na rais wa marekani....
   
 3. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  iii) Kama ipo haja ya kukopa kwanini ni Stanbic na sio say NMB ambako Serikali still inahold some share ili tuwe sehemu ya hiyo ya faida ya interest?

  (iv) Halafu pesa yetu ni Tsh kwanini wakope US $ au ndio pesa ya safari hii jamani mbona wanatuonea kiasi hiki?[/B][/QUOTE]


  iii) Huenda wahisani wamewaambia wakope huko. SI unajua tena nchi zetu hizi hata mambo ya ndani kabisa huwa yanapangwa washington DC. Inawezekana serikali imeajiri mshauri (consultant) aliyepewa fees za nguvu ili aishauri ikakope pesa stanbic. This is Tanzania, nadhani kuna shetani amekamata vichwa vya viongozi wetu mpaka wanafanya mambo kana kwamba wako usingizini

  iv) msaada wa wahisani ulikuwa uje kwa US$ hivyo gepu nayo inajazwa kwa USD. Hahahaaaa. Consultant ameshauri hivyo bwana na ushauri wake lazima uchukuliwe maana kasema mzungu.
   
 4. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Sijui tatizo nini hapo, why not for normal procedures through Treasry Bill at BOT?
   
Loading...