hahahaaa! Maumivu ya kichwa huanza pooole pole, dawa ni kuchagua Chadema tuCDM Kilianza Kwa Nguvu Kilimanjaro polepole kikatoboa Arusha kwa kupitia Karatu....Muda si muda kikatoboa Mbulu....Kidogo kidogo kinatoboa Babati na Hanang....kwa mtu anayejua ramani ya Tanzania Hiyo ni Njia ya kuelekea Singida...Kwa hiyo wana Singida mkae mkao wa kukipokea....Uzuri wake chadema ishatanguliza Ngome moja Singida mashariki kwa Tundu Lisu.....Kwa upande Wa kanda ya Ziwa Chadema Ilianza Tarime....hiyooo ghafla ikatoboa Musoma Mjini ikatokezea Mwanza ( Ilemela,na nyamagana na Ukerewe), Ikaruka kwa wakati huo huo kwenda Shinyanga Kishapu, Maswa Na pande za Ngara huko. kanda ya Magharibu ilianza Kigoma....Pole pole ikarukia Mpanda na hivyo inaelekea tabora..... Kanda ya Nyanda za Juu kusini Ilianzia Mbeya..ikashamiri weee.... ikatoboa Iringa....Sasa inazidi kusambaa mpaka ifike Songea.....Kanda ya pwani Hasa dar imeingia ila bado kidogo nguvu kidogo zinahitajika ili iweze kusonga mbele mpaka pwani ya kusini...VIVA CDM.
Bavicha sounds...no ni makalioni kwako....
Huu uchaguzi wa nini tena? Ina maana nchi hii chaguzi haziishi?
Mkuu hakika thread sijaielewa
Kwa wale mnaoendelea kuaminishwa na propaganda za watawala kuwa CHADEMA kinachukiwa na watu, basi fikirieni upya na jipangeni vizuri kwani moto wa chama unazidi kuwaka na kumulika kila kona. Uchaguzi mdogo wa kiti cha mwenyekiti wa mtaa wa Maisaka Kati Jimbo la Babati Mjini mkoa wa Manyara ni kama ifuatavyo
CHADEMA - kura 247
CCM - kura 170
CUF - kura 2
Sasa nyie wafuasi wa Mwigulu mkisaidiwa na Job Ndungai kutaka kuwaaminisha Watanzania kuwa CHADEMA haifai, kwa hilo mmeula wa chuya, jipangeni upya kwani matendo yenu na maamuzi yenu mabaya ya kulinda udharimu wenu Watanzania wa chini kabisa huku mitaani na vitongojini wanaona na wataendelea kuona kama hamtajitambua kwa mbinu zenu chafu na kwa mbinu zenu hizo kila uchaguzi, mtakimbia vituo kabla ya matokeo kutangazwa
hahahaaa! Maumivu ya kichwa huanza pooole pole, dawa ni kuchagua Chadema tu
Haya wee ngoja tuone hiyo toboa toboa yako unayojigamba nayo. ila nafurahi umekiri kimeanzia kilimanjaro kwa hiyo ni cha wakilimanjaro. Mwaka 2014 kuna chaguzi za serikali za mitaa na 2015 kuna msema kweli....acha kimuhemuhe subiri ....utavuka daraja ukilifikia, ndipo tutaamini maneno yako... lakini nikuhakikishie tu kuwa hayo ni majigambo yasiyo na mashiko... angalia CDM kitakavyogaragazwa 2015