CHADEMA yamshauri Nape atafute familia yake kwanza ndipo aingilie mambo ya ndani ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Mzee Mwanakijiji ingekuwa vema sana ungemshauri @Nnauye Jr aache matusi anayomtukana Dr Slaa.Kwa matusi anayomtukana Dr Slaa sishangai watu kuchimba familia ya Nape na kuona kama amefundishwa yale maadili ya kiafrika.

Haiwezekani kwa kijana mdogo kama huyu kumtukana matusi mtu wa rika la Dr Slaa.Ni lazima mtu wa aina hiyo awe ameathirika kisaikolojia.

Sawasawa kabisa. CCM wakitukana ni sawa, ila CDM ikisema ukweli tatizo? ama kweli watz waoga wa kusema ukweli. Amelianzisha alinywe
 
Hata Obama kuna watu walimshuku kama kazaliwa Marekani, kuna wengine walimshuku kuwa ni muislam na wengine walijadili kuwa ana mtoto wa nje ya ndoa.

Ukishakuwa public figure lazima tukujadili tu hata uwe nani. Tatizo la wabongo ni kwamba akijadiliwa Dr Slaa na mchumba wake Josephine mnaona sio siasa. Akijadiliwa Nape kuwa amtafute baba yake mnasema haitakiwi. Kila mtu ambaye ni public figure lazima tumjadili hata kama wengine hamtaki

hili wala siyo tatizo. Nape anaweza kujadiliwa kama wanavyojadiliwa watu wengine. Kinachogomba hapa ni uongozi wa juu wa chama kuingia kwenye malumbano haya. Hivi vinatakiwa kufanywa na mashabiki na wapambe. Kwani hoja hizi za Nape na babake zimeanza jana na kina Kigaiya? zilipotolewa na watu wengine wala hatukujali kwani ni sehemu ya siasa lakini zinapotolewa na uongozi wa juu wa chama kuna tatizo.

Hata mifano ya Obama hivi ulimsikie Seneta au kiongozi gani mkuu wa Republican aliyehoja kuzaliwa kwa Obama au mambo yake ya familia? Waliyaacha kwa wale ma surrogate wao. Hili siyo la level ya uongozi wa kitaifa ni suala la mashabiki, wapambe n.k.
 
ukiona adui yako anaoga kwenye maji machafu na wewe unaingia kuoga ili umkomoe au ili angalau ufanane naye!... "mbona wote tuko wachafu" ndilo jibu?

Hayo unayosema ni sawa na yule mwizi aliyejipaka kinyesi ili asikamatwe ................... kama akingia huko kwenye maji machafu basi inabidi umfuate na ummalizie hukohuko!!
 
Yawezekana mwaka huo wa kumbukumbu Nape alikuwa bado hajazaliwa!!! JF kwa upekenyuzi bwana!

Kama Marehemu Moses Nnauye ali-ishi kati ya 1937-2001 kisha miaka kumi ya kumbukumbu ilikuwa 2011, ambapo Nnape alikuwa na cheo hicho hicho cha Katibu Mwenezi wa Majambazi, ilikuwaje hakutajwa kwenye orodha ya watoto wa Marehemu?

Inawezekana akawa ni Mwanaharamu walimstukia!
 
Kwa NAPE mambo ya familia yake ni sawa yajadiliwe lakini kwa babu enu SLAA ya kuiba mke na kujikopesha ni personal hayatakiwi kujadiliwa.CHADEMA mmeisha kwakweli.mwaka wenu huu hamna pakutokea!

mwaka huu mtajikanyaga sana mtabadilisha majina sana, make chadema imekamilika kila idara hoja utajibiwa kwa hoja, usaliti tutamleta ben sa8, matusi tupo wengi tu na kejeli ndo usiseme tumejaa ccm na masalia sjui mtaponea wapi
 
Mtu mzima haitahiji kushauriwa; mambo mengine mtu unafunzwa na maisha na ulimwengu na hekima. Nape ni mtu mzima.

Hekima ya Nape iko wapi? maisha ndo yanamfundisha sasa, mara ngapi anaongea hovyo kwa watanzania? viongozi wa CDM mnafurahia wakitukanwa na kuvunjiwa heshima ila wenu??
 
Siwezi ku-support ujinga huu hata kama siipendi CCM!. This is dirty politics from the very credible political party like CDM!
 
CDM nilikuwa nawaamini ila kwa hili mmenisikitisha. Hivi watu na akili zenu mnawaita waandishi wa habari na kutoa pumba hivi. Hoja ilikuwa ni kutujulisha kwa nini CDM haitakufa basi na siyo haya mambo ya kihuni yalio na ushahidi mwepesi. Hili mmechemka na ili mrudishe heshima yenu muombeni Nape radhi. Chizi kachukua nguo zenu nyie mkatoka barabarani mnamkimbiza sasa sisi tutawaoneje??????????

Toa maneno yako hapa wewe.Wewe ni CCM kindakindaki.Mshauri kiongozi wako amuombe radhi Dr Slaa kwa matusi anayomtukana.

Eti Chadema imuombe radhi Nape.Huna hata aibu!
 
Hayo unayosema ni sawa na yule mwizi aliyejipaka kinyesi ili asikamatwe ................... kama akingia huko kwenye maji machafu basi inabidi umfuate na ummalizie hukohuko!!

ukishaiingia utakuwa na ujasiri wa kusema "huyu mchafu mimi msafi"?
 
MKJJ,

Siasa za maji taka zimeanzishwa na CCM....................... sasa kama swala la Slaa kuacha upadri ni issue, kuwa na mchumba ni issue kwa nini hili lisiwe issue?? Watanzania wanapenda mipasho kwa hiyo wape mipasho!! Ndiyo maana CCM wanazunguka na taarabu nchi nzima wakati wa kapeni!!
Sasa kwenye hili Nape kafanyanini?? hahusiki na hawezi kubadilisha ni tofauti na hiyo mifano yako
 
"Vicent Nyerere sio wa familia ya Nyerere". Hayo ni maneno ya RAIS Mstaafu wa Tz. Mh. Benjamin Mkapa yakifurahiwa na makada wote wa CCM. Hiyo nayo mnaionaje wakuu?

Kwani Vincent kuwa au kutokuwa wa familia ya Nyerere ilikuwa na umuhimu gani kwa CCM? Sometimes haya mambo ya kipuuzi yapo kwa sababu yanaasisiwa, kulelewa, kuendekezwa, na kufurahiwa na wapuuzi ambao wanatakiwa pia kujibiwa kipuuzi. Na wapuuzi nambari wani nchi hii wanaeleweka.

Usiangalie matokeo angalia chanzo; tena kama unahukumu, hukumu yako na iwe ya haki.
 
Chadema mmeishapotezwa mmelazimishwa kucheza siasa za udaku na nyie mmekubali.

We sindio ulimshikia bango Dr Slaa kuwa ana kadi mbili kama vile wewe ndo unaye zilipia, sasa kamtee Bwanako nape mwana hyaramu anaye lazimisha kuwa mtoto wa NNAUYE kumbe kibaka tu, ndiyo maana kazi yake nikuropokatu
 
Kwani mkutano huo na waandishi wa habari ulikuwa maalum kwa ajili ya Nape? Hakuna issue nyingine iliyozungumzwa na secretariat ya chadema?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom