CHADEMA yafukuza mmoja Morogoro

CHADEMA yafukuza mmoja Morogoro

Inkognito

Member
Joined
Feb 13, 2011
Posts
86
Reaction score
108
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Morogoro kimemfukuza uanachama ndugu Dazza na kuwarudishia uanachama wao wale wote waliokuwa wamefukuzwa uanachama na Kamati Tendaji ya wilaya. Maamuzi ya kuwarudishia uanachama wao wale waliofukuzwa na Kamati Tendaji ya Wilaya ya Morogoro Mjini ulitolewa na Baraza la Uongozi la Mkoa chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Susan Kiwanga Baada ya Baraza hilo kujiridhisha kuwa Kamati Tendaji ya Wilaya ilikiuka Katiba, Kanuni na taratibu za Chama ikiwa ni pamoja na kuwafukuza uanachama wanachama wapatao 15 pasipo kuwapa nafasi ya kusikilizwa na kujitetea.

Mmoja kati ya wahanga wa maamuzi hayo ya Kamati Tendaji ya wilaya ni Mbunge Kivuri wa CHADEMA jimbo la Morogoro mjini mheshimiwa Amani Mwaipaja ambaye pia ni mwanasheria na mmiliki wa Blog ya MWAIPAJA BLOG. wito wangu kwa CHADEMA Morogoro ni kwamba wakati wa kuendekeza siasa za chuki na majungu umepitwa na wakati. Watanxzania wa leo ni waelewa kuliko wanavyofikiri CCM. Fanyeni kazi.
 
Dhambi ya kufukuzana ni kama kula nyama ya binadamu. ukishaanza hutaacha.
 
Susan kiwanga ameachiwa nafasi ya kuringa baada ya rejia mtema mana ndio alikuwa hasimu wake nkuu wa kisiasa morogoro
 
Mtu ukifukuzwa halafu unadanganywa umerudishwa huo ni unafiki,mana umeshachafuka
 
Mleta mada anaonekana ana ugonjwa wa kifafa, mana pale mwisho amemaliza na kibwagizo cha kuitaja ccm hata hakiendani kile alichokizungumza kwenye mada yake, ndio matatizo ya kukariri
 
Mleta mada anaonekana ana ugonjwa wa kifafa, mana pale mwisho amemaliza na kibwagizo cha kuitaja ccm hata hakiendani kile alichokizungumza kwenye mada yake, ndio matatizo ya kukariri

Imekuchoma ee...!!?
 
Dahh tumechoka filamu ya kufukuzana tuleteeni filamu mpya kama ya kisanga cha computer juzi ofisini kwa katibu wenu mkuu
 
Dahh tumechoka filamu ya kufukuzana tuleteeni filamu mpya kama ya kisanga cha computer juzi ofisini kwa katibu wenu mkuu

Wewe unaumwa nini? kuna kisanga gani cha computer? Kwanza unaijua computer ww? Tuondolee ujinga ujinga hapaaa!
 
kuna masalia yamepanga mstari hapo juu mreefu.....pumba tupu..
 
Mtu ukifukuzwa halafu unadanganywa umerudishwa huo ni unafiki,mana umeshachafuka
Pole mkuu, make huwa mnafurahi sana watu wakifukuzwa, sasa umeambiwa 15 wamerudishwa na mmoja ndo kafukuzwa roho inakuuma, unasikia maumivu na hasira, kwani vipi, acheni Chadema nao waongoze nchi mbona Ccm wanakiri wameshindwa?
 
Wtz bila kuadabishana mara nyingi tunataka kwenda kwa mazoea! kazi za siasa zinatutaka kutumikia mfumo (katiba) kwani bila hivyo yatakuwa yaleyale ya ccm!
 
Back
Top Bottom